mkoa wa
mjini magharibi.
Mbunge wa
Jimbo la Fuoni ndugu Said Mussa zubeir amewataka Wananchi wa Fuoni Mambo sasa
kuwekeza zaidi katika sekta ya elimu kwa watoto wao.
mbunge huyo
ameyasema hayo wakati akikabidhi Mabati na fedha taslim kwa Uongozi wa Skuli ya
Maandalizi ya fuoni english media nassery school iliopo Fuoni Mambosasa.
Amesema kuwa
elimu ndio rasilimali hivyo hakuna budi kwa wazazi na walezi kuekeza nguvu zao zaidi
katika sekta ya elimu.
Aidha
kiongozi huyo ameahidi kusaidia mailpo kwa Wanafunzi wanaoishi katika Mazingira
Magumu,Mayatima na Watu wenye Ulemavu.
Mapema
Uongozi wa Skuli hiyo umemueleza Mbunge wa Jimbo la Fuoni kuwa wanakabiliwa na
ulipaji wa kodi kwa sehemu wanayosomeshea na ukosefu wa vitendea kazi zikiwemo kompyuta
na fotokopi.
Akizungumzia
Changamoto zinazowakabili Viongozi wa Skuli hiyo ndugu said ameahidi kushirikiana nao kwa hali
na mali katika kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo.
Skuli ya
Maandalizi ya Kiislamu ya fuoni english media nassery school iliopo fuoni
mambosasa imeanzishwa miaka mitatu iliopita.
mnaendelea
kuskiliza taarifa hii ya khabari kutoka radio adhana fm masjid jumuiya rahaleo
zanzibar.
No comments:
Post a Comment