tangazo

tangazo

Monday, June 30, 2014

VIJANA WAHIMIZWA KUHIFADH QUR-AN


KUWALEA VIJANA KATIKA MAADILI MEMA YA KIISLAM NDIO NJIA PEKEE YA KUULINDA UISLAM KWA KUWAHIFADHISHA VIJANA HAO QUR-AN.

 

HAYO YAMESEMWA NA SAMAHATU SHEKHE PROFESA HAMED RASHID HAMED HIKMAN ALIPOKUWA AKITOA NASAHA FUPI KWA WANAFUNZI NA WAZEE WALIOHUDHURIA KATIKA MASHINDANO YA HIFDHI YA QUR-AN KWA WANAFUNZI WA JUZUU THELATHINI AMBAO NDIO KWANZA MARA YA KWANZA KUSHIRIKI MASHINDANO HAYO HUKO CHWAKA WILAYA YA KATI UNGUJA.

 

VILE VILE AMEWAASA WAISLAM KUIKAMATA QUR-AN KWA KUISOMA ALAU KURASA MOJA KWA SIKU ILI IWE MUONGOZO WA MAISHA YAO.

 

SAMBAMBA NA HAYO AMEWAOMBA WAZEE WA CHWAKA KUIPA NGUVU JUMUIYA YA KUHIFADHISHA QUR-AN KWA HALI NA MALI KATIKA KUFANIKISHA UJENZI WA MAR-KAZI YA KUHIFADHI QUR-AN ITAKAYO JENGWA KIJIJINI KWAO AMBAYO ITASAIDIA KUFANYA TAFITI MBALI MBALI ZA UTAMBUZI WA QUR-AN.

 

AKIMKARIBISHA MGENI RASMI AMIRI MKUU WA JUMUIYA HIYO FADHILAT SHEKHE SULEIMAN OMAR AHMAD AMESEMA,NI WAJIBU WA WAZAZI NA WALEZI KUHAKIKISHA WANAFUNZI WALIOHIFADHI JUZUU THELATHINI KUWATUNZA ILI WALICHOKIHIFADHI KISIPOTEE.

 

HATA HIVYO AMEWAOMBA WAZAZI KUONDOA MIGONGANO BAINA YAO NA WALIMU WA MADRASA ZA QUR-AN ILI KUPELEKA DINI YA KIISLAM MBELE.

 

SAMBAMBA NA HAYO AMESEMA MALENGO YA JUMUIYA HIYO NI KUWAHIFADHISHA VIJANA WOTE WA ZANZIBAR QUR-AN TUKUFU ILI KUPATA LADHA YA UISLAM.

 

MASHINDANO HAYO YA UFUNGUZI YALIYOANDALIWA NA JUMUIYA YA KUHIFADHI QUR-AN ZANZIBAR YALIWASHIRIKISHA WANAFUNZI KUMI NA SITA WA JUZUU THELATHINI AMBAPO MWANAFUNZI SULEIMAN MUHAMMAD JUMA MWENYE UMRI WA MIAKA KUMI NA TATU ALITOKEA WA KWANZA KWA KUPATA ALAMA 98 NA AMEZAWADIWA FEDHA TASLIM LAKI TANO,SAA,TAULA NA SHAHADA YA YA KUMALIZA JUZUU THELETHINI MASHINDANO HAYO YANAENDELEA LEO MASJID TAQWA MELINNE KWA WANAUME NA HAILESALASI KWA WANAWAKE KUANZIA SAA TATU KAMILI ASUBUUHI.

MAALIM SEIF ALAANI HUJUMA ZIDI YA WAGENI ZANZIBAR


MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR MHE. MAALIM SEIF SHARIF HAMAD AMEONYA KUWA VITENDO VYA HUJUMA DHIDI YA RAIA NA WAGENI, VINAWEZA KUATHIRI KWA KIASI KIKUBWA UCHUMI WA ZANZIBAR.

 

AMESEMA ZANZIBAR AMBAYO IMEKUWA IKITEGEMEA ZAIDI SEKTA YA UTALII KUENDELEZA UCHUMI WAKE NA KUKUZA PATO LA TAIFA, IMEKUWA IKIGUSWA NA MATUKIO HAYO YA HUJUMA, NA KWAMBA YANAATHIRI UCHUMI, USTAWI WA JAMII NA SIFA YA UKARIMU KWA ZANZIBAR.

 

MAALIM SEIF AMETOA KAULI HIYO KATIKA MAHOJIANO MAALUM NA KITUO CHA TELEVISHENI CHA ITV, MIKOCHENI DAR ES SALAAM.

 

AMESEMA KATIKA KUKABILIANA NA VITENDO HIVYO, SERIKALI INAKUSUDIA KUTEKELEZA MPANGO WAKE WA KUWEKA KAMERA ZA CCTV KATIKA MAENEO MUHIMU YA UTALII LIKIWEMO ENEO LA MJI MKONGWE, ILI KUWEZA KUWABAINI KWA URAHISI WAHUSIKA WANAFANYA VITENDO HIVYO.

 

KUHUSU ZAO LA KARAFUU KWA MAENDELEO YA UCHUMI WA ZANZIBAR, MAALIM SEIF AMESEMA SERIKALI IMEFANIKIWA KUDHIBITI MAGENDO YA KARAFUU BAADA YA KUONGEZA BEI YA ZAO HILO NA KUWASHINDA WANUNUZI WENGINE WA AFRIKA MASHARIKI AMBAKO KARAFUU HIZO ZILIKUA ZIKIPELEKWA.

 

AIDHA AMESEMA KATIKA KUHAKIKISHA KUWA UBORA WA KARAFUU ZA ZANZIBAR UNALINDWA NA KUDHIBITI WAUZAJI WENGINE, SERIKALI KUPITIA WIZARA YA BIASHARA, VIWANDA NA MASOKO, ITAWEKA NEMBO MAALUM “BRAND”, KUWEZA KUZITOFAUTISHA KARAFUU ZA ZANZIBAR NA MAENEO MENGINE.

Thursday, June 5, 2014

MATAPELI

HUYO ALOWEKA POST YAKE KWENYE JINA LA JULAIBIN DARUWESHI NI MWIZI SIO JULAIBIN MWENYEWE MM SIHUSIKI NA MIKOPO KABISA

Tuesday, June 3, 2014

MUHIBIRI WA KIISLAM AUWAWA GARISA


nairobi.

Muhadhiri  maarufu wakiislam ameuawa katika mji wa Garissa kaskazini mashariki mwa Kenya.

Duru za khbari zimearifu kuwa Sheikh Abdirashid Mohammad alipigwa risasi na kuuawa na watu wasiojulikana Jumapili usiku mjini Garissa.

Mkuu wa Polisi katika jimbo la Garissa Charles Kinyua amesema kuwa muuhadhiri  huyo alipigwa risasi mara kadhaa kwa karibu mita chache  kutoka Msikiti wa Khalifa karibu na Hospitali Kuu ya Garissa.

muhadhiri  huyo Alikuwa amefika msikitini hapo kuswali swala ya Isha.

Afisa huyo wa polisi amesema kuwa lengo la waliomuua bado halijafahamika

 Aidha amedai kuwa mhubiri huyo alikuwa na wapinzani ambao hawakutaka ahubiri katika baadhi ya misikiti.

Duru za khbari mjini Garissa zimedokeza kuwa Sheikh Abdirashid Mohammad aliwahi kunusurika shambulizi kama hilo wakati alipoviziwa katika hoteli moja mjini humo.

Katika siku za hivi karibuni masheikh kadhaa wameuawa nchini Kenya kwa madai yakujihusisha na kundi la al-shabab madai ambayo hayana msingi.

RAIS SHENI AMPONGEZA RAISI MPYA WA MALAWIPeter Mutharika


zanzibar.

 

Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein amemtumia Salamu za Pongezi Rais Mpya wa Malawi Peter Mutharika kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Malawi kufuatia ushindi wake katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika hivi karibuni.

Katika salamu hizo Dk. Shein ameelezea matumaini ya wananchi wa Zanzibar kuwa chini ya uongozi wa Mutharika, ndugu zao wa Malawi wataendeleza umoja wao na kuimarisha maendeleo ya nchi yao.

dr shein amemtakia Rais Mutharika afya njema, kheri na fanaka katika kuiongoza nchi yake.           

ZANZIBAR KUTAFUTA WAFADHILI KWA AJILI YA KUBUNI NJIA MBADALA YA UMEME


ZANZIBAR.

NAIBU WAZIRI WA ARDHI,MAKAAZI,MAJI NA NISHATI HAJI MWADINI MAKAME AMESEMA KUWA SEREKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMEANZA MAZUNGUMZO NA NCHI WAFADHILI KUHUSU JINSI YAKUFANYA UTAFITI WAKUPATIKANA CHANZO MBADALA CHA UMEME HAPA NCHINI.

AKIJIBU MASWALI YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI KATIKA KIKAO KINACHOENDELEA HUKO BWENI WILAYA YA MAGHARIBI UNGUJA WAZIRI MWADINI AMESEMA KUWA SEREKALI IMEAMUA KUFANYA UTAFITI WA UHAKIKA ILI  KUPATIKANA CHANZO CHA KUDUMU CHA NISHATI YA UMEME.

AKIZUNGUMZIA SUALA LA GHARAMA KUBWA ZA UMEME NCHINI AMESEMA KUWA SUALA HILO LITAPATIWA UFUMBUZI BAADA YAKUPATIKANA KWA CHANZO MBADALA CHA NISHATI HIYO.

ZANZIBAR NDIO CHIMBUKO LA UISLAM AFRIKA YA MASHARIKI


zanzibar.

IMEELEZWA KUWA ZANZIBAR NDIO CHANZO CHA UISLAM KATIKA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI.

 

HAYO YAMEELEZWA NA  AMIRI SEIF L-HAK WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAISLAM HUKO MASJID SAID FUONI MAHARIBIKO.

 

AMEWATAKA WAISLAM KUTUMIA NAFASI YAO WALIYONAYO KATIKA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI KUWAPOKEA NAKUWAKIRIBU WAGENI WATAKAOKUJA NCHINI KUHUDHURIA KATIKA IJITIMAI YAKIMATAIFA INAYOTARAJIWA KUFANYIKA TAREHE 13 HADI 16 MWEZI HUU HUKO FUONI MIGOMBANI WILAYA YA MAGHARIBI UNGUJA.

 

AIDHA ALIM HUYO AMEWASISITIZA WAIsLAM KUJITOLEA KWA HALI NA MALI ILI KUFANIKISHA IJTIMAI HIYO YENYE LENGO LAKUWAKUMBUSHA WAISLAM JUKUMU WALILONALO DUNIANI KATIKA KUMTUMIKIA MOLA WAO.

 

HATA HIVYO AMIRI SEIF AMEWAKUMBUSHA WAISLAM KUYATUMIA VIZURI MAISHA YAO YA DUNIA ILI KUACHA ATHARI NZURI YA TABIA NJEMA MARA BAADA YAKUAGA DUNIA.