WILAYA YA MJINI
JAMII NCHINI
IMETAKIWA KUONDOSHA MUHALI
ILI KUTOKOMEZA VITENDO VYA
UDHALILISHAJI KATIKA JAMII.
HAYO YAMESEMWA NA
MRATIBU WA MRADI WA KUIMARISHA FAMILIA NDUGU MAKAME MTWANA HAJI KATIKA
KONGAMANO MAALUM LILILOANDALIWA NA KIJIJI CHA SOS KUHUSIANA NA HIFADHI YA MTOTO
NA MAPAMBANO JUU YA UDHALILISHAJI KATIKA UKUMBI WA MAZSONS HOTELI.
HATA HIVYO
AMEIASA JAMII KUTOKUTENGENEZA MAZINGIRA
YATAYOSABABISHA KUBAKWA KAMA
VILE UVAAJI WA
NGUO ZA KUBANA
NA MAPAMBO.
SAMBAMBA NA HAYO AMEIOMBA POLISI
JAMII KATIKA SHEHIA
MBALIMBALI KUWASAIDIA KUWALINDA
WATOTO KUTOKANA NA
VITENDO VYA UDHALILISHAJI, NA WAO
KUWA MSTARI WA
MBELE KATIKA KUTUNZA
MAADILI.
AKITOA MADA KATIKA
KONGAMANO HILO AFISA WA WATOTO NCHINI NGUGU MUHAMMED JABIR
MAKAME AMEIASWA JAMII
KUTOKUWAFANYIA WATOTO VITENDO
AMBAVYO VITAWAATHIRI KIAKILI, KIMWILI NA KISAIKOLOJIA.
AMESEMA UTAFITI ULIOFANYIKA
MWAKA 2009 UNAONYESHA
KUWA WAFANYAJI WA
VITENDO VYA UDHALILISHAJI WA
WATOTO KIJINSIA NI WATU
WA KARIBU NA
FAMILIA.
HATA HIVYO AMESEMA LICHA
YA MATENDO YA
UDHALILISHAJI KUFANYWA NA WATU
WAZIMA LAKINI PIA NA
WATOTO WENYEWE HUDHALILISHANA KIJINSIA.
VILE VILE AMESEMA KUMEKUWA NA
TABIA YA BAADHI
YA WALEZI NA
VIONGOZI WA TAASISI
MBALIMBALI KUPITIA MAMLAKA
WALIYO NAYO KUSULUHISHA KESI
ZA UDHALILISHAJI KIJINSIA
KIENYEJI.
KWA UPANDE WA
MJUMBE KUTOKA TAMWA BI SHARIFA MAULIDI AKIZUNGUMZIA UTATUZI
WA MIGOGORO AMESEMA
NI LAZIMA KUREJESHA MALEZI
YA PAMOJA KATIKA
JAMII NA KUIMARISHA
NDOA ILI KUILEA
JAMII KATIKA MAADILI.
No comments:
Post a Comment