tangazo

tangazo

Friday, December 26, 2014



ZANZIBAR.
RAIS WA ZANZIBAR DK. ALI MOHAMED SHEIN AMEPOKEA GWARIDE LA WANARIADHA KUTOKA WILAYA KUMI ZA ZANZIBAR, NA KUWATAKA KUSHIRIKI VIZURI PAMOJA NA WAAMUZI WA KUTENDA HAKI KATIKA MASHINDANO HAYO, ILI KUFUFUA VUGUVUGU LA MICHEZO KAMA ILIVYOKUWA  SIKU  ZA  NYUMA.

MAPOKEZI HAYO YA GWARIDE LA WANARIADHA WA ZANZIBAR PAMOJA NA WAAMUZI WA MASHINDANO HAYO, AMBAPO PIA LILIWASHIRIKISHA WANAMICHEZO WENYE ULEMAVU, YALIYOFANYWA NA DK. SHEIN YALIFANYIKA KATIKA UWANJA WA AMAAN MJINI ZANZIBAR, NA KUHUDHURIWA NA VIONGOZI MBALI MBALI WA SERIKALI, MICHEZO PAMOJA NA WANAMICHEZO  NA  WANANCHI.
                                                      
AKIWASALIMIA WANARIDHA HAO MARA BAADA YA KUPOKEA GWARIDE LAO LILILOPITA MBELE YAKE,  DR SHEIN ALIWATAKA WANARIADHA HAO KUSHIRIKI VIZURI  NA KUSHINDANA KWA AMANI, KAMA LILIVYO JINA LA UWANJA HUO WANAOSHINDANIA MASHINDANO HAYO WA AMAAN, AMBAO ULIASISIWA NA RAIS WA MWANZO WA ZANZIBAR ALMARHUUM MZEE  ABEID  AMANI  KARUME.

MAPEMA WANARIADHA HAO WALIKULA KIAPO KUWA WATASHIRIKI NA KUSHINDANA KWA KUFUATA SHERIA ZA SHIRIKISHO LA RIADHA LA AFRIKA NA DUNIA, SAMBAMBA NA KUFUATA KANUNI ZOTE ZINAZOTAWALA MICHEZO HIYO, AMBAPO WAAMUZI NAO WALIAPA KUFUATA SHERIA ZA KIMATAIFA NA KANUNI ZOTE BILA YA WOGA WALA UPENDELEA WOWOTE, HUKU WAKIADIDI  ZAIDI  KUTENDA HAKI.

FAINALI ZA MASHINDANO HAYO ZINATARAJIWA KUFANYIKA KESHO JIONI, AMBAPO PIA DK. SHEIN ANATARAJIWA  KUWA  MGENI RASMI.

No comments:

Post a Comment