DHAKA
WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA WA
BANGLADESH ABDUL LATIF SIDDIQUE AMEVUNJIA HESHIMA MATUKUFU YA KIISLAMU KWA
KUTOA KAULI YA KEJELI JUU YA IBADA YA HIJJA AMBAYO YAMEWAKASIRISHA WANANCHI WA
TAIFA HILO.
KATIKA KEJELI YAKE HIYO DHIDI YA
UISLAM AMBAPO AMEWAAMBIA WABANGALI WANAOISHI MAREKANI KWAMBA WAISLAMU
WANAOKWENDA KUHIJI KATIKA NYUMBA YA MWENYEZI MUNGU HUKO MAKKA WANAFUJA NA
KUHARIBU PESA BURE.
WAZIRI HUYO AMEWATAKA MAELFU YA
WABANGALI WALIOKO MAKKA KWA AJILI YA IBADA YA HIJA WAWEKEZE FEDHA ZAO KATIKA
MASUALA YA KIUCHUMI BADALA YA SAFARI YA HIJA.
WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA WA
BANGLADESH AMEDAI KUWA SAFARI HIYO YA HIJA INAYOFANYWA KILA MWAKA NA WAISLAMU
NI UTAMADUNI USIO SAHIHI.
DHARAU NA MATUSI HAYO YA WAZIRI WA
SERIKALI YA BANGLADESH YAMEWAKASIRI SANA WANANCHI, VIONGOZI NA WAFUASI WA VYAMA
MBALIMBALI NCHINI HUMO.
VIONGOZI WA VYAMA HIVYO UKIWEMO
MUUNGANO WA KIISLAMU WAMETANGAZA KUWA WAZIRI HUYO WA MAWASILIANO AMERITADI NA
KWAMBA ANAPASWA KUCHUKULIWA HATUA KALI ZA KISHERIA.
VILEVILE WAMETOA WITO KWA WAZIRI HUYO AFUKUZWE KATIKA BARAZA LA
MAWAZIRI LA BANGLADESH.
No comments:
Post a Comment