MKOA WA
MJINI MAGHARIBI
JUMLA YA
AJALI MIA TANO NA THELATHINI NA NNE ZA MAKOSA YA USALAMA WA BARABARANI
ZIMERIPOTIWA KUTOKEA KATIKA MWAKA 2013 KWA MKOA WA MJINI MAGHARIBI.
AKIZUNGUMZA
NA ADHANA FM REDIO MKUU WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI SHAFII IDDI HASSAN
AMESEMA ZAIDI YA WATU ARUBAINI WALIFARIKI DUNIA KUTOKANA NA AJILI ZA BARABARANI
HIYO NI KUTOKANA NA UKIUKWAJI WA KANUNI ZA USALAMA BARABARANI.
AIDHA
AMEFAHAMISHA KUWA JESHI LA POLISI KUPITIA KITENGO CHA USALAMA BARABARANI
WAMEANDAA MIKAKATI MADHUBUTI YA KUENDELEZA UPERESHENI ZA BARABARANI KWA LENGO
LA KUPUNGUZA MAKOSA YA USALAMA BARABARANI.
AKIYATAJA
MAENEO YALIYOONGOZA KWA AJALI ZA HIZO KATIKA KIPINDI CHA MWAKA JANA NI PAMOJA
NA MWANAKWEREKWE,MWANYANYA,KINAZINI NA MAISARA.
SAMBAMBA
NA HAYO AMETOA WITO KWA MADEREVA KUFUATA SHERI ZA BARABARANI BILA YA
KUSHURUTISHWA ILI WAWEZE KUONDOKANA NA MAKOSA HAYO.
No comments:
Post a Comment