ZANZIBAR.
Baadhi ya
Abiria wanaotumia daladala za Fuoni wamelalamikia usumbufu wanaofanyiwa na
makonda na madereva kwa kutowafikiswa katika vituo wanavyokwenda.
Akizungumza
na Redio Adhana Fm abiria mmoja wa daladala za fuoni darajani bi salome maarufu
mama Yussuf amesema kuwa amepanda daladala ya Fuoni akiwa katika kituo cha Makaburini
akielekea kituo cha kwa Ndundu ambapo chakushangaza Konda na Dereva wa gari hiyo
walimshusha katika kituo cha ukanda wa Ghaza bila ya kumfikisha anakokwenda.
Amesema
kuwa mara baada ya kutakiwa kuteremka
katika dalala hiyo bila ya kufika kwenye kituo alikataa na hatimaye Konda
akaamua kumkaba shingoni na kumsababishia maumivu makali.
Ameeleza
kuwa mara baada ya kufanyiwa kitendo hicho cha udhalilishaji alikimbilia kituo
cha Polisi Kijito Upele na kutoa taarifa
lakini cha kusikitisha Askari waliekuwepo katika kituo hicho walimtolea
maneno machafu.
Aidha bi
Salome ameiomba Serikali kupitia Wizara husika kutoa elimu kwa Madereva na
Makonda kutoa elimu ili waweze kuondokana na udhalilashaji hususan kwa Wanawake
na Wanafunzi.
kwa upande
wake kamanda wa polisi mkoa wa kusini unguja juma sadi khamis amekiri kupokea
taarifa za tukio hilo na amewataka madereva na makondakta kuwacha tabia
zakuwatolea maneno yakihuni abiria.
No comments:
Post a Comment