tangazo
Thursday, June 5, 2014
MATAPELI
HUYO ALOWEKA POST YAKE KWENYE JINA LA JULAIBIN DARUWESHI NI MWIZI SIO JULAIBIN MWENYEWE MM SIHUSIKI NA MIKOPO KABISA
Tuesday, June 3, 2014
MUHIBIRI WA KIISLAM AUWAWA GARISA
nairobi.
Muhadhiri maarufu wakiislam ameuawa katika mji wa
Garissa kaskazini mashariki mwa Kenya.
Duru
za khbari zimearifu kuwa Sheikh Abdirashid Mohammad alipigwa risasi na kuuawa
na watu wasiojulikana Jumapili usiku mjini Garissa.
Mkuu
wa Polisi katika jimbo la Garissa Charles Kinyua amesema kuwa muuhadhiri huyo alipigwa risasi mara kadhaa kwa karibu
mita chache kutoka Msikiti wa Khalifa
karibu na Hospitali Kuu ya Garissa.
muhadhiri huyo Alikuwa amefika msikitini hapo kuswali swala
ya Isha.
Afisa
huyo wa polisi amesema kuwa lengo la waliomuua bado halijafahamika
Aidha amedai kuwa mhubiri huyo alikuwa na
wapinzani ambao hawakutaka ahubiri katika baadhi ya misikiti.
Duru
za khbari mjini Garissa zimedokeza kuwa Sheikh Abdirashid Mohammad aliwahi
kunusurika shambulizi kama hilo wakati alipoviziwa katika hoteli moja mjini
humo.
Katika
siku za hivi karibuni masheikh kadhaa wameuawa nchini Kenya kwa madai
yakujihusisha na kundi la al-shabab madai ambayo hayana msingi.
RAIS SHENI AMPONGEZA RAISI MPYA WA MALAWIPeter Mutharika
zanzibar.
Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein
amemtumia Salamu za Pongezi Rais Mpya wa Malawi Peter Mutharika kwa kuchaguliwa
kuwa Rais wa Malawi kufuatia ushindi wake katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo
uliofanyika hivi karibuni.
Katika salamu hizo Dk. Shein ameelezea
matumaini ya wananchi wa Zanzibar kuwa chini ya uongozi wa Mutharika, ndugu zao
wa Malawi wataendeleza umoja wao na kuimarisha maendeleo ya nchi yao.
dr shein amemtakia Rais Mutharika afya njema, kheri
na fanaka katika kuiongoza nchi yake.
ZANZIBAR KUTAFUTA WAFADHILI KWA AJILI YA KUBUNI NJIA MBADALA YA UMEME
ZANZIBAR.
NAIBU WAZIRI WA ARDHI,MAKAAZI,MAJI NA NISHATI HAJI
MWADINI MAKAME AMESEMA KUWA SEREKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMEANZA
MAZUNGUMZO NA NCHI WAFADHILI KUHUSU JINSI YAKUFANYA UTAFITI WAKUPATIKANA CHANZO
MBADALA CHA UMEME HAPA NCHINI.
AKIJIBU MASWALI YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI
KATIKA KIKAO KINACHOENDELEA HUKO BWENI WILAYA YA MAGHARIBI UNGUJA WAZIRI
MWADINI AMESEMA KUWA SEREKALI IMEAMUA KUFANYA UTAFITI WA UHAKIKA ILI KUPATIKANA CHANZO CHA KUDUMU CHA NISHATI YA
UMEME.
AKIZUNGUMZIA SUALA LA GHARAMA KUBWA ZA UMEME NCHINI
AMESEMA KUWA SUALA HILO LITAPATIWA UFUMBUZI BAADA YAKUPATIKANA KWA CHANZO
MBADALA CHA NISHATI HIYO.
ZANZIBAR NDIO CHIMBUKO LA UISLAM AFRIKA YA MASHARIKI
zanzibar.
IMEELEZWA KUWA ZANZIBAR NDIO CHANZO CHA UISLAM KATIKA UKANDA
WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI.
HAYO YAMEELEZWA NA
AMIRI SEIF L-HAK WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAISLAM HUKO MASJID SAID FUONI
MAHARIBIKO.
AMEWATAKA WAISLAM KUTUMIA NAFASI YAO WALIYONAYO KATIKA
UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI KUWAPOKEA NAKUWAKIRIBU WAGENI WATAKAOKUJA NCHINI
KUHUDHURIA KATIKA IJITIMAI YAKIMATAIFA INAYOTARAJIWA KUFANYIKA TAREHE 13 HADI
16 MWEZI HUU HUKO FUONI MIGOMBANI WILAYA YA MAGHARIBI UNGUJA.
AIDHA ALIM HUYO AMEWASISITIZA WAIsLAM KUJITOLEA KWA HALI
NA MALI ILI KUFANIKISHA IJTIMAI HIYO YENYE LENGO LAKUWAKUMBUSHA WAISLAM JUKUMU
WALILONALO DUNIANI KATIKA KUMTUMIKIA MOLA WAO.
HATA HIVYO AMIRI SEIF AMEWAKUMBUSHA WAISLAM KUYATUMIA
VIZURI MAISHA YAO YA DUNIA ILI KUACHA ATHARI NZURI YA TABIA NJEMA MARA BAADA
YAKUAGA DUNIA.
Friday, May 30, 2014
VIJANA WAWILI WAPELEKWA RUMANDE KWA WIZI WA MAZAO
Wilaya ya Micheweni .
Mahakama ya Wilaya
Konde imewapeleka rumande kwa muda wa wiki mbili vijana wawili wakaazi wa
Wilaya ya Wete kwa tuhuma za wizi wa mazao .
Vijana hao ni Shaban
Rajab Hamad mkaazi wa Bopwe na Khalfan Shaban Ali Mkaazi wa Mtambwe
ambao wanadaiwa kuiba nazi saba zenye thamani ya shilingi 3,500 mali ya Faki
Ali Faki Mkaazi wa Taifu wilaya ya Micheweni.
Mbele ya Hakimu wa
mahakama hiyo Abdalla Yahya Shamuhuna , mwendesha mashtaka wa serikali Ali
Amour ameiambia mahakama kuwa watuhumiwa hao wametenda kosa hilo mei 26 mwaka
huu majira ya saa saba za mchana .
Baada ya kusomewa
shitaka lao , Mtuhumiwa Shaban Rajab Hamad amekubali kutenda kosa hilo wakati
Khalfan Shaban Ali amekana kutenda kosa hilo .
Hata hiyo watuhumiwa
wote wako rumande hadi tarehe 09 mwezi ujao kesi yao itakapokuja kutajwa tena .
Wakati huo huo
mahakama hiyo pia imempeleka rumande hadi tarehe 03 mwezi ujao kijana Ali
Gharib Hamad mkaazi wa Tumbe akituhumiwa kupatikana na majani makavu
yanayosadikiwa kuwa ni bangi .
Kijana huyo
alikamatwa akiwa na majani hayo tarehe 25 mwezi huu majira ya saa kumi na moja
na nusu za jioni katika eneo la Saninga .
UWEKEZAJI KATIKA MAHOTELI YA KITALII KUTASAIDIA KUITANGAZA ZANZIBAR
ZANZIBAR.
Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuwa uwekezaji
wa hoteli za kisasa zenye hadhi ya Kimataifa, utaisaidia Zanzibar kujitangaza
kiutalii, na kuwafanya watalii wa hadhi ya juu na viongozi wa kimataifa
kushawishika kuitembelea Zanzibar.
Maalim Seif ametoa kauli hiyo wakati
akitembelea mradi wa ujenzi wa hoteli ya kisasa ya Grand Hyatt unaosimamiwa na
Kampuni ya Dubai katika eneo la Shangani, mkabala na jengo la Mambo msige mjini
Zanzibar.
Amesema kuwa kwa kipindi kirefu Zanzibar imekua
na upungufu wa Hoteli zenye hadhi ya kimataifa, na kwamba kukamilika kwa ujenzi
huo itakuwa faraja kwa Zanzibar, nakuhamasisha wawekezaji wengine katika sekta
mbali mbali za kiuchumi.
Katika ziara hiyo Maalim Seif alifuatana na
viongozi mbali mbali wakiwemo Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati,
Ramadhan Abdallah Shaaban pamoja na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko
Nassor Ahmed Mazrui.
Akitoa ufafanuzi kuhusiana na ujenzi huo,
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mji Mkongwe Issa Sarboko Makarani amesema kuwa ujenzi huo
umezingatia viwango vya Kimataifa na umeridhiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa
la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Amesema kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya
mazungumzo ya muda mrefu na shirika hilo linalojishughulisha na urithi wa
Kimataifa, ambapo Mji Mkongwe za Zanzibar ni sehemu ya urithi huo.
Amesema kuwa hoteli hiyo itakapokamilika
mwishoni mwa mwaka huu, itakuwa na uwezo wa kuwahudumia watalii wa hadhi ya juu
pamoja na viongozi mashuhuri wa kimataifa wakiwemo Marais.
Bw. Makarani amefahamisha kuwa hoteli hiyo ya
kisasa ambayo itakuwa na maegesho yaliyo chini ya jengo hilo itakuwa hoteli ya
kwanza ya aina yake kuwahi kujengwa Zanzibar.
Ujenzi wa hoteli hiyo unaotarajiwa kukamilika
mwishoni mwa mwaka huu, utagharimu dola milioni 35 za kimarekani, ambapo ujenzi
wake tayari umefikia zaidi ya asilimia 90.
Subscribe to:
Posts (Atom)