KATIBU
MKUU WA CHAMA CHA WANANCHI CUF MAALIM SEIF SHARIF HAMAD AMESEMA USHIRIKIANO WA
VYAMA VINNE VYA UPINZANI (UKAWA) NDIO JIBU SAHIHI KWA WANANCHI WENGI WALIOKUWA
WAKIHOJI IWAPO CCM ITANG’OLEWA NANI ATACHUKUA NAFASI HIYO NA KUKAMILISHA NDOTO
ZA WATANZANIA KUWA NA MAISHA MAZURI.
MAALIM SEIF AMESEMA HAYO WAKATI
AKIHUTUBIA MIKUTANO YA HADHARA, AKIWA KATIKA ZIARA YA KICHAMA MKOANI MTWARA,
AMBAPO AMEKUWA AKIZINDUA MATAWI MAPYA YA CUF NA KUHIMIZA WANANCHI KUJIANDIKISHA
KATIKA DAFTARI LA KURA NA KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA DISEMBA 14
MWAKA HUU KUKIWEKA UPANDE CCM.
KATIBU MKUU WA CUF AMESEMA KWA MIAKA
MINGI WANANCHI WALIKUWA WAKIJIULIZA NANI ATACHUKUA NAFASI YA CCM KUONGOZA DOLA,
LAKINI SASA WANANCHI HAWANA HOFU TENA BAADA YA VYAMA VYA CUF, CHADEMA, NCCR
MAGEUZI NA NLD KUAMUA KUSHIRIKIANA KUKIONDOA MADARAKANI CCM.
AMESEMA
CCM BAADA YA KUONGOZA NCHI KWA MIAKA 53 TOKEA UHURU KIMESHACHOKA NA HAKINA
JIPYA TENA KINALOWEZA KUWAFANYIA WANANCHI NA KIMEBAKI KUONESHA KIBRI NA UTAWALA
WA MABAVU DHIDI YA WANANCHI.
AMEWATAKA
WANANCHI WASIDANGANYIKE KUWA CCM INAWEZA KUTOA MGOMBEA BORA WA URAIS KWA SABABU
VIONGOZI WOTE WA CCM WANAFUATA MFUMO MMOJA WA CHAMA CHAO AMBAO KWA SASA HAUWEZI
KUWALETEA MABADIKO YA MSINGI WANANCHI WA TANZANIA.
AKIZINDUA
BAADA YA KUZINDUA TAWI JIPYA LA CUF KATA YA UFUKONI, MANISPAA YA MTWARA, MAALIM
SEIF AMESEMA WANANCHI WAMECHOKA KWA BAKORA ZA CCM.
AMESEMA
SERA ZA CCM ZIMEWADHOOFISHA WANANCHI WALIO WENGI HASA VIJANA KIASI KWAMBA
VIJANA WENGI WANAONEKANA NI WAZEE NA UNATAMANI KUWAAMKIA KUTOKANA NA MAISHA
DUNI CHINI YA SERA ZA CCM.
MAALIM
SEIF AMESEMA KAZI ILIYO MBELE YA WANANCHI HIVI SASA NI KUJITOKEZA KWA WINGI
KWENDA KUJIANDIKISHA KATIKA ZOEZI LINALOENDELEA ILI WAWEZE KUSHIRIKI KIKAMILIFU
KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA MWEZI UJAO NA KUKIPA SALAMU CCM MUDA WAO
WA KUONDOKA UMEFIKA.
NAIBU
MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI NA MAWASILIANO YA UMMA WA CUF, ABDUL KAMBAYA
AMESEMA KAMA KUNA WATU WANAPASWA KUPELEKEWA MAGARI YA DERAYA NA KUADHIBIWA NI
VIONGOZI WA CCM WANAOCHOTA FEDHA ZA WANANCHI KWA NJIA YA UFISADI NA SIO
WANANCHI WA MTWARA.
KAMBAYA
AMESEMA HIVI SASA TAIFA LIKO NJIA PANDA NA KAMWE WANANCHI HAWAWEZI KUNYAMAZA
KUTOKANA NA WIZI NA UFISADI UNAOFANYWA AMBAO UNASABABISHA MADHARA MAKUBWA KWA
WANANCHI WANYONGE.
No comments:
Post a Comment