tangazo

tangazo

Tuesday, September 30, 2014

MPIGA PICHA LIYEKAMATWA ZANZIBAR BILA YA KUPANDISHWA KIZIMBANI AACHIWA KWA DHAMANA ZANZIBAR


 ZANZIBAR.

 

Jeshi la Polisi Zanzibar limemuachia kwa dhamana mpiga picha maarufu katika mihadhara yakiislam na harakati zakisiasa al-ustadh Salim Khatib Kombo mwenye umri wa miaka 38 mkaazi wa makondeko Milaya ya Magharibi Unguja baada yakuwekwa kizuizini kwa Takriban siku 39 bila yakufikishwa Mahakamani.

 

Akizungumza na Redio Adhan Fm amesema kuwa alikamatwa na Jeshi la Polisi Jumamosi Jioni ya tarehe 9/8/2014 wakati akichukuwa picha ya video ya mkutano wa chama cha National Reconstraction Allience uliofanyika katika viwanja vya Kombawapya Mjini zanzibar na baadaye kupelekwa katika kituo cha Polisi mwembemadema mjini Zanzibar.

 

Akiwa katika kituo hicho salim amesema kuwa alipewa tuhuma zakuhusika na tukio la mripuko wa bomu uliotokea katika msikiti wa darajani mjini zanzibar tarehe 13 June 2014 baada ya utekelezaji wa swala ya isha nakupelekea kifo cha muhadhiri mmoja wakiislam ambapo alilazwa siku moja na siku ya pili akasafirishwa nakupelekwa katika kituo cha salenda brige Polisi Kinondoni Mjini Dar-es-salaa hadi siku ya Jumatatu nakupelekwa katika chumba maalum kwa ajili ya mahojiano na maafisa wa usalama wa Taifa.

 

Aidha ustadh salim amesema awali alihojiwa kuhusu mripuko wa bomu uliotokea Darajani Mjini Zanzibar nakuhusishwa kuhusika nao na baadaye jioni ya Jumatatu tarehe 11 alipelekwa katika kituo cha Polisi Mabatini Wilaya ya Kinondoni na aliwekwa katika kituo hicho kwa muda wa siku 14 bila yakufanyiwa mateso yoyote isipokuwa kunyolewa ndevu.

 

Hata hivyo Mtuhumiwa huyo amesema kila siku alikuwa akipelekwa katika chumba maalum cha mahojiano ambapo baadaye mambo yalibadilika na Polisi kuchunguza simu yake nakungundua kuwa alikuwa akituma ujumbe mfupi wa maandishi kwa watu wengi kuwajuilisha waislam taarifa kuhusu kukamatwa masheikh kila zinapotokea na ndipo alipobadilishiwa tuhuma na nakuwa zauchochezi.

 

Ustadh salim amesema baada ya wiki mbili kupita alirejeshwa zanzibar nakuzuiliwa tena katika kituo cha Polisi Madema kuanzia tarehe 23/08/2014  hadi 17/9/2014 nakuhojiwa kuhusu suala la ujumbe mfupi wa maandishi aliokuwa akiituma kwa waislam kuhusu harakati za Kiislam na kukamatwa kwa masheikh Zanzibar na Tanzania bara ambao aliupa jina sufa islamic na bustani ya khabari nakutoa ufafanuzi kuhusu suala hilo.

 

Akizungumzia tuhuma mpya alizopewa amesema aliambiwa kuwa anahusika na vitendo vya uchochezi kutokana na ujumbe mfupi wa maandishi aliokuwa akiwatumia Waislam na akakubali tuhuma hizo akitegemea kuwa atapelekwa mahakamani na ilipofika tarehe 17 /09/2014 alikwenda mdogo wake kumchukulia dhamana katika kituo cha Polisi Madema na hatimaye kuachiliwa huru bila yakufikishwa Mahakamani nakutakiwa kuripoti kila wiki katika kituo hicho.

No comments:

Post a Comment