MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR
MHE. MAALIM SEIF SHARIF HAMAD AMEONYA KUWA VITENDO VYA HUJUMA DHIDI YA RAIA NA
WAGENI, VINAWEZA KUATHIRI KWA KIASI KIKUBWA UCHUMI WA ZANZIBAR.
AMESEMA ZANZIBAR AMBAYO IMEKUWA
IKITEGEMEA ZAIDI SEKTA YA UTALII KUENDELEZA UCHUMI WAKE NA KUKUZA PATO LA
TAIFA, IMEKUWA IKIGUSWA NA MATUKIO HAYO YA HUJUMA, NA KWAMBA YANAATHIRI UCHUMI,
USTAWI WA JAMII NA SIFA YA UKARIMU KWA ZANZIBAR.
MAALIM SEIF AMETOA KAULI HIYO KATIKA
MAHOJIANO MAALUM NA KITUO CHA TELEVISHENI CHA ITV, MIKOCHENI DAR ES SALAAM.
AMESEMA KATIKA KUKABILIANA NA VITENDO
HIVYO, SERIKALI INAKUSUDIA KUTEKELEZA MPANGO WAKE WA KUWEKA KAMERA ZA CCTV
KATIKA MAENEO MUHIMU YA UTALII LIKIWEMO ENEO LA MJI MKONGWE, ILI KUWEZA
KUWABAINI KWA URAHISI WAHUSIKA WANAFANYA VITENDO HIVYO.
KUHUSU ZAO LA KARAFUU KWA MAENDELEO YA
UCHUMI WA ZANZIBAR, MAALIM SEIF AMESEMA SERIKALI IMEFANIKIWA KUDHIBITI MAGENDO
YA KARAFUU BAADA YA KUONGEZA BEI YA ZAO HILO NA KUWASHINDA WANUNUZI WENGINE WA
AFRIKA MASHARIKI AMBAKO KARAFUU HIZO ZILIKUA ZIKIPELEKWA.
AIDHA AMESEMA KATIKA KUHAKIKISHA KUWA
UBORA WA KARAFUU ZA ZANZIBAR UNALINDWA NA KUDHIBITI WAUZAJI WENGINE, SERIKALI
KUPITIA WIZARA YA BIASHARA, VIWANDA NA MASOKO, ITAWEKA NEMBO MAALUM “BRAND”,
KUWEZA KUZITOFAUTISHA KARAFUU ZA ZANZIBAR NA MAENEO MENGINE.
No comments:
Post a Comment