tangazo

tangazo

Wednesday, January 7, 2015

WAISLAM WASISITIZWA KUJENGA MSHIKAMANO



WILAYA YA CHAKE CHAKE.

WAUMINI WA DINI YA KIISLAM KOTE NCHINI WAMESISITIZWA  KUJENGA UMOJA NA MSHIKAMANO KATIKA KUJADILI MAENDELEO YA DINI YAO.

WITO HUO UMETOLEWA NA AL- USTADH RAMADHAN MUHAMED WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAISLAM KATIKA MSIKITI WA MKUU WA IJUMAA MACHOMANE CHAKE CHAKE KISIWANI PEMBA.

HATA HIVYO ALIM HUYO AMEWAKUMBUSHA WAISLAM KUYATUMIA MAADHIMISHO YA KUZALIWA KWA MTUME MUHAMMAD (S.W), KWA KUYATEKELEZA KWA VITENDO MAAMRISHO YA QUR-AN NA SUNNA ZAKE,ILI KUPATA MALIPO
MEMA SIKU YA HESABU.

AMEWATAKA WAISLAMU KUEPUKA KHITILAFU KATIKA DINI NA BADALA YAKE KUANGALIA MAMBO YA MSINGI KATIKA DINI YAO NA KUYAFANYIA KAZI.

MAPEMA MUHADHIR  HUYO AMEELEZAEA HAJA KWA WAISLAM WENYE UWEZO KUZITUMIA MALI ZAO KATIKA KUSAIDIA HARAKATI ZA MAENDELEO YA DINI KIISLAM.

Monday, January 5, 2015

WAISLAM WAASWA KUSHIRIKIANA

PEMBA.
NAIBU MUFTI MKUU WA ZANZIBAR SAMAHATU SHEIKH MAHAMOUD MUSSA WADI, AMEWATADHARISHA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU NCHINI, KUENDELEA KUJENGA UMOJA NA MSHIKAMANO WAO, WAKATI NCHI IKIELEKEA KATIKA  MABADILIKO YA UONGOZI MWAKA HUU.

SHEIKH MAHMOUD AMETOA AGIZO HILO KATIKA SHEREHE ZA MAULIDI YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) ZILIZOFANYIKA MJINI CHAKE CHAKE  KISIWANI PEMBA..

AMEWASISITIZA WAISLAM KUENDELEZA  UMOJA NA MSHIKAMANO WALIOOUNYESHA KATIKA MAADHIMISHO HAYO, HADI MWISHO WA MAISHA YAO.

MAPEMA KATIBU MSATAAFU WA OFISI YA MUFTI PEMBA SHEIKH ALI ABDALLA AMANI, AMEWASISITIZA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU, KUENDELEA KUSHIRIKIANA KATIKA MALEZI YA WATOTO ILI KUEPUKANA NA MAJANGA MBALI MBALI.


WANANCHI WATAKIWA KUEKEZA KATIKA ELIMU



mkoa wa mjini magharibi.

Mbunge wa Jimbo la Fuoni ndugu Said Mussa zubeir amewataka Wananchi wa Fuoni Mambo sasa kuwekeza zaidi katika sekta ya elimu kwa watoto wao.

mbunge huyo ameyasema hayo wakati akikabidhi Mabati na fedha taslim kwa Uongozi wa Skuli ya Maandalizi ya fuoni english media nassery school iliopo Fuoni Mambosasa.

Amesema kuwa elimu ndio rasilimali hivyo hakuna budi kwa wazazi na walezi kuekeza nguvu zao zaidi katika sekta ya elimu.

Aidha kiongozi huyo ameahidi kusaidia mailpo kwa Wanafunzi wanaoishi katika Mazingira Magumu,Mayatima na Watu wenye Ulemavu.

Mapema Uongozi wa Skuli hiyo umemueleza Mbunge wa Jimbo la Fuoni kuwa wanakabiliwa na ulipaji wa kodi kwa sehemu wanayosomeshea na ukosefu wa vitendea kazi zikiwemo kompyuta na fotokopi.

Akizungumzia Changamoto zinazowakabili Viongozi wa Skuli hiyo  ndugu said ameahidi kushirikiana nao kwa hali na mali katika kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo.

Skuli ya Maandalizi ya Kiislamu ya fuoni english media nassery school iliopo fuoni mambosasa imeanzishwa miaka mitatu iliopita. 

mnaendelea kuskiliza taarifa hii ya khabari kutoka radio adhana fm masjid jumuiya rahaleo zanzibar.

USUMBUFU WA ABIRIA WA FUONI



ZANZIBAR.

Baadhi ya Abiria wanaotumia daladala za Fuoni wamelalamikia usumbufu wanaofanyiwa na makonda na madereva kwa kutowafikiswa katika vituo wanavyokwenda.

Akizungumza na Redio Adhana Fm abiria mmoja wa daladala za fuoni darajani bi salome maarufu mama Yussuf amesema kuwa amepanda daladala ya Fuoni akiwa katika kituo cha Makaburini akielekea kituo cha kwa Ndundu ambapo chakushangaza Konda na Dereva wa gari hiyo walimshusha katika kituo cha ukanda wa Ghaza bila ya kumfikisha anakokwenda.

Amesema kuwa  mara baada ya kutakiwa kuteremka katika dalala hiyo bila ya kufika kwenye kituo alikataa na hatimaye Konda akaamua kumkaba shingoni na kumsababishia maumivu makali.

Ameeleza kuwa mara baada ya kufanyiwa kitendo hicho cha udhalilishaji alikimbilia kituo cha Polisi Kijito Upele na kutoa taarifa  lakini cha kusikitisha Askari waliekuwepo katika kituo hicho walimtolea maneno machafu.

Aidha bi Salome ameiomba Serikali kupitia Wizara husika kutoa elimu kwa Madereva na Makonda kutoa elimu ili waweze kuondokana na udhalilashaji hususan kwa Wanawake na Wanafunzi.

kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa kusini unguja juma sadi khamis amekiri kupokea taarifa za tukio hilo na amewataka madereva na makondakta kuwacha tabia zakuwatolea maneno yakihuni abiria.

ZAIDI YA SHILINGI MILIONI MOJA ZATUMIKA KUSAMBAZIA UMEME KATIKA KIJIJI CHA MOGA KIRAMA



wilaya ya kaskazini a.
Zaidi shilingi milioni moja khamsini na nane elfu na laki tano zimetumika katika usambazaji wa mradi mpya wa umeme katika kijiji cha Moga Kirama kilichopo wilaya ya kazkazini  “A”unguja.
Akizindua mradi huo Naibu waziri wa khabari,utamaduni,utalii na michezo Bihindi Hamad Khamisi amesema kuwa lengo lakuzinduliwa mradi huo ni kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi serikali ya kuwasogezea wananchi wake maendeleo ya haraka.
Amesema kuwa serikali kwa kushirikiana na wananchi itaendelea kutekeleza miradi ya kijamii ili kukuza maendeleo katika maeneo ya mjini na vijijini.
Naye meneja mkuu wa shirika la umeme Zanzibar (zeco) Hassani Ali Mbaruok amesema kuwa uzinduzi wa mradi huo katika kijiji cha Moga ni katika juhudi za serikali ya mapinduzi katika  kuhakikisha kuwa vijiji vyote vya unguja na pemba vinapata huduma iliyo bora zaidi.
Aidha amefahamisha kuwa wananchi wanawajibu mkubwa wa kulinda na kutunza miundo mbinu ya umeme ili huduma hiyo iwe endelevu.
Kwa upande wao wananchi wa kijiji cha Moga wamesema kuwepo kwa huduma hiyo kutaweza kuwaletea maendeleo kwa kasi zaidi na kukuza uchumi katika kjiji chao.

uzinduzi wa mradi huo  ni miongozi mwa shamra shamra za miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar.