tangazo

tangazo

Monday, November 23, 2015

Upinzani washinda uchaguzi Argentina

Mgombea wa chama cha upinzani cha Conservative Mauricio Macri amethibitishwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais Argentina, huku mgombea wa chama tawala akikubali kushindwa.
Baada ya karibu kura zote kuhesabiwa, Bw Macri alikuwa na 52% akilinganishwa na Daniel Scioli aliyepata 48%.

Shangwe na vigelegele vilitanda katika makao makuu ya kampeni ya Bw Macri baada ya kura za maoni runingani kuonyesha alikuwa ameshinda.

Bw Macri, meya wa zamani wa Buenos Aires, alikuwa ameshindwa na Scioli, ambaye ni gavana wa mkoa wa Buenos Aires, kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi Oktoba.

Lakini wote wawili hawakuweza kushinda moja kwa moja na duru ya pili ikaandaliwa, mara ya kwanza kwa uchaguzi kuingia duru ya pili katika historia ya Argentina.

Ushindi wa Bw Macri ndio wa kwanza katika zaidi ya mwongo mmoja kwa upinzani wenye kuegemea siasa za mrengo wa kati kulia.

Aliingia kwenye uchaguzi huo wa Jumapili akiwa mbele kwa kura za maoni na alikuwa ameahidi kusisimua uwekezaji na kukabili changamoto za kiuchumi, uhalifu na ufisadi.

Bw Macri ni mwana wa mmoja wa watu tajiri zaidi Argentina na alifanya kazi kwa muda mrefu kama mwanabiashara kabla ya kujitosa katika siasa.

Bw Scioli ni mshirika wa karibu wa Rais anayeondoka Cristina Fernandez de Kirchner
Bw Scioli, ambaye ni mwandani mkuu wa Rais anayeondoka Cristina Fernandez de Kirchner, alikuwa ametarajiwa kushinda duru ya kwanza iliyofanyika Oktoba kwa kura nyingi lakini hilo halikuwa.

DK.SHEIN APIGA MARUFUKU MIFUGO MITAANI ZANZIBAR.


NA MWINYI SADALLAH

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, amelitaka Baraza la Manispaa Zanzibar kuimarisha shughuli za usafi wa mazingira, pamoja na kudhibiti mifungo kuingia katikati ya mji huo.

Dk Shein alitoa agizo hilo alipokuwa katika ziara ya kukagua miradi ya ujenzi inayogharamiwa kwa mkopo wa Benki ya Dunia ukiwamo ujenzi wa ukuta wa ufukwe wa Forodhani na mtaro wa maji machafu katika eneo la Mnazi Mmoja, Zanzibar jana.

Alisema wakati Zanzibar ikiwa katika mchakato wa kufikia sifa za kuwa jiji, lazima Baraza la Manispaa liongeze kasi ya usafi ikiwamo uhifadhi wa mazingira ya mji pamoja na udhibiti wa  majitaka visiwani humo.

Alisema haitoi picha nzuri  kuona mifugo bado inaonekana ikiranda mitaani wakati watendaji wametakiwa kuondoa tatizo hilo kwa muda mrefu sasa bila ya utekelezaji kuonekana.

“Lazima tuongeze jitihada za usafi wakati huu tukiwa katika kuelekea kufikia sifa na vigezo vya Zanzibar kuwa jiji,” alisema.

Rais Dk. Shein alisema mradi wa kuboresha mji wa Zanzibar unaofadhiliwa na mkopo kutoka Benki ya Dunia una umuhimu mkubwa katika kuimarisha shughuli za usafi katika manispaa ya mji huo na miji ya Chakechake na Wete, Pemba.

Aliwataka watendaji kuhakikisha miradi hiyo inakuwa endelevu ili lengo lake liweze kuonekana la kuleta mabadiliko makubwa ya usafi wa mji huo.
CHANZO: NIPASHE

Sunday, November 22, 2015

NAIBU WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AWAANDALIA CHAKULA MADAKTARI KUTOKA HISPANIA

 Profesa Jose Pinquet kulia akitambulisha Timu ya Madaktari wanaotoa huduma za Matibabu ya Uti wa Mgongo na Ubongo katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi mmoja kwa Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo.
 Baadhi ya Madaktari wanaotoa huduma za Matibabu ya Uti wa Mgongo na Ubongo katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi mmoja wakipata Cahakula cha Usiku kilichoandaliwa ni Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo.
 Profesa Jose Pinquet akizungumza mara baada ya Chakula cha usiku kilichoandaliwa kwa ajili yao ambapo pia alishukuru mashirikiano wanayopewa na Madaktari Wazawa katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Ocean View.
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na Madaktari wa kujitolea kutoka Hispatinia mara baada ya Chakula cha usiku alichowaandalia kwa lengo la kuwashukuru kutokana na mchango wao mkubwa wanaoutoa katika sekta ya Afya Zanzibar, hafla hiyo ilifanyika Hoteli ya Ocean View.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar

"UCHAGUZI HURU NA WA HAKI, BILA YA WAANDISHI WA HABARI KUZINGATIA MAADILI NI NDOTO"

Mkuu wa Chuo cha Habari Zanzibar Dkt. Aboubakar Rajab akitoa hutuba ya ufunguzi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Ally Mwinyikai katika Mkutano Mkuu wa Wadau wa Jumuiya ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) uliofanyika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean mjini Zanzibar ambapo alisitiza wanahabari kuzingatia maadili ya kazi zao. Kulia ni Katibu wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Chande Omar na kushoto ni Mwenyekiti wa ZPC Abdallah Mfaume.
Katibu wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Chande akitoa Mada ya umuhimu wa kuzingatia Maadili kwa Wanahabari katika fani yao.
Mkulima kutoka kikundi cha Ushirika cha Bambi Mwaka Saburi akichangia katika Mkutano wa Wadau wa ZPC uliofanyika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean mjini Zanzibar ambapo alishauri Wanahabari kuandika zaidi habari za Vijijini bada ya mijini pekee.
Makamu wa Rais wa Chama cha Siasa ADA-TADEA akichangia katika Mkutano wa Wadau wa Mkutano wa Wadau wa ZPC uliofanyika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean mjini Zanzibar.
Katibu wa Jumuiya ya Waandishi wa Habari Zanzibar (ZPC) Faki Mjaka akisoma maazimio ya Mkutano wa Wadau wa ZPC uliofanyika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean mjini Zanzibar.
aadhi ya Washiriki wa Mkutano wa Wadau wa Zanzibar Press Club ZPC wakiwa katika Picha ya pamoja na Mgeni rasmi wa Mkutano huo Dkt. Aboubakar Rajab wakatikati waliokaa huko Hoteli ya Zanzibar Ocean mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.


Wanahabari wametakiwa kuendelea kutii Sheria zilizopo zinazoongoza mwenendo wa utoaji wa habari nchini, huku Taasisi za kihabari zikiendelea kufuatilia upatikanaji wa sheria Bora za habari zinazoendana na wakati uliopo.

Hayo yameelezwa na Katibu wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Chande Omar alipokuwa akiwasilisha Mada katika Mkutano Mkuu wa Wadau wa Jumuiya ya Waandishi wa Habari Zanzibar ZPC uliofanyika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean mjini Zanzibar.
Amesema licha ya kuwepo kwa baadhi ya Sheria za habari zilizopitwa na wakati, ni vyema Wanahabari kuziheshimu na kuzitii huku juhudi mbalimbali zikifanywa na Wadau kuondoa Sheria hizo.
Chande amefahamisha kuwa Taasisi kama Vile Baraza la Habari Tanzania, Tume ya Utangazaji na Jumuiya ya Waandishi wa Habari Zanzibar ZPC ni miongoni mwa Taasisi ambazo zinafanya kazi za kuwepo kwa Sheria zinaendana na wakati kwa maslahi mapana ya Taifa.
Aidha katika Mkutano huo uliojumuisha Washiriki kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali na Binafsi maazimio mbalimbali yalipitishwa ikiwemo Wamiliki wa Vyombo vya Habari na Waaandishi kwa ujumla kuzingatia Weledi katika utekelezaji wa majukumu yao.
Azimio jingine ni kuhakikisha kuwa Taasisi kama Vile Baraza la Habari Tanzania, Tume ya Utangazaji na Jumuiya ya Waandishi wa Habari Zanzibar ZPC zinashiriki kikamilifu katika kuhamasisha upatikanaji wa Maslahi bora kwa Wanahabari ili kuwaepusha kupokea Zawadi kutoka Vyanzo vya habari ambazo hupelekea kukiuka maadili yao.
Aidha wameazimia kujiepusha na Ushabiki wa Kisiasa ili kuepuka upendeleo wa habari wanazojitoa kwa jamii.
Mmoja wa Wachangiaji kutoka Jumuiya ya Wakulima Mpwapwa amewaomba Waandishi wa habari kuandika pia habari za watu wa shamba badala ya kuandika habari zinazohusu watu wa mijini pekee.
Ametoa mfano kwamba katika uchaguzi Mkuu uliopita habari zilizoandikwa zilihusu Watu wa Mijini ambapo kwa  upande wa Vijijini Waandishi walishindwa kuonekana kwenda kuchukua habari.
Hata hivyo Washiriki wa Mkutano huo pia Waliafiki wazo hilo na kuazimia kufanya kazi kizalendo na kushirikisha makundi yote ya kijamii ikiwemo kuandika habari za Vijijini ili kuibua Fursa na changamoto zinazowakabili.
Akitoa hutuba ya Ufunguzi Mkuu wa Chuo cha Habari Zanzibar Dkt. Aboubakar Rajab kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Ally Mwinyikai alisisitiza wanahabari kuzingatia maadili ya kazi zao ili waheshimike katika jamii.
Amesema kukosekana kwa Maadili ya Habari hupelekea Migogoro mingi ikiwemo kuzalisha chuki na fitna miongoni mwa jamii husika.
Jumuiya ya Waandishi wa Habari Zanzibar hufanya Mkutano Mkuu wa Wadau wake kila mwaka na kujadili mada kulingana na wakati husika ambapo katika Mkutano huo Walijadili umuhimu wa Waandishi kuzingatia Maadili katika kupatikana uchaguzi huru na Wahaki.

Saturday, November 21, 2015

PESA ZILIZOCHANGWA KWA AJILI YA HAFLA YA WABUNGE ZIKANUNUE VITANDA MUHIMBILI

Baada ya kulihutubia na kulizindua bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt JOHN POMBE MAGUFULI amehudhuria hafla fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya wabunge katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma na kuagiza fedha zilizochangwa kwa ajili ya kugharamia hafla hiyo zipelekwe Katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kununulia vitanda vya wagonjwa.

Mheshimiwa Magufuli ametoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa kuwa wadau mbalimbali wamechanga kiasi cha shilingi milioni 225 kwa ajili ya kugharamia hafla ya wabunge katika siku ya uzinduzi wa Bunge.

 Dkt Magufuli amesema alipata taarifa za kuwepo kwa michango hiyo ya fedha na kutoa maelekezo kuwa zitumike kwa kiasi kidogo kwa ajili ya hafla hiyo na sehemu kubwa zipelekwe katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili zikatumike kununulia vitanda na hivyo kupunguza tatizo la wagongwa wanaolala chini kutokana na uhaba wa vitanda unaikabili hospitali hiyo.

 “Nilipoambiwa kwamba zimechangwa shilingi milioni 225 zimekusanywa kwa ajili ya sherehe, nikasema fedha hizo zipelekwe katika hospitali ya Taifa Muhimbili zikasaidie kununua vitanda” alisema Dkt Magufuli na kusisitiza kuwa “kwa kufanya hivyo tutakua tumejinyima sisi wenyewe lakini tutakua tumewanufaisha wenzetu ambao wanamatatizo makubwa yanayoweza kutatuliwa kwa fedha hizo”.

 Awali akitoa taarifa ya michango hiyo Ofisa wa Spika wa Bunge Bwana SAID YAKUBU amesema jumla michango iliyopatikana na shilingi milioni 225 na kwamba fedha zilizotumika katika hafla hiyo ni shilingi milioni 24 tu baada ya kuzingatia maagiza ya Rais Magufuli.

 Katika Hafla hiyo Rais Magufuli amekabidhi vyeti vya kutambua mchango wa wadau waliochangia fedha wakiwemo Benki za NMB, CRDB na Benki ya Afrika pamoja na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya PSPF na PPF.

 Gerson Msigwa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano IKULU November 20, 2015

SHIRIKISHO LA VYUO VIKUU CCM



KIDUMU  CHAMA CHA MAPINDUZI.
TAARIFA  KWA VYOMBO VYA  HABARI  JUU YA KUPORWA KWA USHINDI WA CHAMA CHA MAPINDUZI  KULIKOSABABISHWA NA TUME  YA UCHAGUZI KWA KUSHIRIKIANA NA CHAMA CHA  WANANCHI CUF  KATIKA UCHAGUZI WA OKTOBA  25, 2015.
   Awali ya yote shirikisho la  vyuo vya elimu ya juu  CCM –    
   Zanzibar  linapenda kuchukua fursa hii , kumshukuru     
   M/Mungu  kwa kutujaalia nchi yetu  kuwa katika   hali ya  
   amani  na  utulivu.
Pili, tunachukua fursa hii  kuwashukuru nyinyi  vyombo vya  habari  kwa mahudhurio yenu  mazuri kuja  kuchukua taarifa kwa  lengo  la kuwahabarisha umma  juu ya mustakbal wa nchi yetu.
Shirikisho la vyuo vya elimu ya juu CCM  -  Zanzibar  lina masikitiko makubwa juu ya vitendo   zilivyofanywa  na tume  ya uchaguzi ya Zanzibar  kwa kushirikiana  na chama cha  CUF  katika kupora ushindi wa chama cha mapinduzi , hii  ni  kutokana na kua mpaka matokeo ya kura  za  urais kwa majimbo yaliotangazwa Chama Cha Mapinduzi   kilikua kinaongoza.
Hivyo,  kutokea kwa dosari katika baadhi ya majimbo  sio sahihi kwa tume ya uchaguzi kuinyima CCM ushindi wake na kutomtangaza Dk. Ali Mohamed Shein.
 Sisi wanataaluma kutoka shirikisho la vyuo vya elimu ya juu Zanzibar   tunalaani sana     kitendo   hicho  na tunaomba vyombo vinavyohusika kuchukua hatua kwa mujibu wa sharia zilizopo.
Kuna  ushahidi wa kutosha  kuwa tume ya uchaguzi Zanzibar  ilikua kitu kimoja na wapinzani kwa sababu zifuatazo ;-
-         Moja,  kitendo cha tume  ya uchaguzi Zanzibar  (ZEC)  kushindwa kumchukulia hatua  mgombea wa urais  wa CUF  Maalim Seif Sharif Hamad  kuishindikiza tume   imtangaze  yeye kua ni mshindi  alikwishavunja  katiba ya nchi  kwa mujibu wa ibara  ya 119  kifungu kidogo cha  (12)  ambacho kinaeleza kua
‘’  katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti    ya katiba hii , tume ya uchaguzi haitalazimika kufuata  amri au maagizo ya mtu yeyote au idara yoyote ya   serikaIi,  au  maoni ya chama cha siasa ‘’
-         Pili, kuna vifaa vya   uchaguzi   vimekamatwa katika   nyumba  za wafuasi wa CUF  ikiwemo vitabu  32  vya  karatasi za kupigia kura  vifaa hivi  vimekamatwa katika nyumba  ya mfuasi wa CUF  ilioko  Kijichi Spice  na hakuna  hatua zozote   ambazo tume ya uchaguzi  wamezichukua badala yake   kesi  imeachwa  katika kituo cha  Polisi Bububu.

 Aidha ,  sisi wanataaluma tunalaani vikali  kitendo   cha  baadhi ya watu  pamoja na wanasheria kuipotosha  jamii  kwa kusema kuwa  kitendo cha kufutwa kwa uchaguzi   ni batili kwani  M/ kiti wa tume  ya uchaguzi Zanzibar  amefuata  sheria zote pamoja  na katiba ya nchi  kufuta uchaguzi  kwa mfano sheria ya uchaguzi ibara ya 3  kifungu kidogo (1) kinaeleza  hivi  “ kanuni , maelezo  na matangazo yote ambayo tume ina  mamlaka ya kutunga au kutoa itajaaliwa kuwa yametungwa au yametolewa kisheria kama yametiwa sahihi na Mwenyekiti wa Tume au mkurugenzi wa uchaguzi” Kanuni  hii  inaeleza  uwezo  wa tume  kufuta uchaguzi.
Sasa wao wanaozusha  kwa   kusema  wajumbe/ makamishna  wa tume hawakushirikishwa   jambo hilo  sio la kweli  na tunawaomba makamishna  wa CUF  wawaeleze ukweli   wafuasi wao na viongozi wao  na sio  kuwapotosha  kwani kuna taarifa za siri ambazo Kamshina wa CUF Ayoub Bakar amezifanya kwa kushirikina na wenzake kuhujumu uchaguzi mfano:
1.   Tunafahamu kuwa Ayoub Bakari alimuahidi M/Kiti wa tume ya uchaguzi JECHA SALUM JECHA shilling MILION MIA MOJA (100,000,000/=) ili asaidie CUF kushinda , pia Ayoub alimtaka mkurugenzi wa ZEC Salum Kassim Ali aseme anachotaka ili nae asaidie CUF kushinda
2.   Siku ya uchaguzi vyama vingi vilipelekaa malalamiko yao mbali mbali kuhusiana na kutoridhishwa kwao na matokeo ya uchaguzi ule,  lakini ZEC ilisikiliza malalamiko ya Mansori tu na kuyatolea uamuzi wa upendeleo, uamuzi huo ulifanywa na Nassor Khamis na sio M/kiti.
3.   Karatasi za uchaguzi alichapisha Ayoub badala ya tume na serikali, Ayoub alitumia nafasi hio akishirikiana na Maalim Seif kuchapisha baloti paper za ziada.
4.    
5.   ZEC imewazuwia mawakala wa CCM ID za kushiriki uchaguzi mpaka mchana hilo limetoa mwanya kwa CUF kuitumia nafasi hio kwa manufaa yao.
6.   Jaji Abdulhakim Ameir Issa kubainika wazi wazi kua na mapenzi na CUF wakati yeye amwekwa katika tume hiyo kiserikali na zaidi katika masuala ya kisheria.
7.   Pemba nusu ya waopiga kura walipigiiwa na watu maalum bila ya sababu ya msingi, na pia kura zilizopigwa hazifanani na majumuisho, na kuna baadhi  ya kura zimetiwa katika mifuko ya karatasi badala ya mifuko ya plastki iliyowekwa na tume ya uchaguzi, Mifuko ya tume iliosaniwa.
Sambamba na hayo ,  tunawaomba  waangalizi wa nje  wasiwe  sehemu ya kutusababishia  mgogoro kwa kushindikiza  mambo ambayo katiba  na sheria zetu  zimeweka bayana.
Kwa upande  wa tamko  la viongozi wa ukawa  lililotolewa jumapili ya tarehe 15 November 2015  la kuishindikiza  tume ya uchaguzi   Zanzibar  kuitaka  imtangaze maalim Seif   halina msingi  na linapingana  na katiba  ya Zanzibar  ibara ya 119 kifungu kidogo cha 12. Hivyo  sisi wanataluma  tunasema  wakae kimya  na wasiipotoshe  jamii  ya  Watanzania.

Kwa kumalizia , tunaisubiri tume   itangaze tarehe nyengine    ya uchaguzi  lakini tunatoa angalizo  , tunaitaka Tume ya Uchaguzi  Zanzibar  isimamie   katiba na sheria  za nchi na kufuata  maadili,  na endapo itaendelea kushirikiana  na chama cha CUF  tunasema sisi wasomi  hatutokubali na tume itabeba jukumu  kubwa kwa hali yoyote   itakayotokezea.

Vile vile, Tunawaomba wasomi wenzetu  pamoja na wanachama wa  CCM  tuwe watulivu lakini tujiandae  kujitokeza kwa   wingi  mara  baada ya kutangazwa  kwa tarehe ya  uchaguzi  kama  walivijitokeza  kwa wingi katika uchaguzi wa Oktoba 25 , 2015  lakini pia wanachama   wetu wajiandae  kusherehekea ushindi kwani  katiba ya CCM  ibara ya 5  (i) inasema ‘’ Ushindi ni Lazima ‘’
Tunatoa wito kwa wanachama wa CCM na wazanzibar kwa ujumla kua makini na chama cha upinzani kwani imeonekana dhahiri kua viongozi wake hawana nia njema kwani kitendo cha mgombea wao kujitangazia mshindi kwa nini kisherekewe nchini Maskati na London?
Pia, tunalaani kitendo cha wabunge  kutoka kambi ya ukawa kwa kitendo cha utomvu wa nidhamu ndani ya chombo kitakatifu na mbele ya viongozi wetu wa taifa letu, kwani wamejidhihirisha wazi wazi kua wao ni watovu wa nidhamu na hawafai kuongoza hata kikundi cha watu wachache.
Mwisho ,  tunaomba  wanasheria wetu  kupitia Afisi  kuu ya CCM waendelee kuelimisha  jamii ili  kuepusha   upotoshaji unaofanywa na  wapinzani.

Vile vile, tunawapongeza wanachama wa Chama cha Mapinduzi kwa uvumilivu wao na kutovunja sheria kwani licha ya kua hadi  matokeo ya majimbo 31 ya Unguja  yanatoka yalikua yanaonesha kua Chama cha Mapinduzi kilikua kinaoongoza lakini mwisho uchaguzi ulifutwa.
Kitendo cha Mgombea wa urais kupitia CUF  Maalim Seif  Sharif Hamad kujitangaza mshindi kiliingiza nchi  yetu katika majaribio ya uvunjifu wa Amani lakini tunavipongeza sana  sana sana vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuweza kusimamia Amani na utulivu wa nchi kabla na baada ya uchaguzi kwani kuna mifano ya nchi kadhaa haziko salama hadi sasa.
Hata hivyo ,  shirikisho  la  vyuo vya elimu ya juu  CCM – Zanzibar   linachukua fursa hii kumpongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Dk Joh’n  Pombe Joseph Magufuli na Makamu wake Samia Suluhu Hassan  kwa kuchaguliwa  na wananchi  wa  Tanzania  lakini pia  tunaridhishwa na namna  alivyoanza kazi kwa kutoa houtuba mwanana iliyolenga kuwasaidia wananchi wa hali ya chini katika kipindi chake cha awamu ya tano cha serikali ya Jamuhuri ya mungano wa Tanzania kwani, ile kauli mbiyu yake ya ‘’Hapa  Kazi  tuu ‘’  inajidhihirisha wazi wazi.
Mwisho kabisa, tunachukua fursa kumpongeza Mhe. Kassim Majaaliwa kwa kuteuliwa kuwa waziri Mkuu na  sambamba na kupitishwa na bunge kwa zaidi ya  73%  ya wabunge wote waliopiga kura.
Ahsanteni  kwa kunisikiliza.


‘’ Mungu   ibariki  Zanzibar’’
‘’Mungu ibariki Tanzania ‘’
‘’Mungu ibariki Afrika”

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI






Imetiwa Saini na Katibu,


………………………………………..

KNY: Shirikisho la Vyuo Vya Elimu Ya Juu CCM- Zanzibar.
21/11/2015.

Friday, November 20, 2015

MAJALIWA NA UTEUZI WA KUSHTUKIZWA

Waziri Mkuu Mteule, Majaliwa Kassim Majaliwa, amesema kuwa hakuna na taarifa za uteuzi wake hadi aliposikia na kuona kwenye luninga na kulazimika kwenda bungeni.

Akizungumza wakati wa kuwashukuru wabunge katika ukumbi wa Bunge jana mjini Dodoma, Majaliwa alisema nafasi hiyo hakuitegemea, lakini ameipokea na yupo tayari kufanya kazi.

“Sikuwa na maandalizi yoyote, hata karatasi niliyonayo sijaandika chochote, lakini imeniongoza kutambua uwepo wenu na mchango mkubwa, nawahakikishia kuwa jukumu nililopewa na ambalo nitapewa, kama mwakilishi wa wananchi, nitashirikiana nanyi katika kufanya kazi zetu,” alisema.

Aidha, alimshukuru Mungu na Rais kwa kumteua pamoja na wabunge kumthibitisha kwa kura nyingi kushika nafasi hiyo.

“Mheshimiwa Spika, nilikuona nikiwa naangalia kwa njia ya televisheni ulipokuwa unaendesha zoezi la ufunguzi wa bahasha zote tatu...nawashukuru wabunge wote kwa kuridhia, kupiga kura nyingi jina langu, tuweze kufanya kazi kwa pamoja ya kuwatumikia Watanzania.”

Majaliwa aliahidi ushirikiano wa hali ya juu bila kujali vyama kwa kuwa ni wawakilishi wa wananchi wa Tanzania na watafanya kazi kwa pamoja ya ufuatilia wa shughuli za maendeleo na kuisimamia serikali ikiwa ni pamoja na kusikikiza ushauri wa wabunge katika kufanyakazi za kila siku.

KUANZA KAZI KARIBUNI
Majaliwa alisema baada ya kuapishwa atafanya ziara katika majimbo mbalimbali ili kuona changamoto zilizopo, maendeleo waliyofikiwa na kuwasikia Watanzania wana mawazo gani.


HALI ILIVYOKUWA BUNGENI
Majaliwa aliingia bungeni huku wabunge wa CCM wakipiga makofi hadi alipokaa kwenye kiti cha nyuma kabisa.
Kabla ya kushukuru, baada ya kupigiwa kura za kuthibitishwa, alisalimiana na wabunge wa CCM na Upinzani na kwenda moja kwa moja kuwashukuru.

ATHIBITISHWA KURA 73.5%
Awali akisoma matokeo ya uthibitisho huo, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilila, alisema Majaliwa alipata kura za ndiyo 258 (asilimia 73.5), kura 91 za hapana (asilimia 25.9) na kura mbili ziliharibika. Baada ya kuthibitishwa kwa kura hizo, Spika wa Bunge, Job Ndugai, alimkaribisha Majaliwa atoe shukrani kwa wabunge.

Majaliwa katika hotuba yake fupi, alimshukuru Rais John Magufuli kwa imani aliyoionyesha mwake na kuwashukuru wabunge kwa kumthibitisha.
CHANZO: NIPASHE