tangazo
Tuesday, December 1, 2015
MASHUJAA WA ZENJ WAREJEA NYUMBANI WAKUTA LIGI KUU INACHEZWA UWANJA WA AMAAN
Na: Abubakar Kisandu, Zanzibar
Mashujaa wa soka wa Zanzibar (Zanzibar Heroes) wamewasili visiwani mchana wa leo, wakitokea Ethiopia kwenye mashindano ya CECAFA Chalenj Cup ambapo Heroes wametolewa kwenye hatua ya makundi wamefungwa 1-0 na burundi, wakafungwa 4-0 na Uganda, kisha wakashinda 3-1 dhidi ya Kenya ambapo walikuwa wapo kundi B.
Mashujaa hao wamewasili visiwani saa 8:15 za mchana kwenye uwanja wa ndege wa Abeid Aman Karume wakitumia ndege ya Ethiopia.
Punde tu baada ya kuwasili hapa visiwani tukafanikiwa kuzungumza na Meneja wa timu hiyo ambae ni Hashim Salum na kuzungumzia hali halisi ya huko Ethiopia ambapo zaidi akisema baridi imewacost ndo mana wakatoka mapema.
“ Kwa kweli hali ya hewa Adis ilikuwa nzito, mana baridi ilikuwa kali sana lakini vijana walipigana na nyinyi mumewaona”.
Kwa upande wake kocha mkuu wa timu hiyo Hemed Suleiman Morocco amesema kuna mambo mengi yaliopelekea kutolewa mapema.
“Tuwe wazi kwenye mpira, tulikuwa hatuna maandalizi mazuri, hatuwezi kucheza na kombain ya Mjini tukaenda kushindana kwenye mashindano yale, wenzetu Rwanda waliweka kambi mwezi mzima Scotland , pia hatuwezi kumuwacha kocha wa makipa pamoja na mtunza vifaa”. Alisema Morroco.
Viongozi waliokwenda huko Mkuu wa Msafara wa timu hiyo alikuwa ni Sharifa Khamis, meneja wa timu Hashim Salum, kocha mkuu Hemed Suleiman Morroco, makocha wasaidizi Malale Hamsini na Hafidh Muhidin lakini mtunza vifaa wa timu (Mdudu) pamoja na kocha wa Makipa Saleh Machupa wote waliachwa jambo ambalo wadau wengi walilalamika.
Kikosi cha wachezaji wa Zanzibar kilichokwenda Ethiopia ambapo kimerejea nyumbani leo hii kiliundwa na wachezaji:-
Makipa: Mwadini Ali (Azam), Mohamed Abraham (JKU).
Mabeki wa pembeni: Mwinyi Haji (Yanga), Nassor Masoud (Stand United), Adaymu Saleh (Coastal Union) na Ismail Khamis (JKU).
Walinzi wa kati: Nadir Harub (Yanga), Shafii Hassan (Zimamoto), Said Mussa (Mafunzo), Issa Haidary (JKU).
Viungo: Awadhi Juma (Simba), Mudathir Yahya (Azam), Saidi Makapu (Yanga), Mohamed Abdulirahmani Mbambi (Mafunzo), Hamis Mcha (Azam), Suleiman Kassim (Stand United) na Omari Juma (Hard Rock).
Washambuliaji: Ibrahimu Hilika (Zimamoto), Mateo Antony (Yanga) na Ame Ali (Azam).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment