dar-es-salaam.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, dr Jakaya Mrisho Kikwete amechaguliwa kuwa Kiongozi
Mwenye Mchango Mkubwa katika Maendeleo Barani Afrika kwa mwaka 2013 .
kwa mujibu wa
taaarifa iliyotolewa na kurugenzi ya mawasiliano ikulu mjini dar-es-salaam Heshima
hiyo kwa Rais Kikwete imetolewa na jarida maarufu la kimataifa la African Leadership
Magazine Group na Tuzo ya heshima hiyo itatolewa leo jioni katika sherehe iliyopangwa kufanyika katika Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C ikiwa ni pamoja na chakula cha jioni.
Tuzo hiyo itapokelewa kwa niaba ya Rais Kikwete na
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, ambaye
tayari amewasili mjini Washington kwa sherehe hiyo kubwa.
Tuzo hiyo ya heshima kubwa hutolewa kwa viongozi wa
Afrika ambao hutoa mchango mkubwa zaidi wa kiuchumi na kijamii kila mwaka kwa
watu wao na imetolewa kwa Rais Kikwete kwa mwelekeo wake usiokuwa wa kawaida na
wenye mafanikio makubwa katika masuala
ya utawala bora.
Jarida hilo limesema kuwa ukweli wa hali hiyo bora ya
utawala bora chini ya uongozi wa Rais Kikwete umeendelea kumiminiwa sifa
kimataifa na leo umeifanya Tanzania kuwa nchi ya kuigwa mfano kama kituo cha
uhakika cha uwezeshaji kutokana na mageuzi makubwa yaliyofanywa katika sera na
mifumo ya uchumi.
No comments:
Post a Comment