zanzibar.
IMEELEZWA KUWA ZANZIBAR NDIO CHANZO CHA UISLAM KATIKA UKANDA
WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI.
HAYO YAMEELEZWA NA
AMIRI SEIF L-HAK WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAISLAM HUKO MASJID SAID FUONI
MAHARIBIKO.
AMEWATAKA WAISLAM KUTUMIA NAFASI YAO WALIYONAYO KATIKA
UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI KUWAPOKEA NAKUWAKIRIBU WAGENI WATAKAOKUJA NCHINI
KUHUDHURIA KATIKA IJITIMAI YAKIMATAIFA INAYOTARAJIWA KUFANYIKA TAREHE 13 HADI
16 MWEZI HUU HUKO FUONI MIGOMBANI WILAYA YA MAGHARIBI UNGUJA.
AIDHA ALIM HUYO AMEWASISITIZA WAIsLAM KUJITOLEA KWA HALI
NA MALI ILI KUFANIKISHA IJTIMAI HIYO YENYE LENGO LAKUWAKUMBUSHA WAISLAM JUKUMU
WALILONALO DUNIANI KATIKA KUMTUMIKIA MOLA WAO.
HATA HIVYO AMIRI SEIF AMEWAKUMBUSHA WAISLAM KUYATUMIA
VIZURI MAISHA YAO YA DUNIA ILI KUACHA ATHARI NZURI YA TABIA NJEMA MARA BAADA
YAKUAGA DUNIA.
No comments:
Post a Comment