tangazo

tangazo

Thursday, April 24, 2014

zanzibar kuanzimisha wiki ya chanjo afrika

ZANZIBAR.
WIZARA YA AFYA KUPITIA KITENGO CHA CHANJO IMESEMA KUWA ITAADHIMISHA WIKI YA CHANJO KATIKA BARA LA AFRIKA KUANZIA TAREHE 24 HADI 30 MWEZI HUU SAMBAMBA NA KUTOA HUDUMA HIYO KATIKA VITUO VYA AFYA NA HOSPITALI ZOTE HAPA NCHINI.
AKITOA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA MAZSON SHANGANI MJINI ZANZIBAR AFISA WA AFYA WA KITENGO HICHO NDUGU YUSSUF HAJI MAKAME AMESEMA KUWA LENGO LA MAADHIMISHO HAYO NI KUIELIMISHA JAMII UMUHIMU WA CHANJO NA MADHARA YAKU...KOSA HUDUMA HIYO WATOTO WA CHINI YA MIAKA MIWILI.
AIDHA AMEWATAKA WAZAZI NA WALEZI KUWAKAMILISHIA CHANJO WATOTO WAO ILI KUWALINDA NA MARADHI YA KUAMBUKIZA NA KUWAKOMBOA KIAFYA.
KATIKA WIKI HIYO YA CHANJO INAYOANZA LEO ,VITUO VYOTE VITAKUA WAZI KWA HUDUMA HIYO KUANZIA ASUBUHI HADI SAA KUMI JIONI NA HIVYO NI FURSA KWA WAZAZI KUWAPELEKA WATOTO WAO WENYE UMRI WA KANZIA SIKU MOJA HADI MIAKA MIWILI.
KILA MWAKA WIKI YA MWISHO YA MWEZI WA APRIL KATIKA BARA LA AFRIKA HUADHIMISHWA WIKI HIYO AMBAPO KWA TANZANIA UJUMBE WA WIKI HIYO YA CHANJO UNAELEZA KUWA “JAMII ILIYO CHANJWA NI JAMII YENYE AFYA”. NA KAULI MBIU NI” CHANJO NI JUKUMU LETU SOTE”.
MAPEMA AKIZUNGUMZIA MAANDALIZI YA WIKI YA CHANJO AFISA WA AFYA WA KITENGO HICHO NDUGU ABDULHAMID AMEIR SALEH AMEYATAJA MARADHI YANAYO KINGWA WATOTO KWA CHANJO KUWA NI PAMOJA NA HOMA YA INI,NIMONIA ,SURUA, POLIO, NA KUHARISHA.
MENGINE NI DONDAKOO,KIFADURO,PEPO PUNDA, KIFUA KIKUU NA UTI WA MGONGO.

No comments:

Post a Comment