tangazo

tangazo

Saturday, March 21, 2015

VIKUNDI VYA MAZOEZI YA VIUNGO VYAONGEZEKA ZANZIBAR


ZANZIBAR.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amezindua rasmi Kikundi cha Mazoezi ya Viungo cha wanawake kiliopo Mtaa wa Mwera { Mwera Fitness Club }KATIKA Wilaya ya Magharibi.

Uzinduzi huo  UMEFANYIKA katika viwanja vya michezo vya Skuli ya Regeza Mwendo na kushirikisha vikundi kadhaa vya mazoezi vya hapa Unguja wakijumuika pamoja na Viongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo chini ya Waziri wake Said Ali Mbarouk.

Balozi Seif aliyaongoza maandamano ya wana vikundi mbali mbali katika uzindui huo yaliyoanzia Mtofaani kupita Kituo cha Polisi cha Muembe Mchomeke na kuMALIZIA katika Viwanja vya Skuli ya Regeza Mwendo.

Akizungumza na wanavikundi hao Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aMEsema KUWA watu wengi wanaendelea kupoteza maisha na wengine kupata ulemavu wa viungo kutokana na kuugua maradhi ambayo yanaweza kuondoka kabisa iwapo jamii itajipangia utaratibu wa kufanya mazoezi.

Balozi Seif aMEsema KUWA ongezeko la wananchi kukimbilia Hospitalini kupata huduma za afya sambamba na Serikali kuu kuagiza dawa zinazogharimu fedha nyingi litapunguwa IWApo watu wengi watafanya mazoezi kila siku.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaomba wananchi kujipangia utaratibu wa kufanya mazoezi ya  kila siku mara wamalizapo ibada yao ya sala ya alfajiri kabla ya kuanza harakati zao za Kimaisha.

AMEfahamisha kwamba michezo inaleta urafiki baina ya vikundi na MIONGOZI MWA WATU ikiwa ni moja ya mafanikio makubwa katika kuimarisha nyanja za michezo na kuondosha maradhi mbali mbali.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliipongeza Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo kwa juhudi zake za kuhamasisha vikundi MBALI MBALI  nchini kushiriki katika mazoezi ya viungo.

Mapema Mwenyekiti wa zoni D ya Vikundi vya mazoezi Zanzibar Juma Khalid aMEsema KUWA Chama cha Vikundi vya Mazoezi Zanzibar { ZABESA } Kiliamua kuvigawa vikundi vya mazoezi Zanzibar kwa lengo la kupata ufanisi mzuri.

aMEsema KUWA Vikundi vya mazoezi ya viungo lengo lake kuu ni kuhakikisha kwamba sekta ya afya Nchini inapunguza uagizaji  wa dawa ambazo zina gharama kubwa kwa kuhamasisha watu kufanya mazoezi ya viungo.

Mwenyekiti huyo wa Zoni D ya vikundi vya mazoezi ya viungo aliwataka viongozi wa ngazi mbali mbali nchini wafanye mazoezi ili kuweka viwili viwili vyao katika hali ya afya.

Akimkaribisha Mgeni rasmi kwenye hafla hiyo Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk aMEsema KUWA Wizara hiyo itaendelea kuhakikisha kwamba Jamii yote inashawishika katika kufanya mazoezi.

Uzinduzi huo wa kikundi cha mazoezi cha Mwera Fitness Club uliambatana na mchango wa papo kwa papo kusaidia kuimarisha kikundi hicho kichanga kilichoanzishwa mwaka mmoja uliopita na kukifanya kuweka rikodi ya kufikia vikundi 60 vya mazoezi hapa Zanzibar.

No comments:

Post a Comment