DAR-ES-SALAAM.
Ubalozi wa Uingereza nchini umesema KUWA unakusudia
kufanya mabadiliko ya utaratibu wa maombi na utoaji viza kwa Watanzania
wanaotaka kwenda nchini Uingereza kwa kufungua ofisi zitakazotoa huduma hiyo Mjini
Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa masuala ya viza ya Uingereza kwa nchi
za Afrika Kashif Chaudry, amesema AMEYASEMA HAYO MJINI Dar es Salaam ambapo
ameONGEZA KUWA wanakusudia kuanza
kulipia huduma hiyo kwa njia ya simu za mkononi.
Chaudry amesema kupitia utaratibu huo mpya, maombi yote ya viza sasa yatakuwa yaKIfanyika nje ya jengo la ubalozi na kutaja eneo moja Mjini Dar es Salaam kuwa ndiKo ambako watu wanaweza kuomba na kupata viza za kuingia nchini Uingereza.
Amelitaja eneo hILO kuwa ni katika jengo la Viva Towers lililopo katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi Mjini Dar es Salaam na kwamba hatua hiyo inalenga kupunguza usumbufu kwa watu wanaoomba kibali cha kuingia Uingereza.
No comments:
Post a Comment