tangazo

tangazo

Wednesday, April 9, 2014

mitambo ya redio ya kiislam zanzibar yaungua


ZANZIBAR.

studio  namba tatu ya kituo cha radio ya kiislam ya al-noor fm kilichopo katika maeneo ya masjid swahaba mtoni kidatu zanzibar imeungua moto usiku wakuamkia leo baada yakutokea khitilafu za umeme.

akizungumza na radio adhana fm mkurugenzi wa radio hiyo al-ustadh muhammed suleiman  amesema kuwa mtangazaji wa zamu aliyekuwepo studioni hapo jana usiku abuubakar fakih hamad amekatika mguu wakulia na kuumia mkono baada yakujirusha kutoka ghorofa ya kwanza ya jengo la kituo hicho wakati wakujaribu kujinusuru na moto huo.

ameongeza kuwa mtangazaji huyo akupata athari yoyote yakuungua moto huo na hivi sasa anaendelea na matibabu katika hospitali kuu ya mnazi mmoja mjini zanzibar.

akivitaja vifaa vilivyovyongua baada yakutokea moto huo ustadh muhammed amesema kuwa ni pamoja na mtambo wa stl  ambao unatumika  kwaajili yakusafirishia matangazo kutoka katika studio hiyo hadi katika eneo lakurushia matangazo la masingini wilaya ya magharibi unguja,mixer kubwa aina ya yamaha na fanicha kadhaa zilizokuwemo ndani.

ustadh muhammed amesema kuwa katika kuonyesha utukufu wa kitabu kitukufu cha qur-an kilichonusurika katika chumba kilichongua ni misahafu iliyokuwemo  pekee.

aidha mkurugenzi huyo amefafanua kuwa hadi sasa hasara iliyopatikana kutokana na moto huo haijafahamika.

amesema kuwa juhudi zakurejesha matangazo hayo zinaendelea  hivyo amewaomba waskilizaji kuwa wastahamilivu katika kipindi hiki kifupi ambacho matangazo ya radio hiyo hayatokuwa hewani .

kituo cha radio al-noor fm kinatangaza kupitia mhz 93.03  unguja na 92.06 pemba kimekuwa kikiungua mara kadhaa kutokana na khitilafu za umeme.

 

No comments:

Post a Comment