SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMESEMA ITAENDELEA NA ZOEZI LA USAJILI WA ARHI KWA MAENEO MBALIMBAALI YA MIJINI NA VIJIJINI KWA LENGO LA KUPUNGUZA MIGOGORO YA ARDHI INAYOJITOKEZA KATIKA JAMII.
AKIZUNGUMZA KATIKA SHEREHE ZA UTOWAJI WA KADI ZA USAJILI WA ARDHI KWA WANANCHI, WAZIRI WA ARDHI,MAKAAZI,MAJI NA NISHATI MH: RAMADHAN ABDALLAH SHAABAN AMESEMA HALI HIYO YA KUSAJILI KWA KUTUMIA NJIA TEKNOLOJIA ITAPELEKEA WANANCHI KUONDOKANA NA USUMBUFU WA KUMILIKI MAENEO YAO.
AMEFAHAMISHA KUWA ZOEZI LA USAJILI WA ARDHI NI HATUWA MOJA WAPO YA MATUNDA YA SERIKALI YA MAPINDUZI YA 1964 KATIKA KUENDELEZA HAKI KWA WANANCHI WAKE ILI WAPATE UMILIKI HALALI WA ARDHI YAO.
KWA UPANDE WAKE MRAJISI WA ARHI ZANZIBAR BI MWANAMKAA ABDUL-RAHMAN AMESEMA LENGO LA ZOEZI HILO NI KUPUNGUZA ENGEZEKO LSA KESI ZA MIGOGORO YA ARDHI NA KUONDOA TATIZO LA WIZI WA UTUMIAJI WA NYARAKA ZA BANDIA KWA WAMILIKI WA NYUMBA HIZO.
AIDHA AMEFAFANUA KUWA MATUMIZI YA KADI ZA UMILIKI WA ARDHI YATAWASAIDIA WANAFAMILIA KUONDOKANA NA TATIZO LA UDANGANYIFU WA MAENEO HAYO.
JUMLA YA WANANCHI KUTOKA SHEHIA KUMI NA NANE (18) ZA WA MKOWA WA MJINI MAGHARIBI WAMEKABIZIWA KADI HIZO ZA UMILIKI WA ARDHI AMBAPO ZOEZI LA USAJILI WA ARDHI LILIZINDULIWA MNAMO TAREHE 23 MACHI 2013 NA RAISI ZANZIBAR AMBAE PIA NI MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK: ALI MOH”D SHEIN.
No comments:
Post a Comment