ZANZIBAR.
Ujumbe kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF
nawashirika wa maendeleo wanaofadhili Mpango wa kunusuru Kaya Masikini na
zinazoishi katika mazingira hatarishi uko NCHINI KWA LENGO LAKUANGALIA Mpango huo unavyotekelezwa HAPA ZANZIBAR.
Ujumbe huo umepata fursa ya kutembelea shehia
ya Kijini Matemwe mkoa wa Kaskazini Unguja na Shehia ya Kikungwi wilaya ya Kati
mkoa wa Kusini Unguja ambako umezungumza na walengwa wa mpango huo.
Wakizungumza na viongozi hao baadhi ya walengwa
wameELEZEA kuridhika KWAO na mpango wa
kunusuru kaya masikini ambapo wamesema KUWA maisha ya kaya hizo yameanza kuIMARISHWA huku
mmoja wa walimu wa sKULI Za msingi Kikungwi Amrani Kombo akibainisha kuwa tOKEA
kuanza kwa Mpango huo mwaka jana kumekuwa na mahudhurio mazuri kwa
wanafunzi kutoka katika kaya masikini ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla
ya kuanza kwa mpango huo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bwana
Ladislaus
Mwamanga amesema
KUWA Mpango huo umeanza kutekelezwa kwa awamu
nchini baada ya serikali kuridhia utekelezaji wake katika jitihada za kupambana
na umasikini miongoni mwa wananchi.
No comments:
Post a Comment