WILAYA YA MJINI.
WATU WENYE UWEZO WAMETAKIWA KUJITOKEZA
KUMSAIDIA KIJANA SULEIMANA OTHMAN ALI ALIELAZWA KATIKA HOSPITALI KUU YA MNAZI
MMOJA KWA KUSUMBULIWA NA UVIMBE MKUBWA MGONGONI.
KIJANA OTHMAN MWENYE UMRI WA MIAKA 19 AMEPATWA
NA TATIZO LA UVIMBE MKUBWA KWENYE MGONGO WAKE BAADA YA KUPATWA NA AJALI
YA KUGONGWA NA VESPA KWA MUDA MREFU.
AKIWA KATIKA HOSPITALI KUU YA MNAZI MMOJA
ILISHINDIKANA KUPATA MATIBABU KUTOKANA NA DAMU NYINGI ALIOTOKA WAKATI WA
UPASUAJI NA KULAZIMIKA KUSHONWA
BILA YA KUFANYIWA UPASUAJI ULIYOKUWA UMEKUSUDIWA.
FAMILIA YA
KIJANA HUYO IMELAZIMIKA KUOMBA USHIRIKIANO WA KUPATA MSAADA KWA AJILI YA
KUMGHARAMIA MTU MMOJA WA FAMILIA KUFUATANA NAE NCHINI INDIA KWA AJILI YA
MATIBABU, KUTOKANA NA GHARAMA KUWA NI KUBWA NA UWEZO WAO NI MDOGO KATIKA
FAMILIA.
KIJANA
SULEIMANA OTHMAN ALI AMELAZWA
HOSPITALI KUU YA MNAZI MMOJA WODI YA CHINI UPANDE WA DIRISHA LA DAWA KWENYE
KITANDA NO 12.
No comments:
Post a Comment