tangazo
Wednesday, December 2, 2015
SIMBA KUANZA MECHI YA KIRAFIKI KESHO NA UPEPO MKALI (KIMBUNGA)
wachezaji wa timu ya simba wakiwa katika mazoezi yao uwanja wa amani zanzibar.
wachezaji wa timu ya kimbunga wakishangiria ushindi katika moja ya mechi zao.
Na: Abubakar Kisandu, Zanzibar.
Wekundu wa Msimbazi Simba kesho wanatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Kimbunga ambayo inashiriki ligi kuu soka visiwani Zanzibar, mchezo ambao utasukumwa saa10 za jioni kwenye dimba la Amaan.
Katika mchezo huo Simba watautumia kama ni mchezo wa kupata mazoezi na kuwaangalia wachezaji wao wanaotarajia kuwasajili katika dirisha hili dogo la usajili.
Mtandao huu tumefanikiwa kuzungumza na Abdul Mshangama ambae yeye ni mjumbe kamati tendaji wa timu hiyo akiwakilisha hapa Zanzibar na kusema kuwa watacheza michezo mitatu ya kirafiki kabla ya kuwavaa Azam siku ya jumamosi ya tarehe 12 ya mwezi huu kwenye mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara.
“ Kesho sisi Simba tutacheza mchezo wa kirafiki na timu ya Kimbunga, na pia mchezo mwengine tutacheza na kombain ya Unguja siku ya jumamosi, mechi hizi tutazitumia kuwaangalia wachezaji ambao tunatarajia kuwasajili ”. Alisema Mshangama.
Wakati wakijiandaa na msimu mpya Simba walipokuja Zanzibar walishinda michezo yao ya kirafiki yote walipoifunga kombain ya Zanzibar 2-1, pia wakaitwangwa Black Sailors 4-0, na michezo mengine wakaitwanga Polisi 2-0, wakaifunga Jangombe Boys 3-0, wakaipiga KMKM 3-2, wakatoka sare ya 0-0 na KVZ, hivyo wanahistoria nzuri kwa michezo ya kirafiki hapa visiwani kwa mwaka huu.
MAENDELEO YA SEKTA YA ZAO LA KARAFUU YAENDELEA KUIMARIKA ZAIDI.
Na Pili Khatib na Zuhura Omar, MUM
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Biashara la Taifa
Zanzibar ZSTC Mwanahija Almas Ali amesema Maendeleo ya Sekta ya Zao la Karafuu
inaendelea kuimarika zaidi Zanzibar hasa baada ya kuanzishwa kwa Mfuko wa
Maendeleo ya Karafuu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Makao Makuu ya ZSTC
Maisara Bi. Mwanahija alisema Mfuko huo ulianzishwa kuongeza nguvu jitihada za
Serikali za kuimarisha zao hilo la uchumi wa Taifa.
Alisema utafiti ulifanyika juu ya namna ya kufanya mageuzi
yenye tija katika Sekta ya Karafuu ndipo ikaoneka umuhimu wa kuanzisha Mfuko
huo ambapo muda mfupi baada ya kuanzishwa unaonekana kuleta faida katika
uimarishaji wa zao hilo.
“Madhumuni ya kuanzishwa kwa Mfuko wa Maendeleo ya Karafuu
ni kuhakikisha Sekta ya Karafuu inakua na kuimarika zaidi. Kuongeza idadi ya
mikarafuu na uzalishaji ambapo hivi sasa Wananchi wamehamasika zaidi katika
upandaji mikarafuu kwa wingi”. Alifahamisha Bi. Mwanahija.
Alisema Mfuko huo ambao upo chini ya Mkurugenzi Mwendeshaji
wa Shirika la ZSTC umejipanga kufanya sensa ya mikarafuu sambamba na kuwasajili
Wakulima na Wafanyabiashara wa zao hilo ili kurahisisha upatikanaji wa huduma.
Aidha alifahamisha kuwa kupitia Mfuko huo na kwa
kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Maliasili kutafanyika tafiti kwenye kila
eneo linayohusu zao la karafuu kwa lengo la kugundua changamoto na kuzifanyia
kazi.
Alisema Shirika la ZSTC kwa kushirikiana na Wadau wengine
inakamilisha mpango maalumu wa kuziongezea hadhi na thamani karafuu za Zanzibar
kupitia mradi wa ‘Branding’ ili kuongezeka kwa uzalishaji kwenda sambamba na
kuongezeka kwa tija kwa Wakulima na Taifa.
Alisema hivi sasa mpango huo upo katika kutafuta vinasaba
vinavyoonyesha ubora wa karafuu za Zanzibar kupitia Mkemia Mkuu wa Serikali
Zanzibar.
Alisema kupitia Mfuko huo Shirika limeongeza jitihada za
kutoa elimu kwa Wakulima juu ya uchumaji na uanikaji unaotakiwa ili kulinda
ubora wa zao hilo katika soko la nje.
Alisema Mfuko huo umekuwa ni msaada mkubwa katika
uimarishaji wa zao la karafuu hasa kwa Wakulima ambapo unatoa fidia kwa
Wakulima wanaopata ajali wakati wa uchumaji kupitia Shirika la Bima Zanzibar.
Alifahamisha kuwa Mfuko huo umelipa bima ya milioni 60 kwa
Shirika la Bima ili kuwafidia Wakulima 100 wanaokisiwa kupata ajali katika
zoezi la uchumaji wa karafuu mwaka 2015/2016 ambapo hadi sasa tayari watu tisa
wameripotiwa kupata ajali wote kutoka Pemba.
Alisema Wakulima wanaendelea kupata mikopo ya uchumaji
kupitia Mfuko huo na alifahamisha kuwa katika bajeti ya 2015/2016 Mfuko
umepanga kutumia milio 140 kwa ujenzi wa barabara ya Ng’omeni ikiwa ni msaada
wa kusadia miundombinu ya sehemu za uzalishaji wa karafuu.
Akizungumzia makadirio ya mavuno ya karafuu ya mwaka
2015/2016 Mkurugenzi huyo alisema Shirika limekadiria kununua tani 2800 mpaka
3200 katika mwaka huo.
MELI MPYA YA MV MAPINDUZI( II)YAWASILI BANDARI YA ZANZIBAR.
Meli
ya MV MAPINDUZI II yatia nanga Bandari kuu ya Zanzibar ikitokea Korea Kusini.
Meli mpya ya MV. MAPINDUZI II ikiwa nje kidogo ya Bandari ya Zanzibar kabla ya kufunga gati Bandarini hapo.
Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee akitoa maelezo kwa waandishi
wa Habari juu ya matumizi ya gharama zilizotumika mara baada ya kuwasili
kwa Meli ya MV. MAPINDUZI II Mjini Zanzibar.
Sehemu ya ndani ya Meli ya MV. MAPINDUZI II itakayotumika
kwa ajili ya mapumziko kwa abiria watakao safari.
Meli mpya ya MV. MAPINDUZI II ikiwa nje kidogo ya Bandari ya Zanzibar kabla ya kufunga gati Bandarini hapo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizaza ya Miundombinu waliofika
Bandari Kuu ya Zanzibar kushuhudia kuwasili kwa Meli mpya ya MV. MAPINDUZI II
ikitokea Korea kusini.
MELI MPYA YA MV.MAPINDUZI ( II) IMEWASILI BANDARINI ZANZIBAR
KWA AJILI YA KUANZA SAFARI ZAKE BAADA YA KUKAMILIKA UJENZI WAKE HUKO
KOREA YA
KUSINI.
HAFALA YA KUWASILI KWA MELI HIYO IMEONGOZWA NA WAZIRI WA
FEDHA OMAR YUSSUF MZEE AMBAPO AMESEMA UJENZI WA MELI HIYO NI AGIZO LA
RAISI WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOH’D SHEIN.
AMESEMA MELI HIYO BADO IKO KATIKA MIKONO YA WAJENZI HADI
SASA NA INATARAJIWA KUZINDULIWA RASMIN WIKI IJAYO NA RAIS WA ZANZIBAR DKT, ALI
MOH’D SHEIN AMBAYE NI MGENI RASMI KATIKA UZINDUZI HUO.
WAZIRI MZEE AMESEMA MELI HIYO INAVIFAA VYA KUTOSHA KAMA VILE
LIFE JACKET, PAMOJA NA BOTI NDOGO ILI KUWEKA USALAMA KWA ABIRIA WATAOSAFIRI
KATIKA MELI HIYO.
HATA HIVYO AMESEMA MELI HIYO ITASAFIRI PEMBA PAMOJA NA
DARE-SALAM HIVYO AMEWATAKA WANANCHI KUITUNZA MELI HIYO KWANI NI MATUNDA YAO.
NAE KATIBU MKUU WIZARA YA MIUNDO MBINU NA MAWASILIANO
ZANIZAR DK. JUMA MALIK AMESEMA LENGO KULIFANYA SHIRIKA LA MELI LIFANYE KAZI
KIBIASHARA ILI KUONGEZA PATO LA TAIFA.
AMEWAOMBA WANANCHI KUITUNZA NA KUITUMIA VIZURI MELI HIYO
KWANI WAMEFANYA KAZI KUBWA NA KUTUMIA GHARAMA HADI KUFIKIA KUKAMILIKA KWA MELI
HIYO.
SAMBAMBA NA HAYO AMESEMA MELI HIYO INA UWEZO WA KUPAKIA
ABIRIA WASIOPUNGUWA 1,200 PAMOJA NA TANI ZA MIZIGO 200.
MELI HIYO MPYA YA MV.MAPINDUZI ( II) IMETENGENEZWA KOREA
KUSINI NA KUGHARIMU JUMLA YA DOLA MIL.30.4 ZA MAREKANI AMBAPO UJENZI WAKE HADI
KUKAMILIKA UMECHUKUA JUMLA YA MIEZI 18.
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR
CHAMA CHA WANANCHI CUF CHAPATA MSHTUKO MKUBWA BAADA YA KUFANYIKA MABADILIKO YA GHAFLA KATIKA UONGOZI WA PBZ
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Chama Cha Wananchi (CUF) kimepokea kwa mshtuko mkubwa
taarifa za kufanyika mabadiliko ya ghafla ya uongozi wa Benki ya Watu wa
Zanzibar (PBZ) ambayo yametangazwa mwishoni mwa wiki iliyopita na mwanzoni mwa
wiki hii.
Mabadiliko hayo ya ghafla yalianza wiki iliyopita, pale
Mheshimiwa Omar Yussuf Mzee alipotangaza kufuta uteuzi wa Ndugu Ali Abdalla
Suleiman, Prof. Mohamed Warsame, na Ndugu Ahmed Amani Abeid Karume, kuwa
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa PBZ na kutangaza kuteua watu wengine kuchukua
nafasi zao.
Hatua hiyo ikafuatiwa na taarifa ya Ikulu iliyotolewa juzi,
tarehe 30 Novemba 2015, ambayo ilisema Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein amefuta
uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ),
Ndugu Juma Amour Mohamed, na nafasi yake kuteuliwa Ndugu Juma Ameir Hafidh.
CUF imepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za mabadiliko hayo
kwa sababu zifuatazo:
1. Mabadiliko hayo yamefanywa na watu
ambao vipindi vyao vya uongozi vimemalizika kikatiba:-
(i) Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar,
Ibara ya 28(2) Rais ataacha madaraka yake baada ya kumalizika miaka mitano
tokea tarehe alipokula kiapo cha uaminifu na kiapo cha kuwa Rais. Dk. Ali
Mohamed Shein alishamaliza muda huo tarehe 2 Novemba, 2015 baada ya kutimiza
miaka mitano tokea siku aliyoapishwa ambayo ni tarehe 3 Novemba, 2010.
(ii) Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, Ibara ya
42(2), Mawaziri ni lazima wawe wajumbe wa Baraza la Wawakilishi. Ibara ya 48(b)
inaeleza kwamba nafasi ya Waziri, Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Naibu Waziri
itakuwa wazi iwapo mjumbe ameacha kuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa
sababu nyengine zaidi ya kuvunjika kwa Baraza hilo. Katiba hiyo hiyo, Ibara ya
90(1) imetoa nafasi ya kipindi cha baina ya kuvunjika Baraza la Wawakilishi na
kuitishwa Baraza jipya kuwa si zaidi ya siku tisini. Baraza la Wawakilishi
lililopita lilivunjwa tarehe 13 Agosti, 2015 na hivyo siku tisini zimemalizika
tarehe 12 Novemba, 2015. Kwa kutilia nguvu zaidi, Ibara ya 92(1) inasema kwamba
“Maisha ya Baraza la Wawakilishi yataendelea kwa muada wa miaka mitano tangu
tarehe ile ulipoitishwa Mkutano wake wa kwanza baada ya kuundwa, ila tu pale
iwapo Baraza la Wawakilishi limevunjwa mapema kutokana na sababu mbali mbali
zilizoelezwa katika Katiba hii.” Ukizichukua Ibara zote hizi kwa pamoja
ni kwamba kwa sasa Baraza lililopita halipo tena kwa sababu zimeshapita siku
tisini tokea lilipovunjwa na pia Baraza la Wawakilishi jipya lililochaguliwa
tarehe 25 Oktoba, 2015 halijaitishwa. Kwa hivyo basi, Mawaziri waliokuwepo
hawana uhalali tena wa kuendelea kuwa Mawaziri kikatiba. Kwa msingi huo,
Mheshimiwa Omar Yussuf Mzee, kama ilivyo kwa waliokuwa Mawaziri wote, hana sifa
wala uhalali kikatiba wa kuendelea kuwa Waziri.
2. Kwa sababu waliofanya mabadiliko hayo
wameshamaliza vipindi vyao vya uongozi kikatiba, mabadiliko hayo yanaweza kuja
kupingwa uhalali wake. Hali hiyo inaweza kuja kuitia Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar katika msukosuko mkubwa kisheria na pengine hata hasara ya mabilioni
ya shilingi iwapo walioteuliwa kuchukua nafasi hizo watatekeleza madaraka
waliyopewa na kufanya maamuzi, na kukatokea mtu au watu ambao wataweza kuja
kudai kuwa wameathirika kutokana na maamuzi waliyoyafanya.
3. Mshtuko wetu unazidi unapoangalia
kwamba taasisi yenyewe inayohusika ni benki ya kibiashara ambayo inahudumia
maelfu ya wateja ndani na nje ya nchi na inafanya uhaulishaji wa fedha hadi
kimataifa (international transactions). Katika hali hiyo, zikija zikitokea kesi
za kimataifa basi tutakuwa tumeiweka Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) na
Serikali ambayo ndiyo mmiliki wake katika hali ngumu kisheria.
4. Mbali na hoja hizo za kikatiba na
kisheria, CUF tunapata mshtuko mkubwa zaidi tunapoangalia mazingira ya
mabadiliko hayo. Akiwa Mkurugenzi Mtendaji, Ndugu Juma Amour ndiye aliyefanya
kazi kubwa ya kuifufua benki hiyo baada ya kuikuta katika hali mbaya sana
iliyoachwa na uongozi wa Awamu ya Tano ya SMZ ambapo ilifikia hatua ya kutaka
kufutiwa leseni na Benki Kuu ya Tanzania (BOT).
5. Wajumbe watatu wa Bodi ya Wakurugenzi
walioondolewa ndiyo wajumbe waliokuwa na utalaamu na uzoefu wa hali ya juu
ambao hapana shaka yoyote ni sehemu ya mafanikio ya PBZ katika kipindi ambacho
benki hiyo imeshuhudia mafanikio makubwa. Wajumbe hawa waliteuliwa Novemba 2014
na kipindi chao ni miaka mitatu ambayo ingemalizika Novemba 2017.
6. Mshtuko mkubwa zaidi ni wakati huu
ambapo mabadiliko hayo ya ghafla ya uongozi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ)
yamefanyika. CUF na wananchi wa Zanzibar kwa ujumla tuna mashaka makubwa na
wasiwasi kwamba lengo la kuwaondoa viongozi hao wa PBZ ni kutaka kulazimisha
Serikali kukopa kinyume na taratibu kwa kiasi kikubwa cha fedha kutoka benki
hiyo, fedha ambazo ni za wateja, na pengine uongozi uliokuwepo ulionekana ni
kikwazo cha kufanikisha malengo hayo. Tunajiuliza kwamba lengo ni kukopa fedha
ili kugharimia uchaguzi wa marudio unaopigiwa chapuo na viongozi wa CCM
Zanzibar?
7. Hali hii inatia wasiwasi baada ya
kuona taasisi nyengine iliyokuwa imepata mafanikio makubwa yaani Mfuko wa
Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) ambao unatunza fedha za wafanyakazi wa
Serikali na wale wa sekta binafsi kufikishwa katika hali mbaya kifedha baada ya
SMZ kuchukua fedha zake na kugharimia miradi ambayo haina tija kiuchumi kama
ule wa Viwanja vya Kufurahishia Watoto Unguja na Pemba na miradi mingine kama
hiyo. Je, baada ya ZSSF sasa watu wanaelekea PBZ?
Kutokana na sababu hizo, CUF haikubaliani na mabadiliko hayo
ambayo dalili na ishara zote hazioneshi kwamba yana malengo mema kwa wananchi
wa Zanzibar ambao kupitia Serikali yao ndiyo wamiliki wa Benki ya Watu wa
Zanzibar (PBZ).
CUF tulitegemea kwamba Zanzibar tungejifunza kutokana na
hatua anazochukua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk. John
Pombe Magufuli, za kuziba mianya ya upotevu wa mapato ya Serikali, matumizi
mabaya ya fedha za umma na matumizi mabaya ya madaraka. Hata hivyo, kwa hatua
hizi zinazoendelea kufanywa na viongozi ambao wamemaliza vipindi vyao vya
kuwepo madarakani hapa Zanzibar, haionekani kwamba tuna malengo yanayofanana
katika kuwahudumia wananchi.
Tunaamini kwamba mwanya huu unaotumiwa na viongozi hawa
utaondoka pale Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) itakapokamilisha kazi ya
kutangaza matokeo ya uchaguzi wa Urais wa Zanzibar, kumtangaza mshindi na kutoa
nafasi kwa vyama vya CUF na CCM kuunda Serikali mpya ya Umoja wa Kitaifa
kuundwa ili kuipa Zanzibar uongozi mpya wenye dira ya kututoa katika mkwamo huu
uliopo ambao unapelekea kuendelea kufanya maamuzi yasiyo na misingi ya Katiba
na Sheria za nchi.
HAKI SAWA KWA WOTE
ISMAIL JUSSA
MKURUGENZI WA MAWASILIANO – CUF
MRADI WA KIMATAIFA WA UJENZI WA KISIWA CHA UTALII.
Chombo maalum kinachotumika kwa kazi ya uchimbaji wa mchanga
Baharini Chenye uwezo wa kunyonya na kusafirisha mchanga
kutoka ndani ya Bahari sambamba na kukata Majabali na kufukia katika eneo
linalotengenezwa kisiwa cha Mji Mpya mtoni Marine.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wa Pili
kutoka Kulia akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Baghresa Group
Bwana Said Salim Baghresa wakishuhudia harakati za kunyonya na
kusafirisha mchanga kutoka ndani ya Bahari kwa chombo maalum hapo Mtoni Marine.
Sehemu inayoendelea kufukiwa hapo Mtoni Marine ambayo
itatumika hapo baadaye kwa ajili ya eneo maalum litakalotoa fursa kwa Wananchi
kupata mapumziko { Public Beach }.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Baghresa Group Bwana
Said Salim Baghresa akimueleza Balozi Seif juhudi zinazofanywa na Kampuni yake
za kujenga Kisiwa cha Mji Mpya Mtoni Marine.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi
Zanzibar { ZIPA } Nd. Salum Khamis Nassor akimueleza Balozi Seif
hatua zinazochukuliwa na Taasisi yake katika kuona taratibu za uwekezaji
zinachukuliwa kwa wanaowekeza vitege uchumi vyao Nchini.
Balozi Seif akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya Baghresa Group Bwana Said Salim wakitembelea kuona mradi
wa Ujenzi wa Majengo Mapya ya Hoteli ya Mtoni Marine ambayo iko chini ya
Kampuni hiyo kwa hivi sasa.
Mradi mkubwa wa Kimataifa wa ujenzi wa kisiwa cha Kitalii
ambacho kitatengezezwa kwa mfumo wa ufukiaji Bahari umeanza rasmi katika
eneo la Hoteli ya Utalii iliyopo Mtoni Marine kaskazini Magharibi ya Mji wa
Zanzibar.
Hata hivyo gharama kamili za Mradi huo bado
hazijafahamika wakati utakapokamilika rasmi ujenzi wake hapo
baadaye.
Mradi huo unaoendeshwa na Kampuni ya Kizalendo ya
Baghresa Group utahusisha ujenzi wa Hoteli ya Kimataifa ya Ghorofa Tano
ya Daraja la Tano { Five Star + },
utengenezaji wa eneo la wazi la mapumziko { Public Beach } pamoja na
kutengeneza Kisiwa cha Mji mpya .
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
alishuhudia harakati za ujazaji wa mchanga katika eneo linalofukiwa ambazo
hufanywa kwa utaalamu wa hali ya juu.
Mhandisi wa Mradi huo Bwana Ahmed Shamsi alimueleza Balozi
Seif kwamba chombo maalum kinachotumika kwa kazi ya uchimbaji wa mchanga
Baharini kina uwezo wa kunyonya na kusafirisha mchanga kutoka ndani
ya Bahari sambamba na kukata Majabali.
Mhandisi Shamsi alisema kazi hiyo inafanyika kwa saa 12 kila
siku ambapo takwimu zinaonyesha wazi kwamba uchimbaji huo wa mchanga
unaokwenda zaidi ya mita 15 chini ya Bahari unafikia Tani 600 za
mchanga kwa saa Moja.
Alifahamisha kwamba harakati za uchimbaji na kufukia mchanga
katika eneo hilo zilizoanza Mwezi uliopita wa Novemba zinatarajiwa kukamilika
mwezi Januari mwaka ujao.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Baghresa
Group Bwana Said Salim Baghresa alisema kwamba ujenzi wa mradi huo muhimu
kwa uchumi wa Nchi utasaidia mapato ya Taifa pamoja na kutoa ajira kubwa kwa
vijana Wazalendo hapa Nchini.
Bwana Baghresa alisema mfumo wa ufukiaji Bahari kwa ajili ya
kuanzisha miradi ya Kiuchumi ni mfumo unaotumiwa na Mataifa mbali mbali Duniani
ambapo kwa Afrika mradi kama tayari umeanza kutumiwa katika Kisiwa cha
Seycheles.
Akitoa nasaha zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi ameupongeza Uongozi wa Baghresa Group kwa uamuzi uliochukuwa wa
kuanzisha mradi huo mkubwa wa Kimataifa.
Balozi Seif alieleza kwamba kukamilika kwa mradi huo
mkubwa ambao umeshazoeleka katika Mataifa yaliyoendelea utasaidia
kuitangaza Zanzibar na Tanzania kwa ujumla Kiutalii Kimataifa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuhakikishia Uongozi
huo wa Baghresa Group kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itatoa kila
msaada unaohitajika katika kuona mradi huo unafikia malengo uliojipangia.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamui wa Pili wa Rais wa Zanzibar
WOMEN ACADEMY OF AFRICA (WAFA) YAMPONGEZA MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MJINI MAGHARI MHE: ASHA ABDALLA JUMA.
Balozi Amina Salum Ali akizungumza na wageni mbali mbali waliohudhuria katika hafla ya kumpongeza Mhe. Asha Abdalla Juma kwa kuteuliwa kuwa Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Mjini Magharib.
Mhe. Asha Abdalla Juma wakikumbatiana kwa furaha na Balozi Amina Salum Ali mara baada ya kuzungumza na wageni mbalimbali.
ijana wa Skaunt wakimvalisha shada la mauwa Mhe. Asha Abdalla Juma kwenye sherehe hiyo.
Mhe. Asha Abdalla Juma akizungumza na wageni mbalimbali waliohudhuria katika sherehe ya kumpongeza kwa kuchaguliwa kuwa Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mjini Magharib.
Mhe. Asha Abdalla Juma wakikumbatiana kwa furaha na Balozi Amina Salum Ali mara baada ya kuzungumza na wageni mbalimbali.
ijana wa Skaunt wakimvalisha shada la mauwa Mhe. Asha Abdalla Juma kwenye sherehe hiyo.
Mhe. Asha Abdalla Juma akizungumza na wageni mbalimbali waliohudhuria katika sherehe ya kumpongeza kwa kuchaguliwa kuwa Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mjini Magharib.
baadhi ya waliohudhuria katika sherehe ya kumpongeza mbunge wa viti maalum mkoa wa mjini magharib ASHA ABDALLAH JUMA
Tuesday, December 1, 2015
MASHUJAA WA ZENJ WAREJEA NYUMBANI WAKUTA LIGI KUU INACHEZWA UWANJA WA AMAAN
Na: Abubakar Kisandu, Zanzibar
Mashujaa wa soka wa Zanzibar (Zanzibar Heroes) wamewasili visiwani mchana wa leo, wakitokea Ethiopia kwenye mashindano ya CECAFA Chalenj Cup ambapo Heroes wametolewa kwenye hatua ya makundi wamefungwa 1-0 na burundi, wakafungwa 4-0 na Uganda, kisha wakashinda 3-1 dhidi ya Kenya ambapo walikuwa wapo kundi B.
Mashujaa hao wamewasili visiwani saa 8:15 za mchana kwenye uwanja wa ndege wa Abeid Aman Karume wakitumia ndege ya Ethiopia.
Punde tu baada ya kuwasili hapa visiwani tukafanikiwa kuzungumza na Meneja wa timu hiyo ambae ni Hashim Salum na kuzungumzia hali halisi ya huko Ethiopia ambapo zaidi akisema baridi imewacost ndo mana wakatoka mapema.
“ Kwa kweli hali ya hewa Adis ilikuwa nzito, mana baridi ilikuwa kali sana lakini vijana walipigana na nyinyi mumewaona”.
Kwa upande wake kocha mkuu wa timu hiyo Hemed Suleiman Morocco amesema kuna mambo mengi yaliopelekea kutolewa mapema.
“Tuwe wazi kwenye mpira, tulikuwa hatuna maandalizi mazuri, hatuwezi kucheza na kombain ya Mjini tukaenda kushindana kwenye mashindano yale, wenzetu Rwanda waliweka kambi mwezi mzima Scotland , pia hatuwezi kumuwacha kocha wa makipa pamoja na mtunza vifaa”. Alisema Morroco.
Viongozi waliokwenda huko Mkuu wa Msafara wa timu hiyo alikuwa ni Sharifa Khamis, meneja wa timu Hashim Salum, kocha mkuu Hemed Suleiman Morroco, makocha wasaidizi Malale Hamsini na Hafidh Muhidin lakini mtunza vifaa wa timu (Mdudu) pamoja na kocha wa Makipa Saleh Machupa wote waliachwa jambo ambalo wadau wengi walilalamika.
Kikosi cha wachezaji wa Zanzibar kilichokwenda Ethiopia ambapo kimerejea nyumbani leo hii kiliundwa na wachezaji:-
Makipa: Mwadini Ali (Azam), Mohamed Abraham (JKU).
Mabeki wa pembeni: Mwinyi Haji (Yanga), Nassor Masoud (Stand United), Adaymu Saleh (Coastal Union) na Ismail Khamis (JKU).
Walinzi wa kati: Nadir Harub (Yanga), Shafii Hassan (Zimamoto), Said Mussa (Mafunzo), Issa Haidary (JKU).
Viungo: Awadhi Juma (Simba), Mudathir Yahya (Azam), Saidi Makapu (Yanga), Mohamed Abdulirahmani Mbambi (Mafunzo), Hamis Mcha (Azam), Suleiman Kassim (Stand United) na Omari Juma (Hard Rock).
Washambuliaji: Ibrahimu Hilika (Zimamoto), Mateo Antony (Yanga) na Ame Ali (Azam).
Subscribe to:
Posts (Atom)




















