tangazo

tangazo

Saturday, November 21, 2015

SHIRIKISHO LA VYUO VIKUU CCM



KIDUMU  CHAMA CHA MAPINDUZI.
TAARIFA  KWA VYOMBO VYA  HABARI  JUU YA KUPORWA KWA USHINDI WA CHAMA CHA MAPINDUZI  KULIKOSABABISHWA NA TUME  YA UCHAGUZI KWA KUSHIRIKIANA NA CHAMA CHA  WANANCHI CUF  KATIKA UCHAGUZI WA OKTOBA  25, 2015.
   Awali ya yote shirikisho la  vyuo vya elimu ya juu  CCM –    
   Zanzibar  linapenda kuchukua fursa hii , kumshukuru     
   M/Mungu  kwa kutujaalia nchi yetu  kuwa katika   hali ya  
   amani  na  utulivu.
Pili, tunachukua fursa hii  kuwashukuru nyinyi  vyombo vya  habari  kwa mahudhurio yenu  mazuri kuja  kuchukua taarifa kwa  lengo  la kuwahabarisha umma  juu ya mustakbal wa nchi yetu.
Shirikisho la vyuo vya elimu ya juu CCM  -  Zanzibar  lina masikitiko makubwa juu ya vitendo   zilivyofanywa  na tume  ya uchaguzi ya Zanzibar  kwa kushirikiana  na chama cha  CUF  katika kupora ushindi wa chama cha mapinduzi , hii  ni  kutokana na kua mpaka matokeo ya kura  za  urais kwa majimbo yaliotangazwa Chama Cha Mapinduzi   kilikua kinaongoza.
Hivyo,  kutokea kwa dosari katika baadhi ya majimbo  sio sahihi kwa tume ya uchaguzi kuinyima CCM ushindi wake na kutomtangaza Dk. Ali Mohamed Shein.
 Sisi wanataaluma kutoka shirikisho la vyuo vya elimu ya juu Zanzibar   tunalaani sana     kitendo   hicho  na tunaomba vyombo vinavyohusika kuchukua hatua kwa mujibu wa sharia zilizopo.
Kuna  ushahidi wa kutosha  kuwa tume ya uchaguzi Zanzibar  ilikua kitu kimoja na wapinzani kwa sababu zifuatazo ;-
-         Moja,  kitendo cha tume  ya uchaguzi Zanzibar  (ZEC)  kushindwa kumchukulia hatua  mgombea wa urais  wa CUF  Maalim Seif Sharif Hamad  kuishindikiza tume   imtangaze  yeye kua ni mshindi  alikwishavunja  katiba ya nchi  kwa mujibu wa ibara  ya 119  kifungu kidogo cha  (12)  ambacho kinaeleza kua
‘’  katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti    ya katiba hii , tume ya uchaguzi haitalazimika kufuata  amri au maagizo ya mtu yeyote au idara yoyote ya   serikaIi,  au  maoni ya chama cha siasa ‘’
-         Pili, kuna vifaa vya   uchaguzi   vimekamatwa katika   nyumba  za wafuasi wa CUF  ikiwemo vitabu  32  vya  karatasi za kupigia kura  vifaa hivi  vimekamatwa katika nyumba  ya mfuasi wa CUF  ilioko  Kijichi Spice  na hakuna  hatua zozote   ambazo tume ya uchaguzi  wamezichukua badala yake   kesi  imeachwa  katika kituo cha  Polisi Bububu.

 Aidha ,  sisi wanataaluma tunalaani vikali  kitendo   cha  baadhi ya watu  pamoja na wanasheria kuipotosha  jamii  kwa kusema kuwa  kitendo cha kufutwa kwa uchaguzi   ni batili kwani  M/ kiti wa tume  ya uchaguzi Zanzibar  amefuata  sheria zote pamoja  na katiba ya nchi  kufuta uchaguzi  kwa mfano sheria ya uchaguzi ibara ya 3  kifungu kidogo (1) kinaeleza  hivi  “ kanuni , maelezo  na matangazo yote ambayo tume ina  mamlaka ya kutunga au kutoa itajaaliwa kuwa yametungwa au yametolewa kisheria kama yametiwa sahihi na Mwenyekiti wa Tume au mkurugenzi wa uchaguzi” Kanuni  hii  inaeleza  uwezo  wa tume  kufuta uchaguzi.
Sasa wao wanaozusha  kwa   kusema  wajumbe/ makamishna  wa tume hawakushirikishwa   jambo hilo  sio la kweli  na tunawaomba makamishna  wa CUF  wawaeleze ukweli   wafuasi wao na viongozi wao  na sio  kuwapotosha  kwani kuna taarifa za siri ambazo Kamshina wa CUF Ayoub Bakar amezifanya kwa kushirikina na wenzake kuhujumu uchaguzi mfano:
1.   Tunafahamu kuwa Ayoub Bakari alimuahidi M/Kiti wa tume ya uchaguzi JECHA SALUM JECHA shilling MILION MIA MOJA (100,000,000/=) ili asaidie CUF kushinda , pia Ayoub alimtaka mkurugenzi wa ZEC Salum Kassim Ali aseme anachotaka ili nae asaidie CUF kushinda
2.   Siku ya uchaguzi vyama vingi vilipelekaa malalamiko yao mbali mbali kuhusiana na kutoridhishwa kwao na matokeo ya uchaguzi ule,  lakini ZEC ilisikiliza malalamiko ya Mansori tu na kuyatolea uamuzi wa upendeleo, uamuzi huo ulifanywa na Nassor Khamis na sio M/kiti.
3.   Karatasi za uchaguzi alichapisha Ayoub badala ya tume na serikali, Ayoub alitumia nafasi hio akishirikiana na Maalim Seif kuchapisha baloti paper za ziada.
4.    
5.   ZEC imewazuwia mawakala wa CCM ID za kushiriki uchaguzi mpaka mchana hilo limetoa mwanya kwa CUF kuitumia nafasi hio kwa manufaa yao.
6.   Jaji Abdulhakim Ameir Issa kubainika wazi wazi kua na mapenzi na CUF wakati yeye amwekwa katika tume hiyo kiserikali na zaidi katika masuala ya kisheria.
7.   Pemba nusu ya waopiga kura walipigiiwa na watu maalum bila ya sababu ya msingi, na pia kura zilizopigwa hazifanani na majumuisho, na kuna baadhi  ya kura zimetiwa katika mifuko ya karatasi badala ya mifuko ya plastki iliyowekwa na tume ya uchaguzi, Mifuko ya tume iliosaniwa.
Sambamba na hayo ,  tunawaomba  waangalizi wa nje  wasiwe  sehemu ya kutusababishia  mgogoro kwa kushindikiza  mambo ambayo katiba  na sheria zetu  zimeweka bayana.
Kwa upande  wa tamko  la viongozi wa ukawa  lililotolewa jumapili ya tarehe 15 November 2015  la kuishindikiza  tume ya uchaguzi   Zanzibar  kuitaka  imtangaze maalim Seif   halina msingi  na linapingana  na katiba  ya Zanzibar  ibara ya 119 kifungu kidogo cha 12. Hivyo  sisi wanataluma  tunasema  wakae kimya  na wasiipotoshe  jamii  ya  Watanzania.

Kwa kumalizia , tunaisubiri tume   itangaze tarehe nyengine    ya uchaguzi  lakini tunatoa angalizo  , tunaitaka Tume ya Uchaguzi  Zanzibar  isimamie   katiba na sheria  za nchi na kufuata  maadili,  na endapo itaendelea kushirikiana  na chama cha CUF  tunasema sisi wasomi  hatutokubali na tume itabeba jukumu  kubwa kwa hali yoyote   itakayotokezea.

Vile vile, Tunawaomba wasomi wenzetu  pamoja na wanachama wa  CCM  tuwe watulivu lakini tujiandae  kujitokeza kwa   wingi  mara  baada ya kutangazwa  kwa tarehe ya  uchaguzi  kama  walivijitokeza  kwa wingi katika uchaguzi wa Oktoba 25 , 2015  lakini pia wanachama   wetu wajiandae  kusherehekea ushindi kwani  katiba ya CCM  ibara ya 5  (i) inasema ‘’ Ushindi ni Lazima ‘’
Tunatoa wito kwa wanachama wa CCM na wazanzibar kwa ujumla kua makini na chama cha upinzani kwani imeonekana dhahiri kua viongozi wake hawana nia njema kwani kitendo cha mgombea wao kujitangazia mshindi kwa nini kisherekewe nchini Maskati na London?
Pia, tunalaani kitendo cha wabunge  kutoka kambi ya ukawa kwa kitendo cha utomvu wa nidhamu ndani ya chombo kitakatifu na mbele ya viongozi wetu wa taifa letu, kwani wamejidhihirisha wazi wazi kua wao ni watovu wa nidhamu na hawafai kuongoza hata kikundi cha watu wachache.
Mwisho ,  tunaomba  wanasheria wetu  kupitia Afisi  kuu ya CCM waendelee kuelimisha  jamii ili  kuepusha   upotoshaji unaofanywa na  wapinzani.

Vile vile, tunawapongeza wanachama wa Chama cha Mapinduzi kwa uvumilivu wao na kutovunja sheria kwani licha ya kua hadi  matokeo ya majimbo 31 ya Unguja  yanatoka yalikua yanaonesha kua Chama cha Mapinduzi kilikua kinaoongoza lakini mwisho uchaguzi ulifutwa.
Kitendo cha Mgombea wa urais kupitia CUF  Maalim Seif  Sharif Hamad kujitangaza mshindi kiliingiza nchi  yetu katika majaribio ya uvunjifu wa Amani lakini tunavipongeza sana  sana sana vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuweza kusimamia Amani na utulivu wa nchi kabla na baada ya uchaguzi kwani kuna mifano ya nchi kadhaa haziko salama hadi sasa.
Hata hivyo ,  shirikisho  la  vyuo vya elimu ya juu  CCM – Zanzibar   linachukua fursa hii kumpongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Dk Joh’n  Pombe Joseph Magufuli na Makamu wake Samia Suluhu Hassan  kwa kuchaguliwa  na wananchi  wa  Tanzania  lakini pia  tunaridhishwa na namna  alivyoanza kazi kwa kutoa houtuba mwanana iliyolenga kuwasaidia wananchi wa hali ya chini katika kipindi chake cha awamu ya tano cha serikali ya Jamuhuri ya mungano wa Tanzania kwani, ile kauli mbiyu yake ya ‘’Hapa  Kazi  tuu ‘’  inajidhihirisha wazi wazi.
Mwisho kabisa, tunachukua fursa kumpongeza Mhe. Kassim Majaaliwa kwa kuteuliwa kuwa waziri Mkuu na  sambamba na kupitishwa na bunge kwa zaidi ya  73%  ya wabunge wote waliopiga kura.
Ahsanteni  kwa kunisikiliza.


‘’ Mungu   ibariki  Zanzibar’’
‘’Mungu ibariki Tanzania ‘’
‘’Mungu ibariki Afrika”

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI






Imetiwa Saini na Katibu,


………………………………………..

KNY: Shirikisho la Vyuo Vya Elimu Ya Juu CCM- Zanzibar.
21/11/2015.

No comments:

Post a Comment