ZANZIBAR.
RAIS WA ZANZIBAR DK. ALI MOHAMED SHEIN AMEPOKEA GWARIDE LA WANARIADHA
KUTOKA WILAYA KUMI ZA ZANZIBAR, NA KUWATAKA KUSHIRIKI VIZURI PAMOJA NA WAAMUZI
WA KUTENDA HAKI KATIKA MASHINDANO HAYO, ILI KUFUFUA VUGUVUGU LA MICHEZO KAMA
ILIVYOKUWA SIKU ZA
NYUMA.
MAPOKEZI HAYO YA GWARIDE LA WANARIADHA WA ZANZIBAR PAMOJA NA WAAMUZI WA
MASHINDANO HAYO, AMBAPO PIA LILIWASHIRIKISHA WANAMICHEZO WENYE ULEMAVU,
YALIYOFANYWA NA DK. SHEIN YALIFANYIKA KATIKA UWANJA WA AMAAN MJINI ZANZIBAR, NA
KUHUDHURIWA NA VIONGOZI MBALI MBALI WA SERIKALI, MICHEZO PAMOJA NA
WANAMICHEZO NA WANANCHI.
AKIWASALIMIA WANARIDHA HAO MARA BAADA YA KUPOKEA GWARIDE LAO LILILOPITA
MBELE YAKE, DR SHEIN ALIWATAKA
WANARIADHA HAO KUSHIRIKI VIZURI NA
KUSHINDANA KWA AMANI, KAMA LILIVYO JINA LA UWANJA HUO WANAOSHINDANIA MASHINDANO
HAYO WA AMAAN, AMBAO ULIASISIWA NA RAIS WA MWANZO WA ZANZIBAR ALMARHUUM
MZEE ABEID AMANI
KARUME.
MAPEMA WANARIADHA HAO WALIKULA KIAPO KUWA WATASHIRIKI NA KUSHINDANA KWA
KUFUATA SHERIA ZA SHIRIKISHO LA RIADHA LA AFRIKA NA DUNIA, SAMBAMBA NA KUFUATA
KANUNI ZOTE ZINAZOTAWALA MICHEZO HIYO, AMBAPO WAAMUZI NAO WALIAPA KUFUATA
SHERIA ZA KIMATAIFA NA KANUNI ZOTE BILA YA WOGA WALA UPENDELEA WOWOTE, HUKU
WAKIADIDI ZAIDI KUTENDA HAKI.
FAINALI ZA MASHINDANO HAYO ZINATARAJIWA KUFANYIKA KESHO JIONI, AMBAPO PIA
DK. SHEIN ANATARAJIWA KUWA MGENI RASMI.