SERIKALI YA JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu imesema kuwa
itaendelea kuwapatia wananchi takwimu sahihi zinazohusu sekta mbalimbali ili
kuwajengea uwezo wa kushiriki katika ngazi za maamuzi na masuala mbalimbali
nchini.
Kauli hiyo imetolewa
NA Waziri wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Omar
Yussuf Mzee wakati akifungua rasmi maadhimisho ya Siku ya Takwimu
Afrika jijini Dar es salaam yanaoongozwa na kauli mbiu Takwimu Huria kwa
uwajibikaji na ushirikishwaji wa wadau wote.
Amesema KUWA
upatikanaji wa taarifa na takwimu sahihi kwa wananchi unaongeza
ushiriki wao katika maamuzi na kuwajengea uwezo wa kutathmini utendaji wa
Serikali katika masuala mbalimbali yakiwemo mapato na matumizi.
Amesema KUWA Ofisi
ya Taifa ya Takwimu itaendelea kuhakikisha kuwa takwimu mbalimbali zinapatikana
kwa urahisi kupitia mtandao, machapisho na mifumo rahisi ili kuwawezesha
wananchi na wadau mbalimbali kuzipata WATAKApozihitaji.
Amefafanua kuwa
upatikanaji wa takwimu huria unawawezesha wananchi kujua sababu zinazoifanya
serikali kutekeleza maamuzi mbalimbali, kuongeza uwajibikaji na kuwawezesha
kupima matokeo ya sera za Serikali, kutathimini matumizi ya Serikali na
kushiriki katika midahalo mbalimbali ya kitaifa.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Aldegunda
Kombo akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi hiyo amesema kuwa
maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika mwaka huu yameweka msisitizo katika
kuweka miundombinu ya kuwarahisishia wadau kupata takwimu sahihi kwa wakati.
Amesema KUWA maadhimisho
hayo licha ya kujadili masuala mbalimbali yanajikita katika kuweka msukumo wa
kuhakikisha kuwa takwimu sahihi zinawafikia wananchi na wadau mbalimbali wa
maendeleo bila vikwazo vyovyote ili kuongeza uwazi wa utendaji wa shughuli za
serikali serikali.
Naye mwakilishi kutoka nchi washirika wa maendeleo
Bw.Jacques Morisset akizungumza wakati wa maadhimisho hayo ameeleza kuwa
takwimu sahihi ni ufunguo wa maendeleo kwa nchi yoyote duniani.
No comments:
Post a Comment