zanzibar.
Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein
amemtumia Salamu za Pongezi Rais Mpya wa Malawi Peter Mutharika kwa kuchaguliwa
kuwa Rais wa Malawi kufuatia ushindi wake katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo
uliofanyika hivi karibuni.
Katika salamu hizo Dk. Shein ameelezea
matumaini ya wananchi wa Zanzibar kuwa chini ya uongozi wa Mutharika, ndugu zao
wa Malawi wataendeleza umoja wao na kuimarisha maendeleo ya nchi yao.
dr shein amemtakia Rais Mutharika afya njema, kheri
na fanaka katika kuiongoza nchi yake.
No comments:
Post a Comment