RAIS WA ZANZIBAR AMBAYE PIA NI MWENYEKITI
WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN AMESEMA SERIKALI IMEAMUA KUAGIZA
VIFAA VIPYA VYA UJENZI WA BARABARA ILI KUHAKIKISHA KUWA MIRADI YOTE YA BARABARA
ILIYOPANGWA IWEZE KUTEKELEZWA NA KUKAMILIKA IFIKAPO MWEZI AGOSTI MWAKA UJAO.
AKIZUNGUMZA NA VIONGOZI WA
MASHINA NA WENYEVITI WA MASKANI ZA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA KASKAZINI ‘B’,
DK. SHEIN AMESEMA SERIKALI INAFANYA HIVYO ILI KUONGEZA KASI YA UJENZI WA
BARABARA KWA KUWA HIVI SASA VIFAA VILIVYOPO HAVIWEZI KUTEKELEZA MRADI ZAIDI YA
MMOJA KWA WAKATI MMOJA.
HATA HIVYO AMESEMA KUWA SERIKALI
INATAZWA NA MAMBO MADOGO MADOGO LAKINI FEDHA ZA KUTOSHA ZIPO KUFANYA KAZI HIYO
HIVYO WAMEAMUA KUAGIZA VIFAA ZAIDI ILI KUONGEZA KASI KWA KUTEKELEZA MIRADI
ZAIDI YA MOJA KWA WAKATI MMOJA HIVYO MATARAJIO NI KUKAMILISHA MIRADI HIYO
KWENYE MWEZI AGOSTI 2015.
SAMBAMBA NA HAYO AMEWAHAKIKISHIA
WANANCHI WA WILAYA HIYO KUWA BARABARA ZA WILAYA HIYO ZILIZOMO KATIKA MPANGO WA
SERIKALI ZITAJENGWA KATIKA KIPINDI HICHO HIVYO WANACHOTAKIWA KWAO NI KUWA
SUBIRA.
No comments:
Post a Comment