MADINA
KATIBU
MKUU WA JUMUIYA YA USHIRIKIANO WA KIISLAMU (OIC) AMESEMA ONGEZEKO LA WIMBI LA
KUUPIGA VITA UISLAMU KATIKA NCHI ZA MAGHARIBI LINATIA WASIWASI MKUBWA.
KATIBU
MKUU WA JUMUIYA YA USHIRIKIANO WA KIISLAMU DAKTA IYAD AMIN MADANI AMESEMA
KATIKA RISALA ILIYOSOMWA KWA NIABA YAKE KUHUSU WIMBI LA KUUHUJUMU UISLAMU
LIMEFIKIA KIWANGO CHA KUTISHA NA WAISLAMU WANAKABILIWA NA HATARI YA UBAGUZI
KATIKA JAMII ZA NCHI NYINGI ZA MAGHARIBI.
KATIKA
RISALA HIYO ILIYOSOMWA KWENYE MKUTANO WA 8 WA MAWAZIRI WA UTAMADUNI WA NCHI ZA
KIISLAMU ULIOANZA JANA MJINI MADINA, SAUDI ARABIA, MADANI ALIWATAKA MAWAZIRI WA
UTAMADUNI WA NCHI ZA KIISLAMU KUCHUKUA HATUA MWAFAKA ZA KIUTAMADUNI NDANI NA
NJE YA ULIMWENGU WA KIISLAMU KWA LENGO LA KUPAMBANA NA MITAZAMO FINYU INAYOTOA
TASWIRA ISIYO SAHIHI KUHUSU UISLAMU.
VILEVILE
AMEASHIRIA HATARI ZA KUENDELEA KUKALIWA KWA MABAVU ARDHI ZA PALESTINA NA HUJUMA
YA UTAWALA WA ISRAEL DHIDI YA VITUO VYA KIUTAMADUNI NA KIHISTORIA HUKO BAITUL
MUQADDAS NI TISHIO KWA WANADAMU WOTE.
No comments:
Post a Comment