ZANZIBAR.
NAIBU WAZIRI WA ARDHI,MAKAAZI,MAJI NA NISHATI HAJI
MWADINI MAKAME AMESEMA KUWA SEREKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMEANZA
MAZUNGUMZO NA NCHI WAFADHILI KUHUSU JINSI YAKUFANYA UTAFITI WAKUPATIKANA CHANZO
MBADALA CHA UMEME HAPA NCHINI.
AKIJIBU MASWALI YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI
KATIKA KIKAO KINACHOENDELEA HUKO BWENI WILAYA YA MAGHARIBI UNGUJA WAZIRI
MWADINI AMESEMA KUWA SEREKALI IMEAMUA KUFANYA UTAFITI WA UHAKIKA ILI KUPATIKANA CHANZO CHA KUDUMU CHA NISHATI YA
UMEME.
AKIZUNGUMZIA SUALA LA GHARAMA KUBWA ZA UMEME NCHINI
AMESEMA KUWA SUALA HILO LITAPATIWA UFUMBUZI BAADA YAKUPATIKANA KWA CHANZO
MBADALA CHA NISHATI HIYO.
No comments:
Post a Comment