ZANZIBAR
MKURUGENZI WA IDARA YA MIPANGO , SERA NA UTAFITI WA WIZARA YA UWEZESHAJI ,USTAWI WA JAMII, VIJANA ,WANAWAKE NA WATOTO BIBI MHAZA GHARIB JUMA AMESEMA WIZARA YAKE IMEANZA KUTEKELEZA HATUA YA PILI YA UANZISHWAJI WA BARAZA LA VIJANA LA ZANZIBAR BAADA YA KUMALIZIKA HATUA YA KUTIWA SAINI SHARIA HIYO NA RAIS WA ZANZIBAR NA MWEYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI MHE. DKT ALI MOHAMMED SHEIN BAADA YA KUPITISHWA NA BARAZA LA WAWAKILISHI.
MKURUGENZI HUYO AMEYASEMA HAYO HUKO KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA WIZARA HIYO, MWANAKWEREKWE WAKATI WA KIKAO MAALUMU CHA KIKAZI CHA KUZIPITIA KANUNI ZITAKAZOONGOZA BARAZA LA VIJANA LA ZANZBAR, KIKAO KILICHOSHIRIKISHA MAAFISA KUTOKA IDARA TAFAUTI ZA WIZARA HIYO NA WADAU KUTOKA TAASISI MBALI MBALI ZINAZOSHUGHULIKIA MAENDELEO YA VIJANA NCHINI.
MKURUGENZI HUYO AMESEMA TOKEA MWAKA 2000 WIZARA ILIKUWA KATIKA MCHAKATO WA KUANZISHWA BARAZA LA VIJANA LA ZANZIBAR AMBALO SASA LIMEFIKIA HATUA NZURI YA KUZIPITIA KANUNI ZILIZOANDALIWA AMBAZO ZITAWALETEA VIJANA WOTE NCHINI MAENDELEO KATIKA NYANJA ZOTE.
AMESEMA BAADA YA KANUNI HIZI KUPITIWA NA KUWEKWA VIZURI ZAIDI BARAZA HILO LITAANZA KAZI RASMI PAMOJA NA VIJANA NA WANANCHI KUPEWA ELIMU INAYOHITAJIKA KUHUSIANA NA BARAZA HILO.
MAPEMA AKIWASILISHA KANUNI HIZO KWA WADAU WASHIRIKI, MTAALAMU MUELEKEZI KATIKA KUANDAA KANUNI HIZO ND. OMAR SURURU KHALFAN AMESEMA KANUNI HIYO INA VIFUNGU VINANE (8) YENYE JUMLA YA SEHEMU THALATHINI NA TISA (39) AMBZO KUWEPO KWAKE KUTAONGOZA KUWALETEA VIJANA MAENDELEO PAMOJA NA MUSTAKABALI WAO.
AMESEMA BARAZA LA TAIFA LA VIJANA LITAFANYA KAZI KWA UKARIBU ZAIDI NA BARAZA LA VIJANA LA WILAYA PAMOJA NA BARAZA LA VIJANA LA SHEHIA KATIKA KUYATAFUTIA UFUMBUZI WA KUFAA MATATIZO YANAYOWAKABILI VIJANA KATIKA MAENEO WANAYOISHI.
WAKICHANGIA WAKATI WA KUZIPITIA KANUNI HIZO MAAFISA NA WADAU HAO WAMESEMA KANUNI HIZO NI NZURI LAKINI UTEKELZAJI WAKE ZAIDI YAANGALIWE MAZINGIRA YA SHERIA HUSIKA INAYOSIMAMIWA NA KANUNI HIYO ILI KUONDOA MGONGANO NA KULETA UFANISI.
No comments:
Post a Comment