tangazo

tangazo

Wednesday, April 9, 2014

ccm wakanusha kutaka kuchakachua rasimu ya pili ya katiba


ZANZIBAR.

 

CHAMA CHA MAPINDUZI KIMEKANUSHA VIKALI KUWA KINA LENGO KUCHAKACHUA RASIMU YAPILI YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

 

AKIZUNGUMZA NA WATENDAJI WA MIKOA NA MAKATIBU WA WILAYA WA CCM  LEO HUKO KATIKA OFISI KUU YA CCM KISIWANDUI MJINI ZANZIBAR NAIBU KATIBU MKUU WA CCM ZANZIBAR NDUGU VUAI ALI VUAI  AMESEMA KUWA TAARIFA ZILIZOTOLEWA NA VYOMBO VYA KHABARI KUHUSU SUALA HILO HAZINA UKWELI WOWOTE.

 

AMEVITAKA VYOMBO VYA KHABARI KUACHA TABIA YAKUTOA TAARIFA ZISIZO NA UKWELI  NA KUIPOTOSHA JAMII KUWA CCM INA MPANGO WAKUZIPINGA KANUNI ZA BUNGE AMBAZO ZIMEWEKWA KWA LENGO LAKUENDESHA VIKAO VYA BUNGE MAALUM LA KATIBA.

 

AIDHA VUAI AMESEMA KUWA CHAMA CHA MAPINDUZI NI SEHEMU YA WANANCHI HIVYO  MAPENDEKEZO WATAKAYOYATOA BUNGENI YATATOKANA NA MSIMAMO WA CHAMA HICHO.

 

AMEVITAKA VYAMA VYA UPINZANI  KUFAHAMU KUWA BUNGE MAALUM LA KATIBA LIPO KWA MASLAHI YA WATANZANIA WOTE NA SI WAZANZIBARI PEKEE.

mchango wa kikwete barani afrika waonekana


dar-es-salaam.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, dr Jakaya Mrisho Kikwete amechaguliwa kuwa Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa katika Maendeleo Barani Afrika kwa mwaka 2013 .

 

kwa mujibu wa taaarifa iliyotolewa na kurugenzi ya mawasiliano ikulu mjini dar-es-salaam Heshima hiyo kwa Rais Kikwete imetolewa na jarida maarufu la kimataifa la African Leadership Magazine Group na Tuzo ya heshima hiyo itatolewa leo jioni  katika sherehe iliyopangwa kufanyika  katika Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C ikiwa ni pamoja na chakula cha jioni.

 

Tuzo hiyo itapokelewa kwa niaba ya Rais Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, ambaye tayari amewasili mjini Washington kwa sherehe hiyo kubwa.

 

Tuzo hiyo ya heshima kubwa hutolewa kwa viongozi wa Afrika ambao hutoa mchango mkubwa zaidi wa kiuchumi na kijamii kila mwaka kwa watu wao na imetolewa kwa Rais Kikwete kwa mwelekeo wake usiokuwa wa kawaida na wenye mafanikio makubwa katika  masuala ya utawala bora.

 

Jarida hilo limesema kuwa ukweli wa hali hiyo bora ya utawala bora chini ya  uongozi wa Rais Kikwete umeendelea kumiminiwa sifa kimataifa na leo umeifanya Tanzania kuwa nchi ya kuigwa mfano kama kituo cha uhakika cha uwezeshaji kutokana na mageuzi makubwa yaliyofanywa katika sera na mifumo ya uchumi.

 

Jarida hilo linasema kuwa Rais Kikwete alikuwa chaguo kubwa na la kwanza la wasomaji wa Jarida hilo ambao walipiga kura kupitia njia mbali mbali za mawasiliano za jarida hilo.

mitambo ya redio ya kiislam zanzibar yaungua


ZANZIBAR.

studio  namba tatu ya kituo cha radio ya kiislam ya al-noor fm kilichopo katika maeneo ya masjid swahaba mtoni kidatu zanzibar imeungua moto usiku wakuamkia leo baada yakutokea khitilafu za umeme.

akizungumza na radio adhana fm mkurugenzi wa radio hiyo al-ustadh muhammed suleiman  amesema kuwa mtangazaji wa zamu aliyekuwepo studioni hapo jana usiku abuubakar fakih hamad amekatika mguu wakulia na kuumia mkono baada yakujirusha kutoka ghorofa ya kwanza ya jengo la kituo hicho wakati wakujaribu kujinusuru na moto huo.

ameongeza kuwa mtangazaji huyo akupata athari yoyote yakuungua moto huo na hivi sasa anaendelea na matibabu katika hospitali kuu ya mnazi mmoja mjini zanzibar.

akivitaja vifaa vilivyovyongua baada yakutokea moto huo ustadh muhammed amesema kuwa ni pamoja na mtambo wa stl  ambao unatumika  kwaajili yakusafirishia matangazo kutoka katika studio hiyo hadi katika eneo lakurushia matangazo la masingini wilaya ya magharibi unguja,mixer kubwa aina ya yamaha na fanicha kadhaa zilizokuwemo ndani.

ustadh muhammed amesema kuwa katika kuonyesha utukufu wa kitabu kitukufu cha qur-an kilichonusurika katika chumba kilichongua ni misahafu iliyokuwemo  pekee.

aidha mkurugenzi huyo amefafanua kuwa hadi sasa hasara iliyopatikana kutokana na moto huo haijafahamika.

amesema kuwa juhudi zakurejesha matangazo hayo zinaendelea  hivyo amewaomba waskilizaji kuwa wastahamilivu katika kipindi hiki kifupi ambacho matangazo ya radio hiyo hayatokuwa hewani .

kituo cha radio al-noor fm kinatangaza kupitia mhz 93.03  unguja na 92.06 pemba kimekuwa kikiungua mara kadhaa kutokana na khitilafu za umeme.

 

Friday, April 4, 2014

SERIKALI YA SMZ YA AHIDI KUTORUDI NYUMA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO LICHA YA CHANGAMOTO MBALI MBALI


ZANZIBAR

 

SERIKALI IMESEMA HAITARUDI NYUMA KUTEKELEZA AZMA YAKE YA KULIENDELEZA ENEO LA MICHENZANI MJINI UNGUJA HIVYO AMELITAKA SHIRIKA LA HIFADHI YA JAMII ZANZIBAR-ZSSF AMBALO NDILO LINALOTEKELEZA MRADI HUO KUHAKIKISHA KUWA LINAKABILIANA NA CHANGAMOTO ZOTE ZINAZOTOJITOKEZA KATIKA UTEKELEZAJI WAKE.

RAIS WA ZANZIBAR A,BAYE PIA NI MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN AMESEMA HAYO WAKATI ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA VIONGOZI NA WATENDAJI WA SHIRIKA HILO PAMOJA NA VIONGOZI WA SERIKALI WAKATI ALIPOFANYA ZIARA KUKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA MNARA WA KUMBUKUMBU YA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR.

KATIKA MAELEZO YAKE KWA MHE RAIS MKURUGENZI MKUU WA ZSSF BWANA ABDULWAKIL HAJI HAFIDH ALIELEZA KUWA MRADI HUO WA KULIENDELEZA ENEO LA MICHENZANI UNAKABILIWA NA TATIZO LA UMILIKI WA BAADHI YA MAENEO LIKIWEMO LA MAKONTENA HIVYO AKAIOMBA SERIKALI KUSAIDIA KUYATATUA.

ALIUTAKA UONGOZI WA ZSSF KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAFANYA BIASHARA WALIOPO KATIKA ENEO LA MAKONTENA JUU YA NAMNA YA KUPISHA UJENZI KATIKA ENEO HILO NA KUELEZA KUWA ANAAMINI KWAMBA WATAAFIKI KWANI NAO WANGEPENDA KUFANYA SHUGHULI ZAO KATIKA MAENEO MAZURI YENYE KUVUTIA.

ALIWAELEZA VIONGOZI WALIOKUWEPO KATIKA ENEO HILO KUWA AMEAMUA KUTEMBELEA MRADI HUO ILI KUJIONEA MWENYEWE MAENDELEO YA UTEKELEZAJI WAKE KWA KUWA AMEKUWA AKISIKIA NAMNA UJENZI HUO UNAVYOENDELEA KUTOKA KWA WATU MBALIMBALI.

AWALI MKURUGENZI MKUU WA ZSSF BWANA ABDULWAKIL HAJI HAFIDH ALIMUELEZA MHE RAIS KUWA UJENZI WA MNARA HUO WENYE MITA 33 UNAENDELEA VIZURI NA UMESHAFIKIA MITA 21.

ALIELEZA KUWA CHANGAMOTO KUBWA KATIKA KUTEKELEZA MRADI WA KULIBORESHA ENEO LA MICHENZANI KWA KUJENGA MAJENGO YA BIASHARA NA MAKAAZI NI NAMNA YA KUWAHAMISHA KWA MUDA WAFANYABIASHARA WA MAKONTENA PAMOJA NA UTATA WA UMILIKI WA BAADHI YA MAENEO HAYO KUTOTAMBULIWA NA SERIKALI WAKATI WATU WANAYAMILIKI.

WAKATI HUO HUO RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN AMEITAKA ZSSF KUZINGATIA KWA MAKINI UENDESHAJI WA MRADI WA KIWANJA CHA KUFURAHISHIA WATOTO ILI KUHAKIKISHA KUWA KIWANJA HICHO KINAENDESHWA KIBIASHARA NA KIWEZE KUREJESHA FEDHA ZILIZOWEKEZWA.

AKIZUNGUMZA MARA BAADA YA KUTEMBELEA ENEO LA KARIAKOO LINALOJENGWA KIWANJA HICHO DK SHEIN AMELITAKA SHIRIKA HILO KUZINGATIA PIA MASUALA YA USALAMA WA WATU WATAKAOTUMIA KIWANJA HICHO HASA MILANGO YA KUINGILIA NA KUTOKEA.

AKITOA MAELEZO YAKE KWA MHE RAIS, MKURUGENZI MKUU WA ZSSF BWANA ABDULWAKIL HAJI HAFIDH ALIELEZA KUWA UTEKELEZAJI WA MRADI HUO UMESHAVUKA ASILIMIA 50 NA KINATARAJIWA KUKAMILIKA NA KUANZA KUTUMIKA IFIKAPO MWEZI JULAI MWAKA HUU.

HATA HIVYO ALIFAFANUA KUWA SUALA LA KUCHELEWA KUWASILI VIFAA VYA UJENZI NDIO LIMESABABISHA MRADI KUTOKWENDA KWA KASI ILIYOKUSUDIWA LAKINI ALIELEZA KUWA VIFAA HIVYO VINATARAJIWA KUWASILI NCHINI HIVI KARIBUNI.

ALIFAFANUA KUWA KIWANJA HICHO KITAKUWA NA PEMBEA 12 PAMOJA NA HUDUMA NYINGINE KAMA MADUKA 61, SEHEMU ZA KUFANYIA MAONESHO PAMOJA NA HARUSI ,VYOO 30 PAMOJA NA SEHEMU KUBWA YA KUEGESHA MAGARI.

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI ALITEMBELEA PIA SKULI YA SEKONDARI YA LUMUMBA ILIYOPO MJINI UNGUJA AMBAKO ALIKAGUA MAZINGIRA YA SKULI HIYO KONGWE HUMU NCHINI.

Tuesday, April 1, 2014

DOKTA SHEIN AKUTANA NA WAZIRI CHIKAWE


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe ofisini kwake Ikulu.

 

Waziri Chikawe ambaye alifuatana na Naibu wake Bwana Pereira Ame Silima alifika Ikulu kujitambulisha rasmi kufuatia mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete mwezi Januari mwaka huu.

 

Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alimpongeza Waziri Chikawe na Naibu Waziri Silima kwa kukubali uteuzi wa kushika uongozi wa Wizara hiyo yenye majukumu mazito na muhimu ya ulinzi na usalama wa raia na mali zao.

 

Alimueleza waziri huyo kuwa Taasisi za Wizara yake Zanzibar zinafanya vizuri na kuzipongeza taasisi hizo kwa ushirikiano wake na utekelezaji mzuri wa majukumu yao.

 

Hata hivyo alieleza kuwa pamoja na taasisi hizo, ikiwemo Jeshi la Polisi kukabiliwa na changamoto kadhaa lakini watendaji wake wamekuwa wakionesha ujasiri na kuliletea sifa jeshi hilo.

 

Alitoa pongezi maalum kwa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa-NIDA kwa kazi nzuri ambayo imekuwa ikiifanya tangu zoezi la uandikishaji wa vitambulisho hivyo ilipoanza hapa Zanzibar.

 

Dk. Shein aliukumbusha uongozi wa Wizara hiyo ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakiwemo Waziri na Naibu Waziri kuweka utaratibu maalum wa kutembelea taasisi zake zilizoko Unguja na Pemba mara kwa mara ili kuangalia utendaji na mazingira ya utendaji kazi ya taasisi hizo.

 

Katika mazungumzo hayo ambayo yalihudhuriwa pia na Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Bwana Dickson Maimu na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Zanzibar Bwana Vuai Mussa Suleiman, Dk. Shein aliitaka Wizara hiyo pamoja na mafanikio iliyoyapata kuongeza juhudi na kuongeza ufanisi katika kutekeleza majukumu yake.

 

Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mathias Chikawe katika mazungumzo hayo alimwambia Mhe Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kuwa Wizara yake imejidhatiti katika kuimarisha utendaji kazi wa wizara na taasisi zake kwa kubuni mbinu na mikakati ambayo inaendana na mazingira ya sasa.

 

Aliongeza kuwa wizara  na taasisi zake zinatekeleza majukumu yake na ulinzi wa raia na mali zao na kuwa jitihada zinafanywa kuzipatia nyenzo taasisi zinazohusika ili kuongeza ufanisi katika kazi.   

Thursday, March 27, 2014

UINGEREZA WAFANYA MABADILIKO YA UOMBAJI VIZA KWA WATANZANIA


DAR-ES-SALAAM.

 

Ubalozi wa Uingereza nchini umesema KUWA unakusudia kufanya mabadiliko ya utaratibu wa maombi na utoaji viza kwa Watanzania wanaotaka kwenda nchini Uingereza kwa kufungua ofisi zitakazotoa huduma hiyo Mjini Dar es Salaam.

 

Mkurugenzi wa masuala ya viza ya Uingereza kwa nchi za Afrika  Kashif Chaudry, amesema  AMEYASEMA HAYO MJINI Dar es Salaam ambapo ameONGEZA KUWA  wanakusudia kuanza kulipia huduma hiyo kwa njia ya simu za mkononi.


Chaudry amesema kupitia utaratibu huo mpya, maombi yote ya viza sasa yatakuwa yaKIfanyika nje ya jengo la ubalozi na kutaja eneo moja Mjini Dar es Salaam kuwa ndiKo ambako watu wanaweza kuomba na kupata viza za kuingia nchini Uingereza.


Amelitaja eneo hILO kuwa ni katika jengo la Viva Towers lililopo katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi Mjini Dar es Salaam na kwamba hatua hiyo inalenga kupunguza usumbufu kwa watu wanaoomba kibali cha kuingia Uingereza.

MAALIM SEIF ARIDHISHWA KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI


ZANZIBAR.

 

MakamO wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, ameelezea kuridhishwa kwake na hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa miradi mitatu inayoendelea KATIKA uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.

 

Miradi hiyo inahusisha ukarabati na ujenzi wa njia za kupitia ndege wakati wa kuruka pamoja na sehemu ya maegesho ya ndege, ujenzi wa uzio wa eneo la uwanja wa ndege, pamoja na ujenzi wa jEngo jipya la abiria (Terminal 2).

 

Akizungumza katika ziara ya kutembelea miradi hiyo huko uwanja wa ndege wa Zanzibar, Maalim Seif amesema KUWA hatua iliyofikiwa inatia moyo, na kuwataka wakandarasi na wasimamizi wa miradi hiyo  kuhakikisha kuwa inakamilika kwa wakati.

 

Amesema KUWA Serikali kwa upande wake itaweka mkakati wa makusudi ili iweze kumaliza kuwalipa fidia wananchi ambao bado hawajalipwa, na kuruhusu ujenzi wa uzio uweze kukamilika kwa Wakati.

 

Mapema meneja wa mradi wa ujenzi wa uzio huo Bw. Frederick Nkya, alimueleza MakamO wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kwamba hadi sasa tayari asilimia 73 ya ujenzi huo imeshakamilika.

 

Hata hivyo amesema changamoto kubwa inayowakabili ni eneo la mita elfu tatu na mia moja ambapo sehemu kubwa ya eneo hilo bado wananchi hawajalipwa fidia.

 

Amefahamisha kuwa hadi sasa eneo la mita elfu mbili na mia saba ndilo ambalo halijafanyiwa tathmini kuweza kuwalipa wananchi walioko katika maeneo ya mradi huo.

 

Miradi ya ukarabati na ujenzi wa njia za kupitia ndege wakati wa kuruka (Taxiway) pamoja na sehemu ya maegesho ya ndege (Apron) katika uwanja huo inafadhiliwa na Benki ya Dunia pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ambapo mradi wa ujenzi wa uzio wenye urefu wa mita 11,690  katika uwanja huo, unatekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pekee, ambapo zaidi ya shilingi bilioni sita zitatumika hadi kukamilika kwa mradi huo.

 

AKIZUNGUMZIA mradi wa ujenzi wa jengo jipya la abiria meneja wa mradi huo NDUGU Ibrahim Zhang amesema KUWA ,kazi hiyo sasa inaendelea vizuri.

 

Mradi wa ujenzi wa jEngo jipya la abiria awali ulitiwa saini mwezi wa Septemba 2009 KATI ya Wizara ya Miundo mbinu na Mawasiliano na Kampuni ya ujenzi ya Beijing Construction Engineering Group ya China, lakini baadae serikali iligundua kuwa ukubwa wa jengo uliopendekezwa mwanzo haukidhi haja.

 

HATA HIVYO KUFUATIA KASORO HIYO Serikali ilikubaliana na mkandarasi kuongezwa ukubwa wa jengo kutoka mita 15,600 hadi mita 17,800 kwa ongezeko la fedha dola za kimarekani milioni 11 nukta 8, na kufanya gharama za mradi huo kufikia dola la kimarekani milioni 82 nukta 2.