ZANZIBAR.
Jeshi la Polisi Zanzibar limemuachia kwa dhamana mpiga picha maarufu katika
mihadhara yakiislam na harakati zakisiasa al-ustadh Salim Khatib Kombo mwenye
umri wa miaka 38 mkaazi wa makondeko Milaya ya Magharibi Unguja baada yakuwekwa
kizuizini kwa Takriban siku 39 bila yakufikishwa Mahakamani.
Akizungumza na Redio Adhan Fm amesema kuwa alikamatwa na Jeshi la Polisi Jumamosi
Jioni ya tarehe 9/8/2014 wakati akichukuwa picha ya video ya mkutano wa chama
cha National Reconstraction Allience uliofanyika katika viwanja vya Kombawapya Mjini
zanzibar na baadaye kupelekwa katika kituo cha Polisi mwembemadema mjini Zanzibar.
Akiwa katika kituo hicho salim amesema kuwa alipewa tuhuma zakuhusika na
tukio la mripuko wa bomu uliotokea katika msikiti wa darajani mjini zanzibar
tarehe 13 June 2014 baada ya utekelezaji wa swala ya isha nakupelekea kifo cha
muhadhiri mmoja wakiislam ambapo alilazwa siku moja na siku ya pili
akasafirishwa nakupelekwa katika kituo cha salenda brige Polisi Kinondoni Mjini
Dar-es-salaa hadi siku ya Jumatatu nakupelekwa katika chumba maalum kwa ajili
ya mahojiano na maafisa wa usalama wa Taifa.
Aidha ustadh salim amesema awali alihojiwa kuhusu mripuko wa bomu uliotokea
Darajani Mjini Zanzibar nakuhusishwa kuhusika nao na baadaye jioni ya Jumatatu
tarehe 11 alipelekwa katika kituo cha Polisi Mabatini Wilaya ya Kinondoni na
aliwekwa katika kituo hicho kwa muda wa siku 14 bila yakufanyiwa mateso yoyote
isipokuwa kunyolewa ndevu.
Hata hivyo Mtuhumiwa huyo amesema kila siku alikuwa akipelekwa katika
chumba maalum cha mahojiano ambapo baadaye mambo yalibadilika na Polisi
kuchunguza simu yake nakungundua kuwa alikuwa akituma ujumbe mfupi wa maandishi
kwa watu wengi kuwajuilisha waislam taarifa kuhusu kukamatwa masheikh kila
zinapotokea na ndipo alipobadilishiwa tuhuma na nakuwa zauchochezi.
Ustadh salim amesema baada ya wiki mbili kupita alirejeshwa zanzibar
nakuzuiliwa tena katika kituo cha Polisi Madema kuanzia tarehe 23/08/2014 hadi 17/9/2014 nakuhojiwa kuhusu suala la
ujumbe mfupi wa maandishi aliokuwa akiituma kwa waislam kuhusu harakati za Kiislam
na kukamatwa kwa masheikh Zanzibar na Tanzania bara ambao aliupa jina sufa
islamic na bustani ya khabari nakutoa ufafanuzi kuhusu suala hilo.
Akizungumzia tuhuma mpya alizopewa amesema aliambiwa kuwa anahusika na
vitendo vya uchochezi kutokana na ujumbe mfupi wa maandishi aliokuwa akiwatumia
Waislam na akakubali tuhuma hizo akitegemea kuwa atapelekwa mahakamani na
ilipofika tarehe 17 /09/2014 alikwenda mdogo wake kumchukulia dhamana katika
kituo cha Polisi Madema na hatimaye kuachiliwa huru bila yakufikishwa Mahakamani
nakutakiwa kuripoti kila wiki katika kituo hicho.