WILAYA YA KATI
WAZAZI NA WALEZI
NCHINI WAMESHAURIWA KUWA KARIBU NA WATOTO WAO ILI KUWEZA KUWANUSURU NA MAMBO
MAOVU YANAYOJITOKEZA KATIKA JAMII.
WAKIZUNGUMZA NA
ADHANA FM REDIO BAADHI YA WANANCHI WA WILAYA YA KATI WAMESEMA KUTOKANA NA
KUONGEZEKA KWA HARAKATI ZA KIMAISHA WAZAZI WENGI WAMEKUWA WAKIKOSA MUDA
WAKUFATILIA MIENENDO YA WATOTO WAO NA KUPELEKEA KUSHAMIRI KWA VITENDO VIOVU.
WAMEFAHAMISHA
KUWA KUMEKUWA NA WIMBI KUBWA LA WATOTO WANAUJIHUSISHA NA MAKUNDI MAOVU HALI
AMBAYO HUPELEKEA KUZIDI KWA MADHARA KATIKA JAMII.
AIDHA
WAMESEMA NI BUSARA KWA WALEZI KUKA NA WATOTO WAO ILI KUWAELEZA ATHARI NA
MADHARA YA VITENDO VIOVU VINAVYOTENDEKA KATIKA JAMII.
HATA
HIVYO WAMETOWA WITO KWA WAZAZI KUWAHIMIZA VIJANA WAO KUPENDA ZAIDI KUISOMA DINI
YAO KWA LENGO LA KUFUATA MISIMAMO SAHIHI YA DINI YA KIISLAM.
No comments:
Post a Comment