tangazo

tangazo

Wednesday, December 2, 2015

SIMBA KUANZA MECHI YA KIRAFIKI KESHO NA UPEPO MKALI (KIMBUNGA)


 wachezaji wa timu ya simba wakiwa katika mazoezi yao uwanja wa amani zanzibar.
wachezaji wa timu ya kimbunga wakishangiria ushindi katika moja ya mechi zao.

Na: Abubakar Kisandu, Zanzibar.

Wekundu wa Msimbazi Simba kesho wanatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Kimbunga ambayo inashiriki ligi kuu soka visiwani Zanzibar, mchezo ambao utasukumwa saa10 za jioni kwenye dimba la Amaan.

Katika mchezo huo Simba watautumia kama ni mchezo wa kupata mazoezi na kuwaangalia wachezaji wao wanaotarajia kuwasajili katika dirisha hili dogo la usajili.

Mtandao huu tumefanikiwa kuzungumza na Abdul Mshangama ambae yeye ni mjumbe kamati tendaji wa timu hiyo akiwakilisha hapa Zanzibar na kusema kuwa watacheza michezo mitatu ya kirafiki kabla ya kuwavaa Azam siku ya jumamosi ya tarehe 12 ya mwezi huu kwenye mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara.

“ Kesho sisi Simba tutacheza mchezo wa kirafiki na timu ya Kimbunga, na pia mchezo mwengine tutacheza na kombain ya Unguja siku ya jumamosi, mechi hizi tutazitumia kuwaangalia wachezaji ambao tunatarajia kuwasajili ”. Alisema Mshangama.

Wakati wakijiandaa na msimu mpya Simba walipokuja Zanzibar walishinda michezo yao ya kirafiki yote walipoifunga kombain ya Zanzibar 2-1, pia wakaitwangwa Black Sailors 4-0, na michezo mengine wakaitwanga Polisi 2-0,  wakaifunga Jangombe Boys 3-0, wakaipiga KMKM 3-2, wakatoka sare ya 0-0 na KVZ,  hivyo wanahistoria nzuri kwa michezo ya kirafiki hapa visiwani kwa mwaka huu.

No comments:

Post a Comment