KUWALEA
VIJANA KATIKA MAADILI MEMA YA KIISLAM NDIO NJIA PEKEE YA KUULINDA UISLAM KWA
KUWAHIFADHISHA VIJANA HAO QUR-AN.
HAYO
YAMESEMWA NA SAMAHATU SHEKHE PROFESA HAMED RASHID HAMED HIKMAN ALIPOKUWA AKITOA
NASAHA FUPI KWA WANAFUNZI NA WAZEE WALIOHUDHURIA KATIKA MASHINDANO YA HIFDHI YA
QUR-AN KWA WANAFUNZI WA JUZUU THELATHINI AMBAO NDIO KWANZA MARA YA KWANZA
KUSHIRIKI MASHINDANO HAYO HUKO CHWAKA WILAYA YA KATI UNGUJA.
VILE
VILE AMEWAASA WAISLAM KUIKAMATA QUR-AN KWA KUISOMA ALAU KURASA MOJA KWA SIKU
ILI IWE MUONGOZO WA MAISHA YAO.
SAMBAMBA
NA HAYO AMEWAOMBA WAZEE WA CHWAKA KUIPA NGUVU JUMUIYA YA KUHIFADHISHA QUR-AN
KWA HALI NA MALI KATIKA KUFANIKISHA UJENZI WA MAR-KAZI YA KUHIFADHI QUR-AN
ITAKAYO JENGWA KIJIJINI KWAO AMBAYO ITASAIDIA KUFANYA TAFITI MBALI MBALI ZA
UTAMBUZI WA QUR-AN.
AKIMKARIBISHA
MGENI RASMI AMIRI MKUU WA JUMUIYA HIYO FADHILAT SHEKHE SULEIMAN OMAR AHMAD
AMESEMA,NI WAJIBU WA WAZAZI NA WALEZI KUHAKIKISHA WANAFUNZI WALIOHIFADHI JUZUU
THELATHINI KUWATUNZA ILI WALICHOKIHIFADHI KISIPOTEE.
HATA
HIVYO AMEWAOMBA WAZAZI KUONDOA MIGONGANO BAINA YAO NA WALIMU WA MADRASA ZA
QUR-AN ILI KUPELEKA DINI YA KIISLAM MBELE.
SAMBAMBA
NA HAYO AMESEMA MALENGO YA JUMUIYA HIYO NI KUWAHIFADHISHA VIJANA WOTE WA
ZANZIBAR QUR-AN TUKUFU ILI KUPATA LADHA YA UISLAM.
MASHINDANO
HAYO YA UFUNGUZI YALIYOANDALIWA NA JUMUIYA YA KUHIFADHI QUR-AN ZANZIBAR
YALIWASHIRIKISHA WANAFUNZI KUMI NA SITA WA JUZUU THELATHINI AMBAPO MWANAFUNZI
SULEIMAN MUHAMMAD JUMA MWENYE UMRI WA MIAKA KUMI NA TATU ALITOKEA WA KWANZA KWA
KUPATA ALAMA 98 NA AMEZAWADIWA FEDHA TASLIM LAKI TANO,SAA,TAULA NA SHAHADA YA
YA KUMALIZA JUZUU THELETHINI MASHINDANO HAYO YANAENDELEA LEO MASJID TAQWA
MELINNE KWA WANAUME NA HAILESALASI KWA WANAWAKE KUANZIA SAA TATU KAMILI
ASUBUUHI.
No comments:
Post a Comment