KAIMU KATIBU MKUU WA UMOJA WA VIJANA WA CHAMA CHA MAPINDUZI (UVCCM) SHAKA HAMDU SHAKA AMEMTAJA MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR KUPITIA CUF MAALIM SEIF SHARIF HAMAD KUWA HAFAI KUWA RAIS WA ZANZIBAR AMA KUPEWA MADARAKA YA NGAZI ZA JUU KWANI AMEWAHI KUSHIRIKI VITENDO VYA UFISADI NA UFUJAJI WA FEDHA ZA UMAA WAKATI AKIWA WAZIRI KIONGOZI WA SSERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR.
SHAKA AMETOA MADAI HAYO JUZI KATIKA UZINDUZI MKUTANO WA KAMPENI ZA CCM JIMBO LA MWANAKWEREKWE MJINI UNGUJA ZILIZOFANYIKA KWENYE VIWANJA VYA IJTMAI YA ZAMANI, AMESEMA MGOMBEA HUYO WA URAIS WA ZANZIBAR KUPITIA TIKETI YA CUF NI KING'ANG'ANIZI WA MADARAKA ASIYETOSHEKA KWA NAFASI YEYOTE NA KWAMBA KUTAMANI KWAKE URAIS HUENDA ANA AJENDA YA SIRI DHIDI MAENDELEO YA ZANZIBAR NA MUSTAKABALI WAKE KISIASA , KIUCHUMI NA KIUSALAMA.
AMESEMA MWANASIASA HUYO AKIWA WAZIRI KIONGOZI AKICHUKUA SHILINGI MILIONI 100 KWA AJILI YA KUJITIBU MARADHI YA MATONSISI NCHINI BRUNEI HADI SASA HAJAONYESHA VILELELEZO , VIAMBATANSHO AU MCHANGANUO WA MATUMIZI YA FEDHA ZA UMMA, AMBAZO MPAKA SASA HAJAWAHI KUZITOLEA MAJIBU YA KURIDHISHA.
AIDHA SHAKA AMEMTUHUMU KIONGOZI HUYO KWAMBA FEDHA ZA SMZ ANAZOTUMIA KWA AJILI YA MATIBABU YAKE NI SHILINGI MILIONI 80 KWA SAFARI MOJA HUKO INDIA WAKATI ALISEMA NA KUAHIDI AKIWA SERIKALINI ANGETIBIWA NCHINI KATIKA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA, KAULI AMBAZO KWA SASA ZINAONYESHA WAZI KUWA NI KIONGOZI ASIYEFAA KUWAONGOZA WANANCHI.
KAIMU KATIBU MKUU HUYO AMESEMA MWANASIASA HUYO ANAPOSEMA ANA UWEZO WA KULETA MABADILIKO YA KIUCHUMI NA KULETA MAISHA BORA KWA WANANCHI WOTE KWA SIKU MIA MOJA ANAJITAFUTIA UMARUFU WA KISIASA NA WALA HANA UBAVU WA KUTEKELEZA HAYO KAMA ANAVYODAI KWENYE MAJUKWAA YA KISIASA.
SHAKA ALIMEMTUPIA LAWAMA MAALIM SEIF NA KUDAI MWAKA 1995 ALITAMKA KWAMBA AKISHINDA URAIS ATAUTAMBUA UFALME ULIOPINDULIWA ZBAR MWAKA 1964 NA KWAMBA ATAYAZAMISHA MAPINDUZI YA ZBR KATILA MKONDO WA NUNGWI.
AMEFAFANUA KUWA KUTOKANA NA KAULI PAMOJA NA VITENDO VYA MAALIM SEIF HANA NIA NJEMA YA KUJENGA UMOJA NA KULETA MAELEWANO BALI ANAKUSUDIA KUSHIKA URAIS ILI KUWAGAWA WANANCHI WA ZBR KWA MAPANDE YA UNGUJA NA UPEMBA.
AMEWATAKA WANANCHI KUAMKA , KUMTAZAMA NA KUTOMPIGIA KURA ZA NDIYO MGOMBEA HUYO URAIS WA CUF NA KUMHESBU KAMA NI ADUI NAMBA MOJA WA MISINGI YA UMOJA, UPENDO NA MSHIKAMANO WA KITAIFA ANAYEPIGANIA KUVIZA JUHUDI ZA VYAMA VYA ASP NA TANU.
AMEWATAKA WANANCHI WA MWANAKWEREKWE KUMCHAGUA MGOMBEA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGAMO DK JOHN MAGUFULI KUPITIA CCM NA DK ALI MOHAMED SHEIN KWA URAIS WA ZANZIBAR , MGOMBEA UWAKILISHI ABDALLA BUNGENI ALI KOMBO NA AHMADA ABDUL WAKIL MGOMBEA UBUNGE NA MADIWANI TOKA CCM .
No comments:
Post a Comment