tangazo

tangazo

Friday, April 25, 2014

WIZARA NA IDARA ZA SERIKALI ZAKUMBUSHWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO


ZANZIBAR

RAIS WA ZANZIBAR DK. ALI MOHAMED SHEIN AMEZIKUMBUSHA WIZARA NA IDARA ZA SERIKALI KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE KWA WAKATI NA KURIPOTI KWA MAMLAKA HUSIKA ILI MATOKEO YAWEZE KUTOLEWA KWA WANANCHI. 

AKIHITIMISHA KIKAO CHA KUJADILI UTEKELEZAJI WA MPANGOKAZI WA WIZARA YA MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO KWA KIPINDI CHA JULAI 2013 HADI MACHI 2014 IKULU JANA DK. SHEIN ALISISITIZA UMUHIMU KWA WIZARA NA IDARA ZA SERIKALI KUTUMIA MAMLAKA ZINAZOONGOZA WIZARA NA IDARA ZA SERIKALI KUJADILI MASUALA YAO NA KUYACHUKULIA HATUA.

DK. SHEIN AMELEZA NA KUSISITIZA MASHAURIANO KATI YA WIZARA NA BODI ZINAZOSIMAMIA TAASISI ZA SERIKALI KUWA NI LAZIMA YAFANYIKE MARA KWA MARA NA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA ZILIZO JUU YAKE.

AIDHA DK.SHEIN AMEBAINISHA KUWA WAJIBU WA BODI HIZO NI KUZISAIDIA WIZARA KUSIMAMIA TAASISI ZILIZO CHINI YAKE KWA MUJIBU WA SHERIA NA TARATIBU ZILIZOWEKWA HIVYO MAWASILIANO YA MARA KWA MARA NA WIZARA NI KITU CHA LAZIMA.

AMESEMA NA KUSISITIZA KUWA HUO NDIO UTARATIBU UNAOPASWA KUFUATWA ILI SHUGHULI ZA SERIKALI ZIWEZE KUFANYIKA KWA WAKATI NA KWA UFANISI.

 

KATIKA KIKAO HICHO MHE RAIS AMEZIAGIZA WIZARA ZA SERIKALI KUVIPATIA NYENZO VITENGO VYA UKAGUZI WA NDANI KWA MUJIBU WA MAHITAJI NA UWEZO WA FEDHA ULIOPO ILI VITENGO HIVYO VIWEZE KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE KIKAMILIFU NA KWA UHURU.  

 

AWALI AKIWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI MPANGOKAZI WA WIZARA HIYO KATIBU MKUU DK.  JUMA MALIK AKIL ALIELEZA KUWA KATIKA KIPINDI HUSIKA WIZARA YAKE ILIPANGA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO 14 INAYOJUMUISHA UJENZI WA BARABARA, MIUNDOMBINU YA VIWANJA VYA NDEGE NA BANDARI PAMOJA NA MRADI WA MAGEUZI YA MFUMO WA TAASISI.

 

AMEFAFANUA KUWA MIRADI HIYO IMEZINGATIA UTEKELEZAJI WA MIPANGO MIKUU YA MAENDELEO YA NCHI IKIWEMO DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2020, MKAKATI WA KUKUZA UCHUMI NA KUPUNGUZA UMASIKINI-MKUZA II, SERA YA USAFIRI ZANZIBAR, SERA YA TEHAMA NA MPANGO MKUU WA USAFIRI ZANZIBAR (ZANZIBAR TRANSPORT MASTERPLAN 2009).

 

KWA UPANDE WA UKUSANYAJI MAPATO, DK AKIL ALIELEZA KUWA HADI MWEZI MACHI 2014 WIZARA YAKE IMEWEZA KUKUSANYA JUMLA YA SHILINGI MILIONI 306 IKIWA NI ASILIMIA 75 YA LENGO LA WIZARA HIYO LA KUKUSANYA SHILINGI MILIONI 406 KWA MWAKA WA FEDHA WA 2013/2014.

TASAF KUNUSURU KAYA MASIKINI


ZANZIBAR.

 

Ujumbe kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF nawashirika wa maendeleo wanaofadhili Mpango wa kunusuru Kaya Masikini na zinazoishi katika mazingira hatarishi uko NCHINI KWA LENGO LAKUANGALIA  Mpango huo unavyotekelezwa HAPA ZANZIBAR.

 

Ujumbe huo umepata fursa ya kutembelea shehia ya Kijini Matemwe mkoa wa Kaskazini Unguja na Shehia ya Kikungwi wilaya ya Kati mkoa wa Kusini Unguja ambako umezungumza na walengwa wa  mpango huo.

 

Wakizungumza na viongozi hao baadhi ya walengwa wameELEZEA kuridhika KWAO  na mpango wa kunusuru kaya masikini ambapo wamesema KUWA  maisha ya kaya hizo yameanza kuIMARISHWA huku mmoja wa walimu wa sKULI Za msingi Kikungwi Amrani Kombo akibainisha kuwa tOKEA kuanza kwa Mpango huo  mwaka jana kumekuwa na mahudhurio mazuri kwa wanafunzi kutoka katika kaya masikini ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla ya kuanza kwa mpango huo.

 

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bwana Ladislaus

Mwamanga amesema

KUWA Mpango huo umeanza kutekelezwa kwa awamu nchini baada ya serikali kuridhia utekelezaji wake katika jitihada za kupambana na umasikini miongoni mwa wananchi.

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR KUHAKIKISHA KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO


ZANZIBAR.

 

WIZARA ya Afya Zanzibar, imesema kuwa itahakikisha hatua zilizofikiwa katika kupunguza vifo vya akimama wajawazito na watoto wakati wa kujifungua zinakuwa endelevu ili kufikia malengo ya millennia.

Mkurugenzi Mipango, Sera na Utafiti katika wizara hiyo Abdullatif Haji, amesema katika mkutano wa siku moja kufunga mradi wa miaka mitano uitwao MAISHA uliofanyika katika hoteli ya Grand Palace Zanzibar, kuwa lazima juhudi za kuimarisha afya ya mama na mtoto ziendelezwe.

Mkurugenzi huyo amepongeza hatua iliyofikiwa kwa kupunguza vifo hivyo kutoka 377 mwaka 2012, hadi kufikia 221 kwa sasa.

Amefahamisha kuwa, vifo vya akimama wajawazito na watoto vinaweza kupunguzwa na kumalizwa kabisa, kama kutakuwa na mkakati madhubuti wa utoaji huduma endelevu na uangalizi wa kutosha kabla na baada ya kujifungua.

Mkurugenzi huyo amewashukuru watu wa Marekani na serikali yao na USAID, kwa msaada wao mkubwa na muhimu, kwa kufanya kazi bega kwa bega na Zanzibar katika kuhakikisha vifo  vitokanavyo na uzazi vinapungua kwa kiasi kikubwa Unguja na Pemba.

Alisema lengo la Wizara ya Afya, ni kuhakikisha kuwa vifo vya mama wajawazito vinavyotokana na uzazi na vya watoto wanaokufa wakati wa kuzaliwa, vinapungua hadi 150 ifikapo mwaka 2015.  

Mapema, Mkurugenzi Mkazi wa Jhipiego nchini Tanzania Maryjane Lacoster, ameelezea kuridhishwa kwake  na ushirikiano wanaoupata kutoka serikali zote mbili, ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Mapinduzi Zanzibar.

Naye Mwakilishi wa USAID nchini Tanzania Lisa Patel, ameishukuru Wizara ya Afya Zanzibar, kwa kuupa ushirikiano mradi huo uliorahisisha wanawake kupata huduma bora kutokana na vifaa vya kisasa wakati wa ujauzito, kabla na baada ya kujifungua.

Kwa upande wake, msimaizi mkuu wa mradi wa MAISHA Dk. Dunstan Bishanga, alieleza kuwa, tangu kuanzishwa kwa mradi huo mwaka 2008, zaidi ya watoa huduma 250 Unguja na Pemba,  wamepatiwa mafunzo kuhusiana na jinsi ya kuwahudumia akina mama wajawazito na watoto.

LIPUMBA ASEMA UKAWA WAENDELEA KUPIGANIA UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI


DAR-ES-SALAAM.

 

Mwenyekiti Taifa wa chama cha WANANCHI CUF Prof. Ibrahim Haruna Lipumba, amesema KUWA kundi LA Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) litaendelea kupigania haki ya Watanzania ya kupata katiba wanayoitaka KULINGANA NA maoni yao waliyoyatoa mbele ya Tume ya Marekebisho ya Katiba.

 

Kundi hilo linajumuisha wajumbe wa bunge maalum la katiba wanaopinga MADAI YA ubabe UNAOFANYWA NA BAADHI YA WAJUMBE WA bunge hilo.

 

Akizungumza MJINI DAR-ES-SALAAM Prof. Lipumba amesema KUWA kundi hilo liko tayari kurejea bungeni iwapo CCM itaahidi kuheshimu rasimu ya katiba iliyoandaliwa na Tume YA MABADILIKO YA KATIBA.

 

Kundi hilo liliondoka kATIKA vikao vya bunge maalum la Katiba wiki iliyopita likilalamikia kudharauliwa rasimu ya katiba.

 

Wajumbe hao KUTOKA UKAWA waMEsema KUWA kuna njama ya kupuuza vipengeLe muhimu vya rasimu ya katiba; jambo ambalo wameSISITIZA kulipinga kwa nguvu zote.

Thursday, April 24, 2014

zanzibar kuanzimisha wiki ya chanjo afrika

ZANZIBAR.
WIZARA YA AFYA KUPITIA KITENGO CHA CHANJO IMESEMA KUWA ITAADHIMISHA WIKI YA CHANJO KATIKA BARA LA AFRIKA KUANZIA TAREHE 24 HADI 30 MWEZI HUU SAMBAMBA NA KUTOA HUDUMA HIYO KATIKA VITUO VYA AFYA NA HOSPITALI ZOTE HAPA NCHINI.
AKITOA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA MAZSON SHANGANI MJINI ZANZIBAR AFISA WA AFYA WA KITENGO HICHO NDUGU YUSSUF HAJI MAKAME AMESEMA KUWA LENGO LA MAADHIMISHO HAYO NI KUIELIMISHA JAMII UMUHIMU WA CHANJO NA MADHARA YAKU...KOSA HUDUMA HIYO WATOTO WA CHINI YA MIAKA MIWILI.
AIDHA AMEWATAKA WAZAZI NA WALEZI KUWAKAMILISHIA CHANJO WATOTO WAO ILI KUWALINDA NA MARADHI YA KUAMBUKIZA NA KUWAKOMBOA KIAFYA.
KATIKA WIKI HIYO YA CHANJO INAYOANZA LEO ,VITUO VYOTE VITAKUA WAZI KWA HUDUMA HIYO KUANZIA ASUBUHI HADI SAA KUMI JIONI NA HIVYO NI FURSA KWA WAZAZI KUWAPELEKA WATOTO WAO WENYE UMRI WA KANZIA SIKU MOJA HADI MIAKA MIWILI.
KILA MWAKA WIKI YA MWISHO YA MWEZI WA APRIL KATIKA BARA LA AFRIKA HUADHIMISHWA WIKI HIYO AMBAPO KWA TANZANIA UJUMBE WA WIKI HIYO YA CHANJO UNAELEZA KUWA “JAMII ILIYO CHANJWA NI JAMII YENYE AFYA”. NA KAULI MBIU NI” CHANJO NI JUKUMU LETU SOTE”.
MAPEMA AKIZUNGUMZIA MAANDALIZI YA WIKI YA CHANJO AFISA WA AFYA WA KITENGO HICHO NDUGU ABDULHAMID AMEIR SALEH AMEYATAJA MARADHI YANAYO KINGWA WATOTO KWA CHANJO KUWA NI PAMOJA NA HOMA YA INI,NIMONIA ,SURUA, POLIO, NA KUHARISHA.
MENGINE NI DONDAKOO,KIFADURO,PEPO PUNDA, KIFUA KIKUU NA UTI WA MGONGO.

utoro wa wanafunzi huchangia kushuka kiwango cha elimu


wilaya ya kusini.

 

Walimu Wa Skuli Ya Mtende wilaya ya kusini unguja Wamelalamikiya Tatizo La Utoro Wa Wanafunzi Katika Skuli Hiyo Amblo unachangia Kushuka Kiwango Cha Ufauli Kwa Wanafunzi.

Akizungumza Na Adhana Fm  Mwalimu Mkuu Wa Skuli Hiyo ndugu Faruku Issa Ahmed Amesema kuwa Tatizo La Utoro Limekuwa Likichangiwa Na Vitendo Vya Anasa Vinavyofanya Na Baadhi Ya Wanafunzi Wa Skuli Hiyo.

 

Amefahamisha Kuwa Wanafunzi  Wengi Wamekuwa Wakiutumia Muda Wao K Wa Kuangalia Mambo Yasiyofaa Katika Televisheni Na Kwenda Katika Kumbi Za Disko Siku Za mwisho wa wiki Hali Inayopelekea Kukosa Muda Wa Kufuatilia Masomo Yao.

 

Amefafanuwa Kuwa Licha Ya Walimu Kukemea Vitendo Hivyo Kwa Kuwapa Adhabu Wanafunzi  Bado Vitendo Hivyo Vimekuwa Vikiendelea.

 

Hata Hivyo Amesema kuwa Hali Hiyo Imekuwa Ikiwaathiri Wanafunzi Wengi nakushindwa Kuendelea Na Masomo kutokana  naKujiingiza Katika Matumizi Ya maDawa ya Kulevya  Na Kuengezeka Kwa Mimba Za Umri Mdogo Katika Kijiji Hicho.

 

Kwa Upande Wao Wanafunzi Hao Wamesema kuwa Ushirikiano Mdogo kati  Ya Wazazi Na Walimu Ndio Chanzo Cha Kuengezeka Matatizo Katika Skuli Hiyo.

 

hata hivyo  wanafunzi hao Wameongeza Kuwa Ugumu Wa Maisha umekuwa ukichangia Kushuka kwa kiwango cha Ufaulu Kwa Wanafunzi.

dokta sheni azitaka ofisi za serikali kufanya kazi kwa pamoja


ZANZIBAR.

 

Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein amesisitiza umuhimu wa taasisi za serikali kufanyakazi kwa pamoja katika kupanga na kugawana rasilimali fedha ili kufanikisha utekelezaji wa malengo yaliyowekwa.

 

Dk.  Shein ameeleza hayo alipokuwa akizungumza na uongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo katika kikao cha kutathmini utekelezaji wa mpango kazi na bajeti ya Wizara hiyo katika kipindi cha miezi tisa kuanzia Julai 2013 hadi 2014.

 

Amesema kuwa utaratibu wa kupanga na kutekeleza kwa pamoja kazi za Wizara na kuweko na uwazi katika ugawaji na utumiaji wa rasilimali fedha ndio njia pekee zitakazosaidia kufikia malengo yaliyopangwa na Wizara kwa ufanisi.

 

aidha kiongozi huyo Amebainisha kuwa watendaji wa serikali wanajukumu kubwa la kuhakikisha kuwa fedha za umma zinazopatikana baada ya kukusanywa kutokana na kodi na malipo mengine mbali mbali zinatumiwa ipasavyo ili kuhakikisha kuwa tija inayotokana na matumizi ya fedha hizo inaonekana na inawanufaisha wananchi wote.

Amezitaka taasisi za serikali kuwa na muongozo utakaoweka bayana vipaumbele vyake, na mgawanyo wa fedha kufanywa kwa mujibu wa vipaumbele vitakavyobainishwa katika  muongozo husika.

Akizungumzia suala la kuimarisha Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC), Rais wa Zanzibar ameiagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo kuchukua hatua za dharura kukabiliana na changamoto zinazolikabili Shirika hilo ili liweze kuendesha shughuli zake kwa mafanikio sambamba na kukabiliana ushindani mkubwa wa kibiashara.

Amesema serikali tayari imeshatoa fedha nyingi katika Shirika hilo na kusisitiza kuwa hakuna sababu ya kushindwa kujiendesha kibiashara.

Aidha, Rais wa Zanzibar ameiagiza Wizara hiyo kufikiria namna itakavyoweza kuimarisha Tume ya Utangazaji Zanzibar ili iweze kufanya kazi zake ipasavyo.