PEMBA.
NAIBU MUFTI MKUU WA ZANZIBAR SAMAHATU SHEIKH MAHAMOUD MUSSA WADI,
AMEWATADHARISHA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU NCHINI, KUENDELEA KUJENGA
UMOJA NA MSHIKAMANO WAO, WAKATI NCHI IKIELEKEA KATIKA MABADILIKO YA UONGOZI MWAKA HUU.
SHEIKH MAHMOUD AMETOA
AGIZO HILO KATIKA SHEREHE ZA MAULIDI YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) ZILIZOFANYIKA
MJINI CHAKE CHAKE KISIWANI PEMBA..
AMEWASISITIZA WAISLAM
KUENDELEZA UMOJA NA MSHIKAMANO
WALIOOUNYESHA KATIKA MAADHIMISHO HAYO, HADI MWISHO WA MAISHA YAO.
MAPEMA KATIBU
MSATAAFU WA OFISI YA MUFTI PEMBA SHEIKH ALI ABDALLA AMANI, AMEWASISITIZA
WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU, KUENDELEA KUSHIRIKIANA KATIKA MALEZI YA WATOTO ILI
KUEPUKANA NA MAJANGA MBALI MBALI.
No comments:
Post a Comment