nairobi.
Muhadhiri maarufu wakiislam ameuawa katika mji wa
Garissa kaskazini mashariki mwa Kenya.
Duru
za khbari zimearifu kuwa Sheikh Abdirashid Mohammad alipigwa risasi na kuuawa
na watu wasiojulikana Jumapili usiku mjini Garissa.
Mkuu
wa Polisi katika jimbo la Garissa Charles Kinyua amesema kuwa muuhadhiri huyo alipigwa risasi mara kadhaa kwa karibu
mita chache kutoka Msikiti wa Khalifa
karibu na Hospitali Kuu ya Garissa.
muhadhiri huyo Alikuwa amefika msikitini hapo kuswali swala
ya Isha.
Afisa
huyo wa polisi amesema kuwa lengo la waliomuua bado halijafahamika
Aidha amedai kuwa mhubiri huyo alikuwa na
wapinzani ambao hawakutaka ahubiri katika baadhi ya misikiti.
Duru
za khbari mjini Garissa zimedokeza kuwa Sheikh Abdirashid Mohammad aliwahi
kunusurika shambulizi kama hilo wakati alipoviziwa katika hoteli moja mjini
humo.
Katika
siku za hivi karibuni masheikh kadhaa wameuawa nchini Kenya kwa madai
yakujihusisha na kundi la al-shabab madai ambayo hayana msingi.
No comments:
Post a Comment