WILAYA
YA CHAKE CHAKE.
WAUMINI
WA DINI YA KIISLAM KOTE NCHINI WAMESISITIZWA
KUJENGA UMOJA NA MSHIKAMANO KATIKA KUJADILI MAENDELEO YA DINI YAO.
WITO HUO
UMETOLEWA NA AL- USTADH RAMADHAN MUHAMED WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAISLAM KATIKA
MSIKITI WA MKUU WA IJUMAA MACHOMANE CHAKE CHAKE KISIWANI PEMBA.
HATA
HIVYO ALIM HUYO AMEWAKUMBUSHA WAISLAM KUYATUMIA MAADHIMISHO YA KUZALIWA KWA
MTUME MUHAMMAD (S.W), KWA KUYATEKELEZA KWA VITENDO MAAMRISHO YA QUR-AN NA SUNNA
ZAKE,ILI KUPATA MALIPO
MEMA
SIKU YA HESABU.
AMEWATAKA
WAISLAMU KUEPUKA KHITILAFU KATIKA DINI NA BADALA YAKE KUANGALIA MAMBO YA MSINGI
KATIKA DINI YAO NA KUYAFANYIA KAZI.
MAPEMA
MUHADHIR HUYO AMEELEZAEA HAJA KWA
WAISLAM WENYE UWEZO KUZITUMIA MALI ZAO KATIKA KUSAIDIA HARAKATI ZA MAENDELEO YA
DINI KIISLAM.
No comments:
Post a Comment