wilaya ya kusini.
Walimu Wa Skuli Ya Mtende wilaya ya kusini unguja Wamelalamikiya
Tatizo La Utoro Wa Wanafunzi Katika Skuli Hiyo Amblo unachangia Kushuka Kiwango
Cha Ufauli Kwa Wanafunzi.
Akizungumza Na Adhana Fm Mwalimu Mkuu Wa Skuli Hiyo ndugu Faruku Issa
Ahmed Amesema kuwa Tatizo La Utoro Limekuwa Likichangiwa Na Vitendo Vya Anasa
Vinavyofanya Na Baadhi Ya Wanafunzi Wa Skuli Hiyo.
Amefahamisha Kuwa Wanafunzi Wengi Wamekuwa Wakiutumia Muda Wao K Wa
Kuangalia Mambo Yasiyofaa Katika Televisheni Na Kwenda Katika Kumbi Za Disko
Siku Za mwisho wa wiki Hali Inayopelekea Kukosa Muda Wa Kufuatilia Masomo Yao.
Amefafanuwa Kuwa Licha Ya Walimu Kukemea Vitendo Hivyo Kwa
Kuwapa Adhabu Wanafunzi Bado Vitendo
Hivyo Vimekuwa Vikiendelea.
Hata Hivyo Amesema kuwa Hali Hiyo Imekuwa Ikiwaathiri Wanafunzi
Wengi nakushindwa Kuendelea Na Masomo kutokana naKujiingiza Katika Matumizi Ya maDawa ya
Kulevya Na Kuengezeka Kwa Mimba Za Umri
Mdogo Katika Kijiji Hicho.
Kwa Upande Wao Wanafunzi Hao Wamesema kuwa Ushirikiano
Mdogo kati Ya Wazazi Na Walimu Ndio
Chanzo Cha Kuengezeka Matatizo Katika Skuli Hiyo.
hata hivyo
wanafunzi hao Wameongeza Kuwa Ugumu Wa Maisha umekuwa ukichangia Kushuka
kwa kiwango cha Ufaulu Kwa Wanafunzi.
No comments:
Post a Comment