tangazo

tangazo

Sunday, November 30, 2014

AFYA YA RAIS KIKWETE YAIMARIKA


RAIS WA JAMUHURI WA MUUNGANO WA TANZANIA JAKAYA MRISHO KIKWETE AMESEMA AMEPONA SARATANI BAADA YA KUFANYIWA UPASUAJI MAPEMA MWEZI HUU NCHINI MAREKANI.

KIONGOZI HUYO WA TAIFA MWENYE UMRI WA MIAKA 64 AMETOA HOTUBA KWA TAIFA KUELEZEA AFYA YAKE.

HATA HIVYO AMESEMA ALIGUNDULIKA KUWA NA HATUA YA PILI YA SARATANI YA KIBOFU, AMBAYO BAADAYE IKAONEKANA KUWA NI HATUA YA KWANZA.

VILE VILE AMEONGEZA KUWA SASA HALI YAKE IKO VIZURI NA MADAKTARI WALISEMA SARATANI HAIKUENEA KATIKA SEHEMU NYINGINE ZA MWILI NA BAADA YA UPASUAJI SASA WAMESEMA AMEPONA SARATANI.

RAISI KIKWETE ALIGUNDULIKA KUWA NA SARATANI YA KIBOFU ZAID YA MWAKA MMOJA ULIOPITA NA ALIFANYIWA UPASUAJI KATIKA HOSPITALI MOJA NCHINI MAREKANI MWEZI NOVEMBA.

KIKWETE AMBAYE ANAMALIZA MUHULA WAKE WA PILI MWAKANI AMESEMA WANANCHI WAJENGE TABIA YA KUPIMA AFYA ZAO ILI WAGUNDUE MARADHI MAPEMA.

SERIKALI YA ZANZIBAR KUAGIZA VIFAA VIPYA KWA UJENZI WA BARABARA


RAIS WA ZANZIBAR AMBAYE PIA NI MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN AMESEMA SERIKALI IMEAMUA KUAGIZA VIFAA VIPYA VYA UJENZI WA BARABARA ILI KUHAKIKISHA KUWA MIRADI YOTE YA BARABARA ILIYOPANGWA IWEZE KUTEKELEZWA NA KUKAMILIKA IFIKAPO MWEZI AGOSTI MWAKA UJAO.

 

AKIZUNGUMZA NA VIONGOZI WA MASHINA NA WENYEVITI WA MASKANI ZA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA KASKAZINI ‘B’, DK. SHEIN AMESEMA SERIKALI INAFANYA HIVYO ILI KUONGEZA KASI YA UJENZI WA BARABARA KWA KUWA HIVI SASA VIFAA VILIVYOPO HAVIWEZI KUTEKELEZA MRADI ZAIDI YA MMOJA KWA WAKATI MMOJA.

 

HATA HIVYO AMESEMA KUWA SERIKALI INATAZWA NA MAMBO MADOGO MADOGO LAKINI FEDHA ZA KUTOSHA ZIPO KUFANYA KAZI HIYO HIVYO WAMEAMUA KUAGIZA VIFAA ZAIDI ILI KUONGEZA KASI KWA KUTEKELEZA MIRADI ZAIDI YA MOJA KWA WAKATI MMOJA HIVYO MATARAJIO NI KUKAMILISHA MIRADI HIYO KWENYE MWEZI AGOSTI 2015.

 

SAMBAMBA NA HAYO AMEWAHAKIKISHIA WANANCHI WA WILAYA HIYO KUWA BARABARA ZA WILAYA HIYO ZILIZOMO KATIKA MPANGO WA SERIKALI ZITAJENGWA KATIKA KIPINDI HICHO HIVYO WANACHOTAKIWA KWAO NI KUWA SUBIRA.

WANANCHI WATAENDELEA KUPATA TAKWIMU SAHIHI


SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu imesema kuwa itaendelea kuwapatia wananchi takwimu sahihi zinazohusu sekta mbalimbali ili kuwajengea uwezo wa kushiriki katika ngazi za maamuzi na masuala mbalimbali nchini. 

 

Kauli hiyo imetolewa NA Waziri wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  Omar Yussuf  Mzee wakati akifungua rasmi maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika jijini Dar es salaam yanaoongozwa na kauli mbiu Takwimu Huria kwa uwajibikaji na ushirikishwaji wa wadau wote.

 

Amesema KUWA upatikanaji wa taarifa na  takwimu sahihi kwa wananchi unaongeza ushiriki wao katika maamuzi na kuwajengea uwezo wa kutathmini utendaji wa Serikali katika masuala mbalimbali yakiwemo mapato na matumizi.

 

Amesema KUWA Ofisi ya Taifa ya Takwimu itaendelea kuhakikisha kuwa takwimu mbalimbali zinapatikana kwa urahisi kupitia mtandao, machapisho na mifumo rahisi ili kuwawezesha wananchi na wadau mbalimbali kuzipata WATAKApozihitaji.

 

Amefafanua  kuwa upatikanaji wa takwimu huria unawawezesha wananchi kujua sababu zinazoifanya serikali kutekeleza maamuzi mbalimbali, kuongeza uwajibikaji na kuwawezesha kupima matokeo ya sera za Serikali, kutathimini matumizi ya Serikali na kushiriki katika midahalo mbalimbali ya kitaifa. 

 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Aldegunda Kombo akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi hiyo amesema kuwa maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika mwaka huu yameweka msisitizo katika kuweka miundombinu ya kuwarahisishia wadau kupata takwimu sahihi kwa wakati.

 

Amesema KUWA maadhimisho hayo licha ya kujadili masuala mbalimbali yanajikita katika kuweka msukumo wa kuhakikisha kuwa takwimu sahihi zinawafikia wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo bila vikwazo vyovyote ili kuongeza uwazi wa utendaji wa shughuli za serikali serikali.

 

Naye mwakilishi kutoka nchi washirika wa maendeleo Bw.Jacques Morisset akizungumza wakati wa maadhimisho hayo ameeleza kuwa takwimu sahihi ni ufunguo wa maendeleo kwa nchi yoyote duniani.

BILIONI 306 BADO NI MALI YA UMMA


Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imesisitiza kuwa ShILINGI  bilioni 306 zilizochukuliwa kATIKA Akaunti ya Tegeta Escrow ni za umma na waliohusika katika sakata hilo wachukuliwe hatua kali na za kinidhamu.

Akihitimisha mjadala huo uliochangiwa na wabunge 35 na wawili kwa njia ya maandishi, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Zitto Kabwe alisema fedha hizo ni mali ya umma na hilo limethibitishwa na ofisi nyeti za Serikali.

Zitto alizitaja ofisi hizo kuwa ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ,Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Alisema kwa miaka 11 Tanesco walikuwa wakisema fedha ni za kwao, lakini mwaka wa 12 kikao KATIKA kimoja pekee waLIsema fedha siyo za kwao, hapo hakuna ukweli wowote.

KWA UPANDE WAKE Mbunge wa Nzega (CCM), Dk KHamisi Kigwangalla aMEsema KUWA ukubwa wa Bunge katika Bunge hilo wakati tunafanya uamuzi, CCM watatawala na kila kitu kutokana na wingi lakini hilo WATalifikia IWAPO WAtaweka mbele na kuthamini ukubwa wa Bunge i.

Thursday, November 27, 2014

SMZ NA MPANGO WA KUKUZA UCHUMI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa katika Mpango wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umasikini Zanzibar (MKUZA), sekta ya utalii ndio sekta mama na nyegine zimekuwa zikiongeza nguvu hivyo inahitaji kuendelea kuungwa mkono ndani na nje ya nchi.

Dk. Shein aliyasema hayo wakati alipofanya mazungumzo na  Balozi mpya wa Tanzania nchini Canada Mhe. Jack Mugendi Zoka,  Ikulu mjini Zanzibar aliyefika kwa ajili ya kuaga kwenda katika kituo chake kipya cha kazi nchini humo  kufuatia uteuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete hivi karibuni.

Katika maelezo yake Dk. Shein alimueleza Balozi huyo mpya wa Tanzania nchini Cadana kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imekuwa ikifanyaa juhudi za makusudi katika kuhakikisha sekta ya utalii inaimarika na inaendelea kuwa sekta mama na muhimu hapa nchini.

Dk. Shein alisisitiza kuwa katika hatua ya uekezaji kwenye sekta ya utalii, serikali imejikita zaidi na uekezaji kwenye ujenzi wa mahoteli ya kitalii kwa kuzingatia kuwa ni miongoni mwa vivutio vikuu katika sekta hiyo ambayo imekuwa aikichangia asilimia 80 ya fedha za kigeni hapa Zanzibar.

Alisema kuwa kutokana na umuhimu huo hivi sasa hapa Zanzibar tayari kuna hoteli kadhaa za daraja la kwanza huku bado serikali ikiendelea kuwakaribisha na kuwahamasisha wawekezaji kutoka katika nchi mbali mbali duniani kuja kuekeza katika ujenzi wa hoteli za kitalii hapa Zanzibar.

Aidha, Dk. Shein alitumiaa fursa hiyo kumpongeza Balozi Zoka kwa kuteuliwa kuwa Balozi nchini humo na kueleza kuwa Zanzibar na Canada  zimekuwa na mashirikiano makubwa hivyo, ipo haja ya kuyakuza na kuyaimarisha zaidi ili kukuza uhusiano uliopo.

Akieleza juu ya sekta ya uwekezaji Dk. Shein alimueleza Balozi Zoka kuwa mbali ya kutilia mkazo uwekezaji katika ujenzi wa mahoteli pia, Serikali imekuwa ikitilia mkazo uwekezaji katika Hospitali za kisasa za binafsi ambazo zinatibu maradhi maalum.

Akiyataja maradi hayo, Dk. Shein alisema kuwa ni pamoja na maradi ya moyo, sukari, figo na mengineyo ambayo bado huduma zake za tiba zinahitajika kwa kiasi kikubwa hapa nchini, hivyo ipo haja kwa wawekezaji kutoka nchini Canada kuangalia fursa hiyo.

Dk. Shein alisema kuwa kupitia Shirika lake la Maendeleo la Kimataifa la Canada (CIDA) , nchi hiyo imeweza kuiunga mkono Zanzibar kwa kiasi kikubwa.

Akizungumzia kuhusu nchi ya Cuba ambapo Balozi Zoka pia, ataiwakilisha Tanzania, Dk. Shein alimueleza Balozi huyo kuwa nchi hiyo imekuwa na mahusiano ya kihistoria kati yake na Zanzibar na kueleza kuwa ni miongoni mwa nchi za mwanzo kuyatambua Mapinduzi ya  Zanzibar ya Januari 12, 1964.

Dk. Shein alimueleza Balozi Zoka haja ya kukuza uhusiano na ushirikiano na Cuba ambayo Balozi Zoka pia, ataifanyia kazi kwani  ni nchi rafiki wa Zanzibar ambayo imeweza kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuimarisha sekta ya afya kwa kusaidia kuleta madaktari wakufunzi pamoja na uanzishwaji wa Chuo cha Udaktari cha Zanzibar  kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Matanzas cha Cuba.

Nae Balozi mpya wa Tanzania nchini Canada Mhe. Jack Mugendi Zoka alitoa pongezi kwa mafanikio yaiopatikana hapa Zanzibar chini ya uongozi wa Dk. Shein katika kuimarisha sekta za maendeleo ikiwemo sekta ya utalii.

Balozi Zoka aliahidi kuwa atatumia fursa aliyoipata ya kuwawakilisha Watanzania wakiwemo Wazanzibari nchini Canada sambamba na kuitangaza Zanzibar kiutalii kutokana na vivutio vyake vilivyopo.

Aidha, Balozi huyo alimueleza Dk. Shein kuwa ameweza kukutana na wadau wa sekta ya utalii paamoja na uwekezaji wa hapa Zanzibar na kuweza kufanya nao mazungumzo pamoja na kubadilishaja nae mawazo juu ya kuzifanyia kazi sekta hizo atakapokuwa nchini humo ambao wameahidi kushirikiana nae kwa maslahi ya nchi.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Wednesday, November 26, 2014

UKAWA WACHANJA MBUGA KUSAKA UUNGWAJI MKONO


KATIBU MKUU WA CHAMA CHA WANANCHI CUF MAALIM SEIF SHARIF HAMAD AMESEMA USHIRIKIANO WA VYAMA VINNE VYA UPINZANI (UKAWA) NDIO JIBU SAHIHI KWA WANANCHI WENGI WALIOKUWA WAKIHOJI IWAPO CCM ITANG’OLEWA NANI ATACHUKUA NAFASI HIYO NA KUKAMILISHA NDOTO ZA WATANZANIA KUWA NA MAISHA MAZURI.

 

MAALIM SEIF AMESEMA HAYO WAKATI AKIHUTUBIA MIKUTANO YA HADHARA, AKIWA KATIKA ZIARA YA KICHAMA MKOANI MTWARA, AMBAPO AMEKUWA AKIZINDUA MATAWI MAPYA YA CUF NA KUHIMIZA WANANCHI KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA KURA NA KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA DISEMBA 14 MWAKA HUU KUKIWEKA UPANDE CCM.

 

KATIBU MKUU WA CUF AMESEMA KWA MIAKA MINGI WANANCHI WALIKUWA WAKIJIULIZA NANI ATACHUKUA NAFASI YA CCM KUONGOZA DOLA, LAKINI SASA WANANCHI HAWANA HOFU TENA BAADA YA VYAMA VYA CUF, CHADEMA, NCCR MAGEUZI NA NLD KUAMUA KUSHIRIKIANA KUKIONDOA MADARAKANI CCM.

 

AMESEMA CCM BAADA YA KUONGOZA NCHI KWA MIAKA 53 TOKEA UHURU KIMESHACHOKA NA HAKINA JIPYA TENA KINALOWEZA KUWAFANYIA WANANCHI NA KIMEBAKI KUONESHA KIBRI NA UTAWALA WA MABAVU DHIDI YA WANANCHI.

AMEWATAKA WANANCHI WASIDANGANYIKE KUWA CCM INAWEZA KUTOA MGOMBEA BORA WA URAIS KWA SABABU VIONGOZI WOTE WA CCM WANAFUATA MFUMO MMOJA WA CHAMA CHAO AMBAO KWA SASA HAUWEZI KUWALETEA MABADIKO YA MSINGI WANANCHI WA TANZANIA.

 

AKIZINDUA BAADA YA KUZINDUA TAWI JIPYA LA CUF KATA YA UFUKONI, MANISPAA YA MTWARA, MAALIM SEIF AMESEMA WANANCHI WAMECHOKA KWA BAKORA ZA CCM.

 

AMESEMA SERA ZA CCM ZIMEWADHOOFISHA WANANCHI WALIO WENGI HASA VIJANA KIASI KWAMBA VIJANA WENGI WANAONEKANA NI WAZEE NA UNATAMANI KUWAAMKIA KUTOKANA NA MAISHA DUNI CHINI YA SERA ZA CCM.

 

MAALIM SEIF AMESEMA KAZI ILIYO MBELE YA WANANCHI HIVI SASA NI KUJITOKEZA KWA WINGI KWENDA KUJIANDIKISHA KATIKA ZOEZI LINALOENDELEA ILI WAWEZE KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA MWEZI UJAO NA KUKIPA SALAMU CCM MUDA WAO WA KUONDOKA UMEFIKA.

 

NAIBU MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI NA MAWASILIANO YA UMMA WA CUF, ABDUL KAMBAYA AMESEMA KAMA KUNA WATU WANAPASWA KUPELEKEWA MAGARI YA DERAYA NA KUADHIBIWA NI VIONGOZI WA CCM WANAOCHOTA FEDHA ZA WANANCHI KWA NJIA YA UFISADI NA SIO WANANCHI WA MTWARA.

 

KAMBAYA AMESEMA HIVI SASA TAIFA LIKO NJIA PANDA NA KAMWE WANANCHI HAWAWEZI KUNYAMAZA KUTOKANA NA WIZI NA UFISADI UNAOFANYWA AMBAO UNASABABISHA MADHARA MAKUBWA KWA WANANCHI WANYONGE.

VIONGOZI WA UAMSHO WAENDELEA KUSOTA RUMANDE


MAHAKAMA KUU ya Tanzania, imeanza kusikiliza maombi ya AMIRI MKUU WA Jumuiya ya MAIMAMU Zanzibar (JumAZA), SAMAHATU Sheikh Farid Hadi Ahmed na wenzake waliyoomba Mahakama KUpitiA kesi ya awali inayowakabili.

Kusikilizwa kwa maombi hayo, kunatokana na mashtaka ya kula njama ya kuingiza watu nchini, kushiriki KATIKA vitendo vyaKIgaidi pamoja na kusaidia kufanyika kwa vitendo hivyo.

Maombi hayo yalisikilizwa JANA mbele ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Dk Fauzi Twaib, Wakili wa Serikali, Peter Njike akisaidiana na George Barasa.

Awali wakili wa utetezi, Abubakar Salum alidai kwamba waMEiomba Mahakama KUtoA tafsiri, kwanini watu wawili walioingizwa nchini kufanya vitendo hivyo, hawafikishwi mahakamani, pia ni raia wa nchi gani, huku mashitaka hayo yakiwa hayaonyeshi lini na eneo gani vitendo hivyo vimefanyika.

Kwa upande wa wakili wa serikali, Njike aliiomba Mahakama impe nafasi ya kusikilizwa, kwa kuwa upande wa Jamhuri ulikosa majibu kutokana na maombi hayo kufikishwa kwa hati ya dharura.

Baada ya kupewa nafasi ya kusikilizwa, Njike aliiomba Mahakama KUpangA tarehe nyingine ili apate muda wa kutoa majibu kuhusu maombi hayo.

Jaji Twaib aliahirisha shauri hilo hadi Desemba 4, mwaka huu ili upande wa Jamhuri uweze kutoa majibu.

Hata hivyo, Jaji Twaib alisema kama upande wa Jamhuri utakuwa na jambo la ziada kuhusu maombi hayo yanayotakiwa kufikishwa Novemba 28, mwaka huu huku upande wa utetezi kama wana jambo la ziada walifikishe Desemba 1, mwaka huu.

Mbali na Farid, washtakiwa wengine wanaokabiliwa na mashtaka hayo ni MAUSTADH Nassoro Hamad, Hassan Bakari, Ahtari Humoud, Mohamed Isihaka, Abdallah Hassan, Hussein Mohamed, Juma Sadala na Said Kassim.

 Wengine ni Khamis Amour, Abubakar Abdallah, Salum Ali, Salum Amour, Alawi Othman, Rashid Ally, Amir Khamis, Kassim Salum na Said SheKhe.

Kesi inayowakabili inadaiwa kuwa kati ya Januari 2013 na Juni mwaka huu .

washtakiwa hao kwa pamoja WAMEDAIWA KUpanga njama ya kutenda makosa hayo ya kula njama za kusaidia na kuwezesha kufanyika vitendo vya kigaidi.

Monday, November 24, 2014

WENYE UWEZO WASAIDIENI WASIOJIWEZA KWENDA NJE KIMATIBABU


WILAYA YA MJINI.

WATU WENYE UWEZO WAMETAKIWA KUJITOKEZA KUMSAIDIA KIJANA SULEIMANA OTHMAN ALI ALIELAZWA KATIKA HOSPITALI KUU YA MNAZI MMOJA KWA KUSUMBULIWA NA UVIMBE MKUBWA MGONGONI.

KIJANA OTHMAN MWENYE UMRI WA MIAKA 19 AMEPATWA NA TATIZO LA UVIMBE MKUBWA KWENYE MGONGO WAKE BAADA YA KUPATWA NA AJALI  YA KUGONGWA NA VESPA KWA MUDA MREFU.

AKIWA KATIKA HOSPITALI KUU YA MNAZI MMOJA ILISHINDIKANA KUPATA MATIBABU KUTOKANA NA DAMU NYINGI ALIOTOKA WAKATI WA UPASUAJI NA KULAZIMIKA KUSHONWA BILA YA KUFANYIWA UPASUAJI ULIYOKUWA UMEKUSUDIWA.

FAMILIA YA KIJANA HUYO IMELAZIMIKA KUOMBA USHIRIKIANO WA KUPATA MSAADA KWA AJILI YA KUMGHARAMIA  MTU MMOJA WA FAMILIA KUFUATANA NAE NCHINI INDIA KWA AJILI YA MATIBABU, KUTOKANA NA GHARAMA KUWA NI KUBWA NA UWEZO WAO NI MDOGO KATIKA FAMILIA.

 

KIJANA SULEIMANA OTHMAN ALI AMELAZWA HOSPITALI KUU YA MNAZI MMOJA WODI YA CHINI UPANDE WA DIRISHA LA DAWA KWENYE KITANDA NO 12.

VIJANA WATAKIWA KUTUMIA FURSA ZA KITAALUMA


WILAYA YA MAGHRIBI

 

VIJANA NCHINI WAMESHAURIWA KUZITUMIA FURSA ZA KITAALUMA ZILIZOPO,ILI  KUJIJENGEA UWEZO  WA  KUJIAJIRI  WENYEWE  SAMBAMBA  NA  KUINUA  UCHUMI  WA  TAIFA.

 

USHAURI  HUO UMETOLEWA  NA  WAJASIRIAMALI  KUTOKA  MAUNGANI  UWANDANI  WAKATI  WALIPOKUWA  WAKIPATA  MAFUNZO  YA  UTENGENEZAJI  WA  SABUNI  KIJIJINI  KWAO.

 

WAMESEMAA  KUWA  VIJANA  WENGI  HAWATAKI  KUJIFUNZA  MAFUNZO  YA  UJASIRIAMALI  KWA  KUONA  KUWA  UJASIRIAMALI  HAUNA  FAIDA  NDANI  YAKE.

 

AIDHA  WAMESEMA  NI  VYEMA  KWA  VIJANA  NA SERIKALI  KULIPA  UMUHIMU  SUALA  LA  MAFUNZO  YA  UJASIRIAMALI  ILI  KUPATA  TAALUMA  YA  UHAKIKA  KWA  MAENDELEO  YAO  NA  TAIFA  KWA  UJUMLA.

 

WAKIWAKILISHA  MAELEZO  JUU YA  TAALUMA  WALIYOIPATA   WAMESEMA  WANAJIFUNZA  KUTENGENEZA  SABUNI  ZA  AINA  ZOTE,KUSHONA  NGUO  PAMOJA  NA  UPISHI  WA  VYAKULA  MBALIMBALI.

MAALIM SEIF NA WAJUMBE WA MAGEREZA AFRIKA MASHARIKI


ZANZIBAR

 

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR, MHE. MAALIM SEIF SHARIF HAMAD AMESEMA NI JUKUMU LA TAASISI ZINAZOSIMAMIA MAGEREZA KATIKA ENEO LA AFRIKA MASHIRIKI KUWEKA MAZINGIRA BORA YATAKAYOWEZA KUHAKIKISHA USALAMA NA HAKI KWA WAFUNGWA NA WATU WALIOMO VIZUIZINI.

 

MAALIM SEIF AMESEMA HAYO ALIPOKUWA AKIFUNGUA MKUTANO WA KANDA UNAOWASHIRIKISHA WAJUMBE KUTOKA ETHIOPIA, MAURITIUS, KENYA, UGANDA NA TANZANIA KUJADILI USALAMA MAGEREZANI, ADHABU MBADALA, KUTOKOMEZA DAWA ZA KULEVYA PAMOJA NA MARADHI YA UKIMWI ULIOFANYIKA HOTELI YA ZANZIBAR OCEAN VIEW KILIMANI MJINI ZANZIBAR.

 

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS AMESEMA KUNA KILIO KIKUBWA MIONGONI MWA MATAIFA TAFAUTI KUTOKANA NA KUWEPO MAZINGIRA YASIYORIDHISHA KATIKA MAGEREZA HALI AMBAYO IMEKUWA NI CHANZO CHA KUVUNJWA KWA HAKI ZA WAFUNGWA AMBAPO PIA HUCHANGIA WATU HAO KUPATA ATHARI ZA KIAFYA.

 

AMELEZA KUWA MSONGAMANO WA WAFUNGWA NA MAHABUSU KATIKA MAGEREZA MENGI UNACHANGIA KUKOSEKANA KWA HUDUMA KAMA VILE KUPATA MWANGAZA WA KUTOSHA, HEWA SAFI AMBAPO MATOKEO YAKE KIWANGO CHA MARADHI YA KIFUA KIKUU NA MAAMBUKIZI YA UKIMWI NI YA KIWANGO CHA JUU KATIKA SEHEMU HIZO.

 

MAALIM SEIF AMESEMA HAYO YANAJITOKEZA LICHA YA KUWEPO MIKATABA YA KIMATAIFA JUU YA HAKI ZA WATU WANAOTUMIKIA VIFUNGO NA WALIOPO VIZUIZINI NA KWAMBA MKUTANO HUO UNAPASWA KUJA NA MAJIBU YA NAMNA BORA KWA NCHI HIZO ZINAVYOWEZA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO HIZO NA KUDUMISHA HAKI ZA WATU HAO.