tangazo

tangazo

Wednesday, January 22, 2014

VITA DHIDI YA WAISLAM


MADINA

KATIBU MKUU WA JUMUIYA YA USHIRIKIANO WA KIISLAMU (OIC) AMESEMA ONGEZEKO LA WIMBI LA KUUPIGA VITA UISLAMU KATIKA NCHI ZA MAGHARIBI LINATIA WASIWASI MKUBWA.

KATIBU MKUU WA JUMUIYA YA USHIRIKIANO WA KIISLAMU DAKTA IYAD AMIN MADANI AMESEMA KATIKA RISALA ILIYOSOMWA KWA NIABA YAKE KUHUSU WIMBI LA KUUHUJUMU UISLAMU LIMEFIKIA KIWANGO CHA KUTISHA NA WAISLAMU WANAKABILIWA NA HATARI YA UBAGUZI KATIKA JAMII ZA NCHI NYINGI ZA MAGHARIBI.

KATIKA RISALA HIYO ILIYOSOMWA KWENYE MKUTANO WA 8 WA MAWAZIRI WA UTAMADUNI WA NCHI ZA KIISLAMU ULIOANZA JANA MJINI MADINA, SAUDI ARABIA, MADANI ALIWATAKA MAWAZIRI WA UTAMADUNI WA NCHI ZA KIISLAMU KUCHUKUA HATUA MWAFAKA ZA KIUTAMADUNI NDANI NA NJE YA ULIMWENGU WA KIISLAMU KWA LENGO LA KUPAMBANA NA MITAZAMO FINYU INAYOTOA TASWIRA ISIYO SAHIHI KUHUSU UISLAMU.

VILEVILE AMEASHIRIA HATARI ZA KUENDELEA KUKALIWA KWA MABAVU ARDHI ZA PALESTINA NA HUJUMA YA UTAWALA WA ISRAEL DHIDI YA VITUO VYA KIUTAMADUNI NA KIHISTORIA HUKO BAITUL MUQADDAS NI TISHIO KWA WANADAMU WOTE. 

MAADILI


WILAYA YA KATI

WAZAZI NA WALEZI NCHINI WAMESHAURIWA KUWA KARIBU NA WATOTO WAO ILI KUWEZA KUWANUSURU NA MAMBO MAOVU YANAYOJITOKEZA KATIKA JAMII.

WAKIZUNGUMZA NA ADHANA FM REDIO BAADHI YA WANANCHI WA WILAYA YA KATI WAMESEMA KUTOKANA NA KUONGEZEKA KWA HARAKATI ZA KIMAISHA  WAZAZI WENGI WAMEKUWA WAKIKOSA MUDA WAKUFATILIA MIENENDO YA WATOTO WAO NA KUPELEKEA KUSHAMIRI KWA VITENDO VIOVU.

WAMEFAHAMISHA KUWA KUMEKUWA NA WIMBI KUBWA LA WATOTO WANAUJIHUSISHA NA MAKUNDI MAOVU HALI AMBAYO HUPELEKEA KUZIDI KWA MADHARA KATIKA JAMII.

AIDHA WAMESEMA NI BUSARA KWA WALEZI KUKA NA WATOTO WAO ILI KUWAELEZA ATHARI NA MADHARA YA VITENDO VIOVU VINAVYOTENDEKA KATIKA JAMII.

HATA HIVYO WAMETOWA WITO KWA WAZAZI KUWAHIMIZA VIJANA WAO KUPENDA ZAIDI KUISOMA DINI YAO KWA LENGO LA KUFUATA MISIMAMO SAHIHI YA DINI YA KIISLAM.

AJALI


MKOA WA MJINI MAGHARIBI

JUMLA YA AJALI MIA TANO NA THELATHINI NA NNE ZA MAKOSA YA USALAMA WA BARABARANI ZIMERIPOTIWA KUTOKEA KATIKA MWAKA 2013 KWA MKOA WA MJINI MAGHARIBI.

AKIZUNGUMZA NA ADHANA FM REDIO MKUU WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI SHAFII IDDI HASSAN AMESEMA ZAIDI YA WATU ARUBAINI WALIFARIKI DUNIA KUTOKANA NA AJILI ZA BARABARANI HIYO NI KUTOKANA NA UKIUKWAJI WA KANUNI ZA USALAMA BARABARANI.

AIDHA AMEFAHAMISHA KUWA JESHI LA POLISI KUPITIA KITENGO CHA USALAMA BARABARANI WAMEANDAA MIKAKATI MADHUBUTI YA KUENDELEZA UPERESHENI ZA BARABARANI KWA LENGO LA KUPUNGUZA MAKOSA YA USALAMA BARABARANI.

AKIYATAJA MAENEO YALIYOONGOZA KWA AJALI ZA HIZO KATIKA KIPINDI CHA MWAKA JANA NI PAMOJA NA MWANAKWEREKWE,MWANYANYA,KINAZINI NA MAISARA.

SAMBAMBA NA HAYO AMETOA WITO KWA MADEREVA KUFUATA SHERI ZA BARABARANI BILA YA KUSHURUTISHWA ILI WAWEZE KUONDOKANA NA MAKOSA HAYO.

wahamiaji wasiofata utaratibu

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema wahamiaji wasiofata utaratibu watadhibitiwa kuingia Zanzibar iwapo kutakuwa na ufuatiliaji wa kila siku kwa wageni wanaoingia pamoja na kuzingatiwa matumizi ya teknolojia ya kisasa. 
Maalim Seif ameyasema hayo huko ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar, wakati alipokuwa na mazungumzo na Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, ambaye alikwenda kujitambulisha baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.
Makamu wa Kwanza wa Rais amesema suala la ufuatiliaji wageni hasa wale wanaoingia ni muhimu kwa Zanzibar, kwa sababu baadhi ya wageni hujifanya wao ni Watanzania waliotokea Tanzania Bara na kuingia Zanzibar, wakati wao si Watanzania.
Amesema tayari wahamiaji wasiofata utaratibu wengi wamekamatwa na wengine wamekimbia baada ya kusikia wanafuatiliwa baada ya kuishi Zanzibar kwa muda mrefu wakijifanya ni Watanzani, jambo ambalo linaweza kusababisha madhara makubwa kwa nchi na raia wake, ikiwemo kuongeza uhalifu.
“Lazima Idara ya Uhamiaji iwe na utaratibu mzuri wa kufuatilia wageni wote wanaoingia Zanzibar kila siku, msisubiri kufanya operesheni maalum kutafuta wahamiaji haramu”, alihimiza Maalim Seif.
Aidha, aliipongeza Idara ya Uhamiaji Zanzibar kwa kuweza kupiga hatua kubwa katika kuondoa urasimu wa upatikanaji hati za kusafiria uliokuwepo siku za nyuma ambapo sasa muombaji hutumia muda usiozidi wiki mbili kuweza kuipata, jambo ambalo halinadubi kuendelezwa.
Amesema ipo haja kwa Idara hiyo kufungua vituo vidogo katiba baadhi ya maeneo ambayo kumekuwa na uingiaji mkubwa wa wageni, ikiwemo katika mkoa wa Kaskazini Pemba, ili kuepusha uingiaji holela wa wageni wanaojihusisha na vitendo viovu, ikiwemo biashara ya dawa za kulevya.
Maalim Seif amemhimiza Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar kuweka mkazo mkubwa zaidi katika kuwapatia mafunzo watendaji wa Idara hiyo, ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi ulio mkubwa zaidi.
Nae Kamishna Sururu amesema Idara hiyo imejipanga vizuri katika kuhakikisha inafanya kazi zake kwa ufanisi na kwa kuzingatia matumizi ya teknolojia ya kisasa pamoja na kupanua shughuli zake katika maeneo mengi zaidi hapa Zanzibar.
Amesema miongoni mwa mikakati yao, hivi sasa wamo katika hatua za kuandaa utaratibu wa kuwarahisishia wasafiri kukamilisha taratibu za kuingia na kutoka nchini kwa kutumia teknolojia za kisasa ambao utakuwa tayari hivi karibuni.  
Ameahidi kuwa Idara hiyo itafanya kazi kwa mashirikiano makubwa miongoni mwa watendaji wake na wananchi na matarajio yao ni kuwa wataweeza kuleta mafanikio na mabadiliko makubwa katika kipindi kifupi kijacho.

Tuesday, January 21, 2014


ZANZIBAR.

 

Jeshi la Polisi nchini limesema KUWA litaendelea kushirikiana na raia katika jitihada zake za kukabiliana na vitendo vya uhalifu.

 

Kauli hiyo imetolewa na  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu, wakati akizungumza na MakamO wa KWanza wa Rais wa Zanzibar  Maalim Seif Sharif Hamad, ofisini kwake Migombani.

 

IGP Mangu ambaye alikuwa amefuatana na Naibu wake Abrahmani Kaniki pamoja na kamishna wa polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame, amesema suala la kudhibiti uhalifu ndio jukumu la msingi la jeshi la polisi, na kwamba litafanya kila juhudi kuona kuwa vitendo vya uhalifu vinadhibitiwa.

 

 

Ameongeza kuwa jeshi la polisi kamwe halipendi kuona kuwa linakuwa chanzo cha vurugu, bali kuzuia vurugu pale zinapotokea na kurejesha amani pale inapotoweka.

 

Aidha IGP Mangu amesema jeshi hilo litaendelea kushirikiana na serikali katika jitihada zake za kukuza uchumi na kupunguza umaskini, kwa kutunza usalama katika maeneo ya utalii ambao ndio sekta kiongozi kwa uchumi wa Zanzibar.

 

Amefahamisha kuwa suala la amani na usalama ni jambo la msingi katika nchi, na kwamba hali hiyo ndio msingi mkuu wa kuvutia wawekezaji wa sekta mbali mbali hasa utalii.

 

Hivyo amesema wataweka mkazo katika maeneo ya utalii ili kuhakikisha kuwa hakuna vitisho wala madhara yanayopatikana kwa wageni wanaoingia nchini.

 

IGP Mangu amesema ingawa jeshi hilo bado linakabiliwa na upungufu wa vitendea kazi vya kisasa, lakini watatumia rasilimali zilizopo katika kuimarisha utendaji wake.

 

Naye Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema suala la ulinzi wa raia na mali zao linapaswa kupewa kipaumbele cha mwanzo katika utendaji wa jeshi hilo.

 

Amesema amani na usalama ndio chachu ya maendeleo kwa uchumi wa Zanzibar ambayo inategemea zaidi sekta ya utalii.

 

Amempongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi aliyepita IGP mstaafu Said Mwema, kwa wazo lake la kuanzisha polisi jamii ambayo imeliweka karibu zaidi jeshi hilo na wananchi.

 

Amemtaka IGP Mangu kuliendeleza wazo hilo, kwani linasaidia kuondosha khofu kwa raia dhidi ya polisi.

Amesisitiza haja kwa jeshi la polisi kuendeleza mahusiano mema na raia, ili kuwawezesha wananchi kujenga imani na jeshi hilo, hatua ambayo itasaidia utendaji wa jeshi.

 

NAYE  MakamO wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amemTAKA  IGP Mangu ya kulisafisha jeshi hilo dhidi ya vitendo vya rushwa vinavyodaiwa kuliandama jeshi hilo.

 

Amesema katika kulisafisha jeshi hilo dhidi ya vitendo vya rushwa, hakuna budi kwa viongozi kuondosha muhali wakati wanapoamua kuwashughulikia watendaji wanaoendesha vitendo hivyo.

mashirikiano ya smz


ZANZIBAR.

 

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema iko tayari kushirikiana na Serikali ya Italia katika nyanja za elimu na hifadhi ya sehemu za historia kama ilivyo katika sekta nyingine.

Hayo yameelezwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein wakati akizungumza na Balozi wa Italia nchini Bwana Luigi Scotto aliyemtembelea Ikulu MJINI ZABNZIBAR.

Katika mazungumzo hayo Balozi Luigi alimueleza Dk. Shein kuwa nchi yake imeanzisha Mpango wa Ushirikiano Kati ya Italia na Afrika ambao umelenga kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hiyo na nchi za Afrika.

Alibainisha kuwa chini ya mpango huo Zanzibar inaweza kufaidika katika suala la uhifadhi na ukarabati wa sehemu za historia kama vile Mji Mkongwe pamoja na masuala ya ufundishaji wa lugha ya Kitaliano hapa nchini.

Dk. Shein alimueleza Balozi Luigi kuwa ukarabati na uhifadhi wa mji Mkongwe ni suala linalopewa umuhimu mkubwa na Serikali hivyo fursa ya kushirikiana na Serikali ya Italia katika suala hilo imekuja wakati muafaka.

Aliongeza kuwa mpango wa kufundisha ya lugha ya kitaliano nao ni muhimu na unaweza kutekelezwa kupitia Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar-SUZA chini ya Skuli ya Kiswahili na Lugha za Kigeni katika chuo hicho.

Dk. Shein alimhakikishia Balozi Luigi kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kufanyakazi na Serikali ya Italia ili kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya nchi mbili hizo.

NAYE  Balozi Luigi Scotto kwa upande wake alimueleza Dk. Shein kuwa nchi yake inaupa umuhimu mkubwa uhusiano wake na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Zanzibar ikiwemo.

Alifafanua kuwa mbali ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na unaoendelea kufanywa na wananchi wa Italia humu nchini, nchi mbili hizo zina mambo yanayofanana kama vile sehemu nyingi za kihistoria.

Monday, January 20, 2014

UTEUZI WA MAWAZIRI

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amefanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri kwa kuwateua mawaziri na manaibu waziri, kuziba nafasi zilizoachwa na mawaziri wanne waliojiuzulu na mmoja aliyefariki dunia hivi karibuni.
Katika uteuzi huo Rais Kikwete amewateua mawaziri wapya wawili na manaibu waziri wapya wanane, huku akiwapandisha vyeo manaibu waziri wanne kuwa mawaziri kamili.
Miongoni mwa mawaziri wapya ni pamoja na aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dokta Asha-rose Migiro, ambaye ameteuliwa kuwa waziri wa Katiba na Sheria, huku Dk. Titus Kamani akiteuliwa kuwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.
Waziri pekee aliyeachwa katika mabadiliko hayo ni aliyekuwa waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira), Dk. Terezya Huvisa.
Miongoni mwa manaibu waziri wapya ni pamoja na Juma Nkamia ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari na mtangazaji, ambaye amepewa dhamana katika Wizara ya Habari, Vijana na Michezo.
Mabadiliko yaliyofanywa na Rais Kikwete yametokana na kujaza nafasi za mawaziri ambao walilazimika kujiuzulu baada ya ripoti ya bunge kuhusu Operesheni Tokomeza Ujangili kubaini kuwepo vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na mauaji, utesaji na udhalilishaji vikidaiwa kutendwa na watekelezaji wa operesheni hiyo.
Ripoti hiyo iliwalazimisha waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki kutangaza kujiuzulu, huku naye waziri wa mambo ya ndani, Dr. Emmanuel Nchimbi kufuata mkondo huo bila kumwaacha waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa, Shamsi Vuai Nahodha, na Dr.
Mathayo David Mathayo aliyekuwa waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, kutokana na wizara zao kuhusika katika usimamizi wa operesheni hiyo ambayo iliwahusisha polisi, askari jeshi na walizni wa wanyamapori.

Huku nafasi ya tano katika baraza hilo ikiachwa wazi na aliyekuwa waziri wa fedha, Dr. William Mgimwa aliyefariki dunia mapema mwezi huu nchini Afrika Kusini alikokuwa akipata matibabu.