wilaya ya kaskazini
a.
Zaidi shilingi milioni moja khamsini na nane elfu
na laki tano zimetumika katika usambazaji wa mradi mpya wa umeme katika kijiji
cha Moga Kirama kilichopo wilaya ya kazkazini “A”unguja.
Akizindua mradi huo Naibu waziri wa khabari,utamaduni,utalii
na michezo Bihindi Hamad Khamisi amesema kuwa lengo lakuzinduliwa mradi huo ni
kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi serikali ya kuwasogezea wananchi wake
maendeleo ya haraka.
Amesema kuwa serikali kwa kushirikiana na
wananchi itaendelea kutekeleza miradi ya kijamii ili kukuza maendeleo katika
maeneo ya mjini na vijijini.
Naye meneja mkuu wa shirika la umeme Zanzibar
(zeco) Hassani Ali Mbaruok amesema kuwa uzinduzi wa mradi huo katika kijiji cha
Moga ni katika juhudi za serikali ya mapinduzi katika kuhakikisha kuwa
vijiji vyote vya unguja na pemba vinapata huduma iliyo bora zaidi.
Aidha amefahamisha kuwa wananchi wanawajibu
mkubwa wa kulinda na kutunza miundo mbinu ya umeme ili huduma hiyo iwe
endelevu.
Kwa upande wao wananchi wa kijiji cha Moga
wamesema kuwepo kwa huduma hiyo kutaweza kuwaletea maendeleo kwa kasi zaidi na
kukuza uchumi katika kjiji chao.
uzinduzi wa mradi huo ni miongozi mwa shamra shamra za miaka 51 ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
No comments:
Post a Comment