ZANZIBAR.
MakamO wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim
Seif Sharif Hamad, ameelezea kuridhishwa kwake na hatua iliyofikiwa katika
ujenzi wa miradi mitatu inayoendelea KATIKA uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Abeid Amani Karume.
Miradi hiyo inahusisha ukarabati na ujenzi wa
njia za kupitia ndege wakati wa kuruka pamoja na sehemu ya maegesho ya ndege,
ujenzi wa uzio wa eneo la uwanja wa ndege, pamoja na ujenzi wa jEngo jipya la
abiria (Terminal 2).
Akizungumza katika ziara ya kutembelea miradi
hiyo huko uwanja wa ndege wa Zanzibar, Maalim Seif amesema KUWA hatua
iliyofikiwa inatia moyo, na kuwataka wakandarasi na wasimamizi wa miradi hiyo
kuhakikisha kuwa inakamilika kwa wakati.
Amesema KUWA Serikali kwa upande wake itaweka
mkakati wa makusudi ili iweze kumaliza kuwalipa fidia wananchi ambao bado
hawajalipwa, na kuruhusu ujenzi wa uzio uweze kukamilika kwa Wakati.
Mapema meneja wa mradi wa ujenzi wa uzio huo
Bw. Frederick Nkya, alimueleza MakamO wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kwamba hadi
sasa tayari asilimia 73 ya ujenzi huo imeshakamilika.
Hata hivyo amesema changamoto kubwa
inayowakabili ni eneo la mita elfu tatu na mia moja ambapo sehemu kubwa ya eneo
hilo bado wananchi hawajalipwa fidia.
Amefahamisha kuwa hadi sasa eneo la mita elfu
mbili na mia saba ndilo ambalo halijafanyiwa tathmini kuweza kuwalipa wananchi
walioko katika maeneo ya mradi huo.
Miradi ya ukarabati na ujenzi wa njia za
kupitia ndege wakati wa kuruka (Taxiway) pamoja na sehemu ya maegesho ya ndege
(Apron) katika uwanja huo inafadhiliwa na Benki ya Dunia pamoja na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar, ambapo mradi wa ujenzi wa uzio wenye urefu wa mita
11,690 katika uwanja huo, unatekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar pekee, ambapo zaidi ya shilingi bilioni sita zitatumika hadi
kukamilika kwa mradi huo.
AKIZUNGUMZIA mradi wa ujenzi wa jengo jipya la
abiria meneja wa mradi huo NDUGU Ibrahim Zhang amesema KUWA ,kazi hiyo sasa
inaendelea vizuri.
Mradi wa ujenzi wa jEngo jipya la abiria awali
ulitiwa saini mwezi wa Septemba 2009 KATI ya Wizara ya Miundo mbinu na
Mawasiliano na Kampuni ya ujenzi ya Beijing Construction Engineering Group ya
China, lakini baadae serikali iligundua kuwa ukubwa wa jengo uliopendekezwa
mwanzo haukidhi haja.
HATA HIVYO KUFUATIA KASORO HIYO Serikali
ilikubaliana na mkandarasi kuongezwa ukubwa wa jengo kutoka mita 15,600 hadi
mita 17,800 kwa ongezeko la fedha dola za kimarekani milioni 11 nukta 8, na
kufanya gharama za mradi huo kufikia dola la kimarekani milioni 82 nukta 2.
No comments:
Post a Comment