ZANZIBAR.
MAKAMU WA
PILI WA RAIS WA ZANZIBAR AL-HAJJ BALOZI
SEIF ALI IDDI AMETEMBELEA MSIKITI MKONGWE ZAIDI KATIKA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI ULIOPO MICHEWENI
MKOA WA KASKAZINI PEMBA.
AKISALIMIANA
NA UONGOZI WA KAMATI YA MSIKITI HUO PAMOJA NA BAADHI YA WAANZILISHI WAKE, BALOZI SEIF ALIWAKUMBUSHA WAUMINI
WA DINI YA KIISLAMU KUENDELEA KUSHIKAMANA KAMA MAAMRISHO YA DINI YAO
YANAVYOELEKEZA.
AMESEMA KUWA
DINI YA KIISLAMU IMEKUWA IKISISITIZA
SUALA LA AMANI, JAMBO AMBALO LITAKAPOFUATWA NA KUTEKELEZWA IPASAVYO HUSAIDIA KUWAPA UTULIVU WANANCHI
KUFANYA IBADA NA SHUGHULI ZAO KAMA
KAWAIDA.
AIDHA BALOZI SEIF AMEWAASA WAISLAM KUWA MAKINI
KATIKA KUCHANGANYA DINI NA SIASA KAMA BAADHI YA WATU HUSUSAN WANASIASA KUJARIBU KUSHAWISHI WATU
KUFANYA HIVYO, MATOKEO YAKE NI KUANZISHA CHECHE ZA UHASAMA NA WASI WASI KATIKA
JAMII.
MSIKITI WA
IJUMAA WA MICHEWENI MJINI UNAKISIWA KUJENGWA TOKEA KARNE YA 14, KIPINDI AMBACHO
KILIKUWA NA HARAKATI ZA KUSAMBAZWA KWA
DINI YA KIISLAMU KATIKA MWAMBAO WA AFRIKA MASHARIKI.
No comments:
Post a Comment