ZANZIBAR.
CHAMA CHA MAPINDUZI
KIMEKANUSHA VIKALI KUWA KINA LENGO KUCHAKACHUA RASIMU YAPILI YA KATIBA YA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
AKIZUNGUMZA NA
WATENDAJI WA MIKOA NA MAKATIBU WA WILAYA WA CCM LEO HUKO KATIKA OFISI KUU YA CCM KISIWANDUI
MJINI ZANZIBAR NAIBU KATIBU MKUU WA CCM ZANZIBAR NDUGU VUAI ALI VUAI AMESEMA KUWA TAARIFA ZILIZOTOLEWA NA VYOMBO
VYA KHABARI KUHUSU SUALA HILO HAZINA UKWELI WOWOTE.
AMEVITAKA VYOMBO VYA
KHABARI KUACHA TABIA YAKUTOA TAARIFA ZISIZO NA UKWELI NA KUIPOTOSHA JAMII KUWA CCM INA MPANGO
WAKUZIPINGA KANUNI ZA BUNGE AMBAZO ZIMEWEKWA KWA LENGO LAKUENDESHA VIKAO VYA
BUNGE MAALUM LA KATIBA.
AIDHA VUAI AMESEMA
KUWA CHAMA CHA MAPINDUZI NI SEHEMU YA WANANCHI HIVYO MAPENDEKEZO WATAKAYOYATOA BUNGENI YATATOKANA
NA MSIMAMO WA CHAMA HICHO.
AMEVITAKA VYAMA VYA
UPINZANI KUFAHAMU KUWA BUNGE MAALUM LA
KATIBA LIPO KWA MASLAHI YA WATANZANIA WOTE NA SI WAZANZIBARI PEKEE.
No comments:
Post a Comment