DAR-ES-SALAAM.
Mwenyekiti Taifa wa chama cha WANANCHI CUF Prof. Ibrahim
Haruna Lipumba, amesema KUWA kundi LA Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA)
litaendelea kupigania haki ya Watanzania ya kupata katiba wanayoitaka KULINGANA
NA maoni yao waliyoyatoa mbele ya Tume ya Marekebisho ya Katiba.
Kundi hilo linajumuisha wajumbe wa bunge maalum la katiba
wanaopinga MADAI YA ubabe UNAOFANYWA NA BAADHI YA WAJUMBE WA bunge hilo.
Akizungumza
MJINI DAR-ES-SALAAM Prof. Lipumba amesema KUWA kundi hilo liko tayari kurejea
bungeni iwapo CCM itaahidi kuheshimu rasimu ya katiba iliyoandaliwa na Tume YA
MABADILIKO YA KATIBA.
Kundi hilo
liliondoka kATIKA vikao vya bunge maalum la Katiba wiki iliyopita likilalamikia
kudharauliwa rasimu ya katiba.
Wajumbe hao
KUTOKA UKAWA waMEsema KUWA kuna njama ya kupuuza vipengeLe muhimu vya rasimu ya
katiba; jambo ambalo wameSISITIZA kulipinga kwa nguvu zote.
No comments:
Post a Comment